Hivi karibuni umefanyika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume ACWECA wa nchi za AMECEA ambapo  Sr. Cecilia Njeri, rais wake amesisitizia malengo ya mkutano huoo Hivi karibuni umefanyika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume ACWECA wa nchi za AMECEA ambapo Sr. Cecilia Njeri, rais wake amesisitizia malengo ya mkutano huoo 

ACWECA:majiundo katika uongozi wa Mashirika ya kitawa ni muhimu!

Shirikisho la Mashirika ya kitawa ACWECA ya nchi za AMECEA,pamoja na mambo mengine waliyo nayo,wanaunga mkono Wosia wa Baba Mtakatifu wa Laudato Si,kuhusu utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja katika nyanja kuu nne:Malezi na utume,Familia na Utume wa Vijana,Haki,Amani na Uumbaji fungamani na Maendeleo ya Taasisi.

Na Padre Angelo Shikombe –Vatican

Shirikisho la Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume katika Nchi za AMECEA, ACWECA, yaani Afrika Mashariki  lililoanzishwa kunako mwaka 1974 na kwa sasa linawajumuisha Watawa wa kike zaidi ya 20, 000. Shirikisho hili ACWECA pamoja na mambo mengine mengi waliyo nayo, wanaunga mkono Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato si, kuhusu utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya  pamoja katika nyanja kuu nne:Malezi na utume, Familia na Utume wa Vijana, Haki, Amani na Uumbaji fungamani na Maendeleo ya Taasisi. Hatua hii kubwa imeelezwa katika maandalizi ya Mkutano wa 18 wa Shirikisho la Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume (ACWECA) katika Nchi za AMECEA, yaani za Afrika Mashariki..

Naye Rais wa Shirikisho la Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume Sr. Cecilia Njeri, (LSOSF), ametoa mwaliko huo tarehe 31 Agosti 2019, akieleza kuwa sehemu kubwa ya maandalizi ya mkutano wa Shirikisho la watawa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mkutano wa 17 uliofanyika Agosti 2017 Dar es Salaam, Tanzania kukamilika. Aidha Sr. Cecilia ametoka kifua mbele akidadavua kuwa, Mkutano wa 17 ndio uliozindua mkakati wa miaka mitano yaani kuanzia 2017 hadi 2022 wenye lengo la kuiwezesha sekretarieti kujiendeleza ili kuwa na uwezo mkubwa inavyotakiwa.  Sekretarieti wakishirikiana na wajumbe kutoka Shirikisho la Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume (ACWECA) wamekuwa na malengo makuu manne: Majiundo na Umisionari, Familia na Utume wa Vijana, Haki, Amani Maendeleo fungamani ya watu na viumbe.

Majiundo katika uongozi wa Mashrika ya kidini ni muhimu

Katika kuendeleza umoja wao (ACWECA) watawa hawa wanahisi kwamba majiundo katika uongozi wa Mashirika ya kidini ni wa muhimu. Hivyo wameunda mfumo wa uwezeshaji katika uongozi wenye kujenga vinasaba na ufahamu wa viongozi ili uweze kuwa na ufanisi zaidi.  Katika kupambanua maada hiyo Sr. Cecilia amesema kwamba katika maisha ya kitawa, watawa wengi wanaopungukiwa vinasaba na mbinu za uelewa, mara nyingi ndiyo wanaochaguliwa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali, hivyo wanahitaji kujengewa uwezo. Akiendelea kufafanua zaidi maada hiyo amesema, tangu mchakato huo uanze, Sekretarieti (ACWECA) imejikita katika kulea makundi mawili yanayojengewa uwezo. Moja likwa la  viongozi wapya waliochaguliwa katika ofisi mbalimbali za mashirika yao na la pili, ni kundi la wanaong’atuka katika madaraka.

Jitihada hizi zimepongezwa na mashirika yao. Aidha katika malezi na Utume Sekretarieti (ACWECA) imeandaa ufadhili wa tukio hilo ili kuwezesha  mkakati wa majuma sita ambayo Sr. Cecilia akiwa Mama Mkuu wa Shirika la Masista wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Assisi, umefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Sr. Secilia amesema, wamekuwa na watawa walioweza kufika kwa muda wa wiki tatu na kurudi tena kwa awamu nyingine ya majuma matatu. Hivyo, kuna haja ya kuandaa Watawa, kufadhili hizo warsha ndani ya maeneo yao, na kuhamasisha utendaji wa pamoja. Sr. Secilia amekiri kuwepo kwa warsha hizo kila mwaka.

Kazi ya ACWECA

Katika kufafanua zaidi juu ya kazi za ACWECA,amesema katika sekretarieti hiyo, watu wengi wameamshwa katika usingizi na kupewa vinasaba vya kujitegemea kiuchumi na hivyo wamefanya miradi mipya fungamani inayoshawishi viongozi kutumia raslimali zilizopo na kubuni mbinu mpya za utekelezaji makini.  Katika kusisitiza zaidi amesema, tunahitaji kujua namna ya kutegemeza Mashirika ya kitawa Barani Afrika, kwa kutumia rasilimali tulizonazo. Hivyo suala la mikakati ya kimalezi ambalo tumekwisha anzisha limo ndani ya wigo huo.  Aidha ufafanuzi wa  mahusiano ya familia na Utume wa Vijana, Sekretarieti (ACWECA) imeshirikiana na Shirika la kitaifa na kutoa ushawishi mkubwa ili kuwa na mikakati ya kifamilia na vijana.  Tunawashauri watawa kutembelea familia ili waweze kuelewa changamoto na matatizo ambayo familia zinakumbana nayo. Anakiri kuwa wako watawa wafanyakazi wa jamii na kazi yao ni kuwawezesha ili waweze kuendesha warsha mbalimbali za kifamilia.

Watawa wanahamasishwa kuwa bega kwa bega katika utume wa vijana

Kwa upande wa vijana amesema, tunawashauri Masista kujishirikisha na maisha ya Utume wa vijana katika mashule yanayoendeshwa na Kanisa Katoliki. Aidha Secretarieti (ACWECA) imeweza kuongoza mafunzo kwa Masista wa Haki, Amani na Uumbaji fungamano. Juhudi ambazo zimefanikiwa sana.  Sr. Secilia akihamasisha anasema, “Tuwawasihi Masista kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa Haki, Amani na uumbaji fungamano katika kujengeana umahiri”. Aidha kuunga mkono harakati za Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Laudato si, juu ya  utunzaji  bora wa mazingira Nyumba yetu ya pamoja. Hivyo anawasihi watawa wajibidishe katika upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira. Roho hii kwa hakika imeanza kukua katika mashirika yaliyo mengi ya kitawa!

03 September 2019, 11:50