Vatican News
Congo; Wataalam wa afya wakifanya utafiti kwa mgonjwa anayefikiriwa kuwa na ugonjwa wa Ebola Congo; Wataalam wa afya wakifanya utafiti kwa mgonjwa anayefikiriwa kuwa na ugonjwa wa Ebola  

Congo; Askofu Ngumbi: asema "muwaamini madaktari wa afya"

Askofu Willy Ngumbi Ngenele wa Jimbo Katoliki la Goma lililoko nchi ya Congo DRC ametoa mwaliko wa kuwaamini madaktari wa Afya pamoja na Tume yao ili kuepuka maambukizo zaidi ya ugonjwa wa Ebola.Ujumbe huo umetolewa katika mkutano wa jumuiya za kidini juu ya elimu ya afya, chanjona na tafiti za tiba ya magonjwa hatarishi unaoendelea kufanyika nchini Congo.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Jumuiya za kidini mnamo tarehe 23 Septemba, 2019, zimetoa rai kwa jamii nzima nchini Congo kuwaamini madaktari wa afya. Ujumbe huo umetolewa na Askofu Willy Ngumbi Ngenele Askofu wa Jimbo Katoliki la Gomalililoko mashariki mwa nchi ya Congo, na kutumwa  kwa Shirika la kimataifa la kimisionari (Agenzia Fides),  katika maadhimisho ya jubilee ya elimu ya afya juu ya tafiti za tiba ya magonjwa hatarishi, umesisitiza kujenga imani kwa watalaam wa afya pamoja na Tume yao. Askofu Goma amewashawishi wananchi kuwa na imani kwa madaktati wa afya pamoja na Tume yao ya utafiti ili waweze kutumi dawa wanazopewa. Askofu Willy Ngumbi Ngenele Goma amewatahadharisha kuwa bila kuwa na imani na watalaam wa afya idadi kubwa ya watu watakumbwa na ugonjwa huo. Hivyo ili kuweza kunusuru sehemu kubwa ya watu, lazima watu washirikiane na watalaam katika utumiaji wa dawa wanazopewa. 

Askofu Willy Ngumbi Ngenele, ameeleza nia njema ya Tume ya Watafiti wa Afya wanaojiandaa kufanya chanjo ya pili dhidi ya ugonjwa wa Ebola kuanzia mwezi Oktoba, 2019. Kutokana na uzoefu walioupata kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini Sierra Leone wangependa kuchukua tahadhari kubwa na Kanisa linao wajibu wa kuhamasisha jamii ili kuikoa na janga hilo linalohatarisha afya za watu. Kanisa likiungana na Shirika la Afya Duniani, WHO, linapenda kuwataarifa kuwa hadi kufikia tarehe 9 Septemba, 2019 idadi ya waathirika ilikuwa imefikia watu zaidi ya elfu tatu (3,000) na waliokwishapoteza maisha ni zaidi ya watu elfu mbili na sabini (2,070) takwimu hizi zinaifanya inchi ya Congo kuwa ya pili katika historia kwa kuathirika na ugonjwa wa Ebola.  Mwishoni, Askofu Willy Ngumbi Ngenele, amewalika Taifa la Mungu kushirikiana wa watalaam wa afya ili kuweza kuokoa afya zao.

 

02 October 2019, 10:49