Vatican News
Ni lazima kukumbatia teknolojia mpya kwa ajili ya kutangaza Neno la Kristo kama wale ambao tutatakiwa kutangazia hata juu ya paa! Ni lazima kukumbatia teknolojia mpya kwa ajili ya kutangaza Neno la Kristo kama wale ambao tutatakiwa kutangazia hata juu ya paa! 

Papua New Guinea:teknolojia mpya ni kama chombo cha kuhubiria juu ya paa!

Mabadiliko endelevu ya vyombo vya habari na mazingira ya mawasiliano yanahitaji njia madhubuti ya Kanisa ili iweze kubaki karibu na watu.Ni kwa mujibu wa Bi Agatha Ferei Furivai mlei mkatoliki na Rais wa Sigins wa kanda ya Pasifiki na Mkurugenzi wa Caritas huko Fiji Papua New Guinea ,kandoni mwa Jukwaa kuhusu Elimu ya Utume wa Kimisionari iliyofanyika hivi karibuni nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya Mwezi Maalumu wa Kimisionari Bi Agatha Ferei Furivai, mlei mkatoliki na Rais wa Sigins kwa upande wa Kanda ya Pasifiki na Mkurugenzi wa Caritas huko Fiji, Papua New Guinea amesema kuwa, teknolojia mpya ni kama zana kwa ajili ya kuhubiri juu ya paa. Amesema hayo kandoni mwa Jukwa lililokuwa linahusu "Elimu ya Utume wa Kimisonari"  na kwamba mabadiliko endelevu ya vyombo vya habari na mazingira ya mawasiliano yanahitaji njia madhubuti ya Kanisa ili iweze kubaki karibu na watu.

Mawasiliano kati ya watu yamebadilika sana

Bi Furivai akifafanua zaidi amesema kwamba, mawasiliano binafsi kati ya watu yamebadilika sana katika miaka ishirini ya mwisho. Vizazi vipya vinatengenezwa na wenyeji wa kidijitali na wana ufundi zaidi wa kiteknolojia, japokuwa ni watu wanaoendelea kwenda mbali kutoka katika mawasiliano ya moja kwa moja, yaani ya uso kwa uso katika familia na jamuiya! Kwa maana hiyo wazazi, babu na bibi, wazee wa jumuiya na wale wote ambao wanamajukumu hasa katika utunzaji na makuzi ya watoto, ni lazima waweze kutembea bega kwa bega na watoto wao! Maneno hayo muhimu ya Bi Agatha Ferei Furivai yalisikika kandoni mwa Jukwaa la Elimu ya Utume wa Kimisonari iliyokuwa inaongozwa na mada ya “Utume wa kimisionari katika enzi za vyombo vya habari na mawasiliano ya papo hapo”. Jukwaa hilo liliandaliwa siku zilizopita wakati wa Mwezi Maalumu wa Kimisionari Okotba 2019 katika Taasisi ya Kitaalimungu Katoliki huko Bomana, nchini Papua New Guinea.

Umuhimu wa kurudi katika mahusiano ya kweli

Hata hivyo suala la kurudi katika mahusianoa  halisi  lilikabiliwa na Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe kwa ajili ya Siku ya Mawasiliano ya Kijamii  duniani  2019 ambapo anasisitiza kuwa, haitoshi kuzidisha viunganisho eti kwa sababu kuongeza  uelewano badala yake alitoa mwakiko wa kujenga Kanisa la kweli mahali ambapo anasema umoja hauna maana ya neno la  "like", lakini ni kuhusu ukweli wa dhati juu ya imani ambayo kila mmoja anatakiwa kuwa ni Mwili wa Kristo kwa kuwapokea na kuwakaribisha wengine. Katika mapendekezo hayo Mkurugenzi wa Caritas wa Fiji amesema: Katika utamaduni mpya uliojikita na uwepo wa compyuta binafsi, Kanisa linaweza kutoa ujumbe wake  duniani kote, kusikiliza kwa uwazi sauti ya maoni ya umma na kuingia katika mijadala ili kutafuta suluhisho la pamoja la matatizo mengi ya dharura ya wanadamu. Ni lazima kukumbatia teknolojia mpya kwa ajili ya kutangaza Neno la Kristo kama wale ambao tutatakiwa kutangazia juu ya paa, amesisitiza.

Utume wa waamini walei ni safari ya uhusiano binafsi

Bi Furivai akitamaza  kwa ndani juu ya suala la utume, anasema: “utume wa waamini walei ni safari iliyo na uhusiano binafsi na ili kujua Kristo kwa wengine. Katika safari hiyo tunaweza kutumia zana za mawasiliano ya  vyombo vya habari ili kuongezea sauti zetu”. Aidha amebainisha kuwa, hata katika eneo lao la Pasifiki wameweza kuweka majukwaa ya mitandao ya kijamii kama mtindo wa mawasiliano na huku akiwaalika kutumia vyombo hivyo kwa ajili ya kupanua mpango wa kimungu aliye Muumba wetu na kueneza Neno la Mungu. Na kwa kuhitimisha anasema: “ Sisi sote ni watumiaji na wazalishaji wa ujumbe ambao ukatisha katika mzunguko wa mawasiliano. Hii ni sababu nzuri kwa ajili ya jitihada za kushirikiana kati ya Kanisa na vyombo vyote vya habari.

Msisitizo juu ya siku ya Mawasiliano duniani 2019

Ikumbukwe kwamba: Siku ya Mawasiliano duniani 2019, imeongozwa na kauli mbiu kutoka katika maneno ya Mtakatifu Paulo kwa Waefeso yasemayo: “kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine (Ef 4,25). Kutoka katika jamii hadi Jumuiya” kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko alichagua kauli mbiu hiyo akitaka  kusisitizia umuhimu wa kurudisha mawasiliano katika mantiki pana zaidi ambayo ni msingi wa mtu na msisitizo wa thamani ya mwingiliano unaolenga mazungumzo daima  kama fursa ya kukutana na mwingine!

04 November 2019, 16:05