Vatican News
Viongozi wa dini na serikali walaani kitendo kibaya cha kushambulia nyumba ya mkuu wa kiyahudi Jijini New York, Marekani Jumamosi 27 Desemba 2019 na kujeruhiwa watu watano Viongozi wa dini na serikali walaani kitendo kibaya cha kushambulia nyumba ya mkuu wa kiyahudi Jijini New York, Marekani Jumamosi 27 Desemba 2019 na kujeruhiwa watu watano  (ANSA)

Shambulizi la nyumba ya mkuu wa Kiyahudi jijini New York!

Kardinali Dolan amesema shambulizi la kigaidi katika nyumba ya Mkuu wa Kiyahudi jijini New York ni kitendo cha kuchukiza na cha dhuluma kinachokwenda kinyume na imani.Aidha viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo hata Bwana Donald Trump analaani tendo hilo la kinyama huku akiomba kuwa na umoja ili kupambana na kuweza kuondoa janga baya na kukemea ubaguzi huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni kitendo cha kuchukia na dhulima dhdi ya kaka na dada zetu Wayahudi. Ndiyo Maneno ya Askofu Mkuu katoliki wa Jijini New York, Kardinali Timothy Dolan, alivyo fafanua kuhusu shambulizi la nyumba ya Mkuu wa Kiyahudi Chaim, Rottenberg huko  Monsey lililotokea Jumamosi jioni wakati wanaadhimisha sikukuu ya Hanukkah. Watu watano wamejeruhiwa na wawili wako katika hali mbaya na kati yao kuna hata mtoto wa Mkuu wa Jumuiya ya Kiyahudi. Mhalifu wa tendo hilo anaitwa Grafton E. Thomas, ambaye ameshikiliwa na vyombo vya usalama kabla  kabla ya kufikishwa mahakamani kwa  kesi ya madai ya kujaribu mauaji.

Hili ni moja ya ya shambulizi la mwisho kati ya mashambulizi mengi dhidi ya Jumuiya ya kiyahudi ambayo yanapaswa kuhukumiwa bila kubakiza kwa sababu yanakwenda kinyume na imani inavyowakilishwa, amesisitiza Kardinali. Aidha amesema  “chuki haina nafasi katika mji wetu, serikali yetu  na taifa letu, au mahali pengine popote kwenye sayari yetu.” Kardinali Dolan ameelezea wazi wazi kuwa “shambulio kwa mtu yeyote au kikundi kwa sababu ya imani yake ya kidini ni shambulio dhidi yetu sisi sote” Aidha katika misa ya Jumapili  29 Desemba 2019 aliyoongoza mwenyewe, maombi  maalum yalielekezwa kwa waathirika ili kuelezea mshikamano na kupinga chuki na kutenda kwa makusudi mahali  popote inapotokea.

Naye Rais wa Marekani Bwana Donald Trump ni siku ya Jumapili Mchana alipoandika katika Tweter yake kuhusiana na janga akiomba kuwa na umoja ili kupambana na kuweza  kuondoa janga baya na kukemea ubaguzi huo.

Naye Gavana wa serikali ya  New York, Bwana Andrew Cuomo, wakati akitoka katika nyumba ya mkuu wa Kiyahudi alisisitiza kwamba shambulio hilo pia limechochewa na hali ya kukosa uvumilivu ambao unatawala nchini humo, kwa hasira inayolipuka na  kwa chuki,  ushahidi wote wa uwepo wa “saratani” katika siasa za Marekani. Amebainisha.

30 December 2019, 14:54