Vatican News
2020.04.26 Samuel Zan Akologo,Katibu Mkuu wa  Caritas nchini Ghana 2020.04.26 Samuel Zan Akologo,Katibu Mkuu wa Caritas nchini Ghana  

Ghana#coronavirus.Huduma ya Caritas kwa ajili ya maskini zaidi itaendelea!

Huduma ya Caritas nchini Ghana itaendelea kujibu mahitaji ya maskini na wengi wenye mazingira magumu walioshambuliwa na janga la virusi vya corona,hata baada ya kumalizika karantini.Haya yamethibtishwa na Katibu Mkuu wa Caritas nchini Ghana Bwana Samuel Zan Akologo,aliyetajwa katika tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Afrika Kanda ya Magharibi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa kiungo muhimu cha Kanisa katika kutoa msaada amebanisha kuwa Caritas nchini Ghana itendelea kutoa jibu kwa dharura ya maskini na watu wenye mazingira magumu ambao wameshambuliwa na janga la corona hata baada ya kuhitimisha hata hizo za karantini zilizowekwa kwa mujibu wa kiafya. Bwana  Samuel Zan Akologo, aliyetajwa katika tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Afrika wa  Kanda ya  Magharibi (Recowa-Cerao), amebainisha kuwa, lengo lao ni kuedelea na jithada kwa ajili ya masikini hasa wale ambao  kwa namna ya pekee wamekumbwa na hali halisi ya kutengwa kijamii katika muktadha wa dharura ya kiafya.

Akiwaalika wote kuwa na uwajibikaji wa kizalendo wa kuheshimu miongozo iliyotolewa kuhusiana na kuzuia maambukizi, kiongozi huyo wa Caritas amewashauri watu kuwa na matumaini na mshikamano ambao ndiyo silaha kubwa inayoweza kushinda hofu na hisia mbayo ipo katika kipindi hiki kigumu cha kihistoria.

Zaidi ya waathirika wa virusi vya corona, Caritas nchini Ghana ina wasiwasi hata juu ya mlundikano wa watu uliosababishwa na kubomolewa kwa nyumba zilizojengwa bila vibali hivi karibuni katika maeneo Old Fadama, kitongoji cha Accra, katika jiji kuu la Ghana. Wiki ya hivi karibuni amesisitiza Bwana Akologo, kuwa Caritas iliorodhesha zaidi ya familia 150 waliorundikana na wenye kuwa na  mahitaji ya dharura ya kibinadamu. Na hii amsisitiza ni misaada ambayo imeongezwa kwa maana hiyo hata kwa watu walio tenga  kutokana na maambukizi na kwa wale wote wanaotaka kurudi kwenye jamuiya  zao mahalia.

Kwa mujibu wa takwimu za tarehe 23 Aprili, nchini Ghana kulikuwa  na kesi chanya zipatazo 1,154 za Covid-19'  na 120 walipona na vifo tisa. Wakati huo huo, mkuu wa nchi, Nana Akufo-Addo, tangu Aprili 20 aliondoa marufuku ya harakati za kutengwa katika eneo la mji mkuu wa Accra na Kasoa,na katika eneo la mji mkuu wa Kumasi na wilaya zake zinazoungana, akisisitiza kwamba nchi ina uwezo wa kukabiliana na janga na hatua muhimu za usafi. Lakini ni uamuzi ambao Caritas inauona kuwa na ugumu wake, wakihofia kwamba inawezekana  kuchangia kuenea kwa maambukizo mapya.

25 April 2020, 16:11