Maaskofu katoliki nhini Ghama wamefanya mkutano wao wa Mwaka huku wakikabiliana na changamoto za sasa zinazoikabili nchi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira,ufisadi na uharibifu wa mazingira Maaskofu katoliki nhini Ghama wamefanya mkutano wao wa Mwaka huku wakikabiliana na changamoto za sasa zinazoikabili nchi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira,ufisadi na uharibifu wa mazingira 

Maaskofu nchini Ghana mbele ya changamoto za sasa!

Kati ya changamoto zilizo kuwa kiini cha Mkutano wa mwaka hivi karibuni wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini Ghana ni ukosefu wa ajira kwa vijana,unyonywaji wa mali za asili,ukataji hovyo wa misitu,ufisadi,umaskini na ukosefu wa usawa,wa usalama na uhalifu uliotapakaa.Kwa uchaguzi mkuu 2020,wanaomba mchakato uwe wa kweli pia maaskofu wanapinga mitaala ya shule ya kitaifa kuingiza kozi ya masomo ya ngono.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu wa Ghana wanaonesha msimamo wao  madhubuti wa kupinga kuingizwa katika mitaala ya shule  kitaifa  kozi za masomo ya ngono (Comprehensive Sexual Education - Cse) ambayo inahamasisha utamaduni wa mashoga (Lgbt). Hata hivyo Rais Nana Akufo-Addo  alikuwa tayari amethibitisha kuwa serikali yake haina nia ya kupitisha mpango kama huo na kuibua maandamano ya upinzani katika nchi yake, japokuwa maaskofu wanaomba hali hiyo iwe pia ni  wakati wa ujao na kwamba serikali ibaki kidete bila kuyumba.  

Raia wanahimizwa kuzingatia maadili na thamani katika mtindo wa maisha

Hayo yote yanaonekana katika waraka wa mwisho wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu nchini Ghana uliofanyika hivi karibuni huko Elmina, Jimbo Kuu katoliki la  Cape Coast, ambapo wanabainisha kuwa uchochezi hai wa maandamano dhidi ya kuingiza mtaala wa kozi ya mafunzo ya ngono, umeonesha wazi wazo la kitu gani kinaweza kujitokeza iwapo sera za kisiasa zinapendekeza kutoa nje bila kuwashirikisha wazalendo husika. Na kwa maana hiyo maaskofu wanainyoshea kidole dhidi ya mashirika ya kimataifa ambayo yanazidi kuhamasisha mitindo ya maisha tofauti na thamani za utamaduni wa asili wa dunia nzima na kwa haki ni thamani za utamaduni na maadili nchini Ghana.

Nafasi kubwa ya changamoto za sasa za uchumi na kijamii nchini  Ghana

Katika kiini cha mkutano ambacho kiliongozwa na mada ya “Utume wa Kanisa nchini Ghana leo hii”, kiliwaongoza zaidi hasa  katika mtazamo wa Maadhimisho ya Miaka 100  tangu kuandikwa  Waraka wa Kitume wa “Maximum Illud” wa Papa Benedikto XV, ambapo Baba Mtakatifu Francisko alipendelea kuuenzi kwa njia ya kutangaza Mwezi Maalum wa Kimisionari mwezi Oktoba uliopita! Aidha nafasi kubwa ya kazi yao kwa maaskofu katika Mkutano wao wa Mwaka imejikita katika kutazama na kutafuta namna ya suluhisho la changamoto za sasa za uchumi na kijamii nchini Ghana.  Changamoto, wanabanisha zinatokana na kwenda sambamba na ukosefu wa dhamiri nyoofu ya thamani za Kiinjili na mbazo zinajenga msingi wa jamii inayotarajia na kuelekeza maono kwa Mungu.

Kati ya mambo hayo kwa namna ya pekee maaskofu wamejikita  pia juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana, unyanyaswaji wa katika rasilimali za asili za nchi, ukataji hovyo wa misitu, ufisadi, umaskini na ukosefu wa usawa unaozidi kuongezeka katika nchi , ukosefu wa usalama na uhalifu uliotapakaa kila kona.  Licha ya utambuzi wa maendeleo na jitihada za Serikali kwa namna ya pekee juu ya kukabiliana na madeni ya fedha na katika kambi za elimu na afya, lakini maaskofu wa Ghana wanataka matendo yawe hai na  kuchukua uamuzi wa dhati kwa upande wa serikali.

Maaskofu wanaomba mchakato wa uchaguzi uwe wa dhati na wa kidemokrasia

Hatimaye katika Waraka wao wa mwisho  wa Mkutano wanatazama  suala la uchaguzi mkuu  kwa namna ya pekee  uchaguzi  wa Rais na wabunge mwaka 2020, mahali ambapo raia wa Ghana watatakiwa kufanya kura ya maoni. Katika pendekezo hilo Maaskofu wanatoa wito kwa raia wote ili kuchangia kwa sababu uchaguzi uweze kuwa na mchakato wa dhati na wa kidemokrasia huku wakijaribu kuwa makini wa kukataa kura za mabadilisho, zenye kuleta hatari, ghasia fujo, udanganyifu na kutukanana hovyo.

MAASKOF GHANA
23 November 2019, 10:23