Ili kuendelea na mafundisho ya elimu kwa watoto na vijana na katekesimu wakia nyumbani kimeundwa kikundi cha ubunifu. Ili kuendelea na mafundisho ya elimu kwa watoto na vijana na katekesimu wakia nyumbani kimeundwa kikundi cha ubunifu. 

ITALIA #coronavirus:Katekesi na ushauri wa mafunzo ya kielimu katika kipindi hiki!

Ushauri,katekesi,msaada kwa ngazi ya kielimu na kichungaji, pendekezo lililotolewa na kikundi cha ubunifu ambacho kinataka kujikita kutoa masaada wa kuondoa upweke binafsi na kijamii uliosababishwa na janga la Virusi vya corona nchini Italia.Suala hili linawahusu wahudumu wote wa kichungaji,makatekista,viongozi wasimamizi wa maparokia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ushauri, katekesi, msaada kwa ngazi ya kielimu na kichungaji, ndiyo pendekezo lililotolewa na kikundi cha ubunifu ambacho kinataka kujikita kutoa  masaada  wa kuondoa upweke binafsi na kijamii uliosababishwa na janga la Virusi vya corona nchini Italia.  Suala hili linawahusu wahudumu wote wa kichungaji, makatekista, viongozi wasimamizi wa maparokia ambao wanataka kuendeleza uhusiano wao wa kielimu na vijana wao ambao wako majumbani mwao kufuatia na janga hili la kimataifa.

Kipindi cha Kwaresima mwaka huu

Kwa mujibu wa barua ya kuwakilisha mpango huu inasema “Ni kwaresima ngumu mwaka huu ambayo haijawahi kuonekana namna hiii na ambapo inahitaji kufanya sadaka nyingi za kujitolea na kujinyima. Kipindi hiki ambacho ni vigumu kukutana binafsi  lakini bado kinafungua njia mpya za mawasiliano, majadiliano na kuelimisha katika nyanja ya elimu na hivyo kikundi cha ubunifu kinataka kutoa mchango wake wa bure kwa ajili ya maparokia, majimbo  na taasisi zote za  nyumba za Maisha ya Kitawa.

Mpango huo unaitwa creativ E- Academy

Mpango wake uliopewa jina la Creativ E-Academy, umefikiria kupanua na kuweza kupita bila kikwazo mipango iliyopo, vizingiti na umbali kwa kuamini kuwa ubunifu huo ni kwa ajili ya wema wa wote na zaidi wa maisha binafsi  hata kitaaluma. Moja ya utume huu ni kuwasindikiza na kukabiliana kwa pamoja katika kuunda mipango mipya na mitindo ambayo inafaa ili kuifuatilia kwa umbali katika kuwasaidia kuwa na tafakari ya kiroho au kielimu msingi kwa kupitia maparokia yao  na wahudumu wote wa kichungaji.

Inawezekana kuomba ushauri wwote na kushiriki mchakato wa mafunzo ya elimu

Inawezekana kwa namna hiyo hata kuomba ushauri, kushiriki mchakato wa mafunzo ya elimu na makatekista wanaweza kuendelea  kuendesha makundi yao ya vijana bila kuacha katekisimu au shughuli mbambali zenye uhusiano wa kielimu na kwa njia hiyo umbali unakuwa karibu ili kukabiliana na dharura hii na kufanya kila njia ili shughuli za kichungaji zisisimame. Kikundi hiki cha ubinifu, kinapendekeza  hata kuwasaidia familia kuendelea na mafundisho ya elimu na kiroho.

03 April 2020, 11:29