Vatican News
Matunda yameanza kuonekana baada ya mwezi mmoja tangu kuhitimishwa kwa siku ya vijana duniani huko Panama 22-27 Januari 2019 Matunda yameanza kuonekana baada ya mwezi mmoja tangu kuhitimishwa kwa siku ya vijana duniani huko Panama 22-27 Januari 2019  (Vatican Media)

Panama:Askofu Mkuu Ulloa anasema hata wadogo pembezoni wameota ndoto!

Baada ya mwezi mmoja tangu kumalizika kwa Siku ya vijana duniani huko Panama iliyoanza tarehe 22-27 Januari 2019, Askofu Mkuu Ulloa wa Jimbo Kuu katoliki Panama anatoa maelezo mafupi ya urithi wa Baba Mtakatifu aliouacha katika kizazi cha Amerika ya Kusini na kwa namna ya pekee kwa vijana wa Panama

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baada ya Siku ya vijana Duniani wadogo na ambao wako pembezoni mwa jamii wanasimulia ni kwa jinsi gani waliweza kuota ndoto na kuonja huruma ya Mungu na Kanisa kwa njia ya mikono ya Baba Mtakatifu Francisko. Ni mwezi mmoja baada ya Siku ya Vijana huko Panama ambapo  vijana wote  bado wanaishi hali halisi ya amani, furaha na matumaini ambayo Baba Mtakatifu amecha kama urithi katika nchi ya Panama. Katikati ya watu  bado wanahisi kiukweli ukosefu wa hija hiyo maalumu na ambayo lakini haiwazuii kutoendelea kufanya shughuli zao kwa mwendelezo wa Siku ya vijana. Ndiyo maelezo ya Askofu Mkuu José Domingo Ulloa wa Panama mara baada ya mwezi mzima wa hitimisho la Siku ya Vijana Duniani 22-27 Januari. Amethibitisha hayo akizungumza nje ya Mkutano tarehe 19 Februari  ulioandaliwa Mjini Roma na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini katika Ubalozi wa Panama mjini Vatican, kwa kuongozwa na mada ya Kumbukumbu ya shukrani na jitihada za Siku ya vijana huko Panama.

 Shughuli ya kuendelea ni kufuata maelekezo ya Baba Mtakatifu

Na askofu anathibitisha kuwa sasa ni uwajibikaji wa kupeleka mbele kazi ambayo imeanzishwa na Siku ya vijana. Kazi hiyo ya Kanisa la Panama inajihusisha na wahusika wote na ambao zaidi ni walei na wanawake. Hata hivyo Askofu Mkuu Ulloa anathibitisha kwamba, maelekezo yaliyotolewa na Baba Mtakatifu kwa ishara zake na maneno yake, yameangaza hali halisi ya Panama na kanda nzima. Mtazamo wa Baba Mtakatifu Francisko ulijikita juu ya uchungu wa dunia kwa kutazama nyuso za vijana wengi wanaoteseka. Hata hivyo baada ya Mkutano  wa siku ya vijana Askofu anathibitisha wamekuwa na ukweli zaidi wa kuweza kuwapatia vijana wote na hasa wale ambao wanaishi pembezoni mwa ardhi yao,ikiwa ni watu wa asili,watu mchanganyiko na hali halisi iliyopo katika bara la Amerika ya Kusini.

Kulinda mazingira kwa mujibu wa maandiko ya Baba Mtakatifu Francisko katika Laudato Si

Kadhalika Askofu Mkuu Ulloa ameweza kubainisha juu ya matunda ya kwanza ya Siku ya vijana duniani ya kwamba ni kuundwa kwa tume ya kazi ya Kiispania na Amerika kwa ajili ya utafiti na kujifunza kwa kina waraka wa Mafundisho jamii ya Kanisa kwa upeo wake mkubwa,katika matendo na kuzaliwa kwa makanisa mahalia,ya makundi ya Parokia za kiekolojia ili kuhamasisha utamaduni wa kulinda mazingira kwa mujibu wa maandiko ya Baba Mtakatifu Francisko katika Laudato Si. Lakini pia mtazamo wa shughuli ya wakati ujao inayotazama kwa karibu Siku ya vijana kuanzia ijayo huko Lisbon mwaka 2022 ambayo inachota mawazo kutoka Panama.

Panama na Ureno ni nchi mbili zinazofanana kuwa na mchanganyiko wa watu

Panama na Ureno ni ardhi mbili zinazoungana au kufanana kwa njia ya uwepo wa mchanganyiko wa watu anabainisha Askofu Mkuu, kwa kukumbuka ukaribu wa nchi ya Ulaya na nchi za Afrika katika kielelezo cha lugha ya kireno , kama vile Angola, Capo Verde, Guinea na Msumbiji. Kwa njia hiyo anaamini kwamba, tangu wakati huu na baadaye Siku ya vijana duniani itajikita kwa kina kuwa na mtazamo katika hali halisi ambazo zinapaswa kujikita katika maono hayo si katika wazaliwa na watu wa asilia tu, lakini pia hata vipande vipande vya watu kama vile makabila ya warom na Wasinthi barani Ulaya.

20 February 2019, 16:06