Vatican News
Sanda Takatifu:Sanda Takatifu: Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki anawaalika wote kushiriki sala mbele ya Sanda kwa njia ya mitando ya kijamii Jumamosi Kuu 11 Aprili Sanda Takatifu:Sanda Takatifu: Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki anawaalika wote kushiriki sala mbele ya Sanda kwa njia ya mitando ya kijamii Jumamosi Kuu 11 Aprili  

Jumamosi Kuu:Sala ya moja kwa moja mbele ya Sanda Takatifu huko Torino!

Jimbo Kuu Katoliki la Torino,Italia limetangaza kuwa Juamaosi Kuu,tarehe 11 Aprili saa 11.00 jioni majira ya Ulaya Askofu Mkuu Cesare Nosiglia ataongoza liturujia ya sala na kutafakari mbele ya Sanda Takatifu katika Kikanisa kidogo cha kuhifadhia.Tukio hili litaoneshwa moja kwa moja na televisheni na mitandao yote ya kijamii.

Na Sr. Angela  Rwezaula- Vatican

Jumamosi tarehe 4 Aprili 2020 saa sita kamili majira ya Ulaya, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki na Askofu wa Susa Cesare Nosiglia, kwa kupitia mitandao ya kijamii, ametangaza kuwa Jumamosi tarehe 11 Aprili 2020 saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya ataongoza sala na kutafakari mbele ya Sanda Takatifu katika Kikanisa ndani ya Kanisa Kuu hili ambapo Sanda hiyo imehifadhiwa. Kipindi hicho cha sala na tafakari, kitaonyeshwa mubashara, iwe televisheni na majukwaa yote ya mitandao ya kijamii. Mwisho wa sala ya moja kwa moja, katika televisheni, mitandao ya kijamii majadiliano na tafakari vitaendelea na hotuba mbalimbali za wataalam na sauti za mashuhuda kwa kipindi kilichopo.

Upendo wa Yesu ambao alitoa maisha yake kwa ajili yetu ambayo tunaadhimisha wakati wa Wiki Kuu ni wenye nguvu ya kila matatizo, ya kila ugonjwa na kila ambukizo, kila jaribio na kila ukatishwaji tamaa. Hakuna na wala chochote ambacho kinaweza kututenganisha na upendo ambao ni mwaaminifu daima na unatuunganisha katika mafundo yasiyofunguka. Kwa njia ya maneno haya Askofu Mkuu Cesare Nosiglia ambaye ni mlinzi wa Kipapa wa Sanda Takatifu, ametaka kutoa tangaza kuhusu maombi maalum mbele ya Sanda hiyo. Aidha amesema maelfu na maelfu ya ujumbe umemfikia kutoka kwa watu, kuanzia wazee, watu wazima na vijana wenye afya na wagonjwa ambao wakiomba katika kipindi hiki kigumu cha matatizo makubwa tunayoishi, kuweza kusali katika Wiki Kuu Takatifu mbele ya Sanda ili kuchota kutoka kwa Kristo aliyekufa na kufufka na ambaye Sanda yake inawakilisha namna ya kweli na ya dhati, ile neema ya kushinda ubaya kama alivyoshinda yeye, kwa kuamini katika wema na huruma ya Mungu.

Askofu Mkuu anabainisha kupokea kwa shauku kubwa maombi na kuwahakikishia wote juu ya kufanya hivyo Jumamosi Kuu mchana saa 11 kamili mbele ya Sanda hiyo. Kuanzia muda huo yeye binafsi atakaa mbele ya Sanda Takatifu kusali na kutafakari. Anatoa shukrani kwa vyombo vya habari kama televisheni na mitandao ya kijamii katika muda  huo wa kutafakari  utakaowawezesha wote katika dunia nzima kukaa mbele ya Picha hiyo Takatifu, ambayo inatukumbusha mateso na kifo cha Bwana, lakini hata kutfungua mioyo yetu katika imani ya ufufuko wake.

Upendo una nguvu. Ndiyo tangazo la Pasaka ambalo Sanda Takatifu liinatuonyesha na kutufanya tuishi na kujazwa mioyo yetu katika utambuzi na imani amesema ì Askofu Mkuu. Papa Francisko katika ujumbe wake wakati wa fursa ya kuweka  Sanda Takatifu kunako mwaka 2013 alitueleza kuwa,  hiyho  siyo sisi tunaotafakari  Sanda, ikionyesha picha yenye macho yaliyofumba kutokana na kifo. Bali ni yule anayetutazama sisi na kutufanya tutambua ule upendo mkubwa aliokuwa nao kwa ajili yetu na kutuondolea dhambi na kifo. Uso huo unazungumza katika mioyo yetu na kututangazia habari kubwa ya amani ambayo ni kama vile anasema “kuwa na imani, usipoteze matumaini, nguvu ya upendo wa Mungu na Mfufuka mshinda yote”.

Kwa kuhitimisha Askofu Mkuu Nosiglia amesema :“Wapendwa mliotawanyika ulimwenguni kote, ninawasubiri Jumamosi ijayo saa 11.00 jioni ili kuinua kwa Mungu kwa njia ya kutafakari kwa kina mbele ya Sanda kwa sauti ya  sala ya pamoja kwa Mwanae Yesu, kaka na mwokozi. Moyo wetu daima urudie kusema “hima hima katika Sanda, upendo una nguvu!! Hata hivyo tukumbukue kwamba onyesho  maalum la Sandakwa umma  lilikuwa tayari limepangwa katika toleo la 43 la Mkutano wa Kimataifa liliondaliwa kuanzia tarehe 28 hadi Mosi 2021 la Jumuiya ya kiekumene ya Taize huko Torino.

04 April 2020, 15:59