Wasiwasi mkubwa wa maaskofu Burundi kuhusiana ndugu zao wakimbizi wanaoishi  nchi jirani: Congo DRC,Rwanda,Uganda na zaidi ya wakimbizi katika nchi ya Tanzania Wasiwasi mkubwa wa maaskofu Burundi kuhusiana ndugu zao wakimbizi wanaoishi nchi jirani: Congo DRC,Rwanda,Uganda na zaidi ya wakimbizi katika nchi ya Tanzania  

Wasiwasi wa Maaskofu nchini Burundi kuhusu ongezeko la mivutano ya kisiasa!

Katika hitimisho la Mkutano wa mwaka wa Baraza la Maaskofu nchini Burundi,wametoa ujumbe wakionesha wasiwasi wa nchi kwa ujumla katika mantiki za mivutano kisiasa inayosabisha hata vifo,janga la wahamiaji,dharura ya Malaria, kuelekea uchaguzi 2020,manyanyaso na mwezi wa Kimisionari kama kitovu cha mkutano huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika hitimisho la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Burundi ulioanza tarehe 4 na kumalizika tarehe 7 Juni huko Gitega, wametoa ujumbe wao ambao kwa hakika unaonesha  wasiwasi wa kuongeza kwa vurugu na ukosefu wa kutovumiliana kisiasa ambapo katika maeneo mengi ya nchi wanasema  wamesababisha mapigano hadi kufikia vifo.

Janga la wahamiaji

Mivutano ya kisaisa ambayo kwa miaka sasa inatingisha nchi, imelazimsisha wakimbizi zaidi ya 374.000  wa Burundi kukimbilia nchi zilizoko karibu na Burundi kama vile  Uganda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Rwanda na zaidi nchini Tanzania mahali ambapo wanahesabu ni zadi ya wahamiaji 192.000, walioko kwenye makambi na mbayo mara nyingi  yanakosa kila kitu hasa zaidi ukosefu wa usalama na mahitaji ya kibinadamu. Katika hali hii, Maaskofu wanathibitisha katika ujumbe wao kuwa: “tumekuwa na uchungu kufuatia na  ukosefu wa usalama  ambao unaoendelea kuwakumbwa watu wetu katika baadhi ya makambi nchini Tanzania.

Dharura ya Malaria

Kati ya matatizo ambayo yamekuwa pia na umakini wa Maaskofu wa Burundi  ni  kuhusu hatari ya malaria katika sehemu mbali mbali za Burundi na kama ilivyo pia matukio ya kijamii kama vile wizi makambini au katika familia, makundi ya yenye silazha, idadi nyingi za kesi za ushirikina ambao wakati mwingine wanasema  unafikia hata mauaji kwa wale wanaodhaniwa ni wachawi, vile vile janga  hata la  biashara mbaya ya wasichana katika baadhi ya maeneo.

Kuelekea uchaguzi 2020

Kuhusiana na suala la maisha ya nchi kwa ujumla, Maaskofu wa Burundi wamejadiliana kwa kiasi kukubwa juu ya hali ya siasa- kijamii kuhusiana na uchaguzi unaotarajiwa kufanyika 2020. Wametafuta kwa namna ya pekee kuchanganua ni mambo yapi Kanisa linapaswa  kuchangia katika mwanga wa utume wake  kwa namna ya kwamba upigaji kura uweze kuwa wa amani na kuhamasisha sababu kuu ya demokrasia.

Masuala ya Manyanyaso na mwezi wa Kimisionari ilikuwa ni kitovu cha mkutano

Hatimaye katika mpango wa Kanisa kwenye mchakato mzima wa Mkutano wao wa Mwaka, umesomwa  “Motu Proprio” ya Baba Mtakatifu Francisko  isemayo “Vos estis lux mundi” “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima” (Mt 5,14).  Uliotangazwa kunako tarehe 9 Mei 2019. Bwana wetu Yesu Kristo anaita kila mwamini awe mfano angavu wa fadhila fungamani na utakatifu. Sisi sote, kwa hakika tunaalikwa kutoa ushuhuda wa dhati wa imani katika Kristo, katika maisha kwa namna ya pekee katika uhusiano na jirani. Maaskofu pia wamejadili kuhusu maadhimisho ya Mwezi maalum wa Kimisionari unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 100 tangu kutangazwa kwa Waraka wa Kitume wa Maximum Illud, uliotolewa na Papa Benedikto XV kunako mwaka 1919 na ambao kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko ameomba kuutilia maanani katika matendo ya kimisionari.

12 June 2019, 15:24