Vatican News
Maaskofu wa Korea mbili katika Mkutano wao wamezungumzia juu ya uchungaji wa vijana na jinsi gani ya kueneza Ujumbe wa upendo wa Kristo kwa vijana wa leo Maaskofu wa Korea mbili katika Mkutano wao wamezungumzia juu ya uchungaji wa vijana na jinsi gani ya kueneza Ujumbe wa upendo wa Kristo kwa vijana wa leo 

Korea:Maaskofu wa Korea wajenga mkakati wa kichungaji!

Taarifa ya Mkutano wa Maaskofu wa nchini ya Korea ya Kusini na Kaskazini inathibitisha kuwa, Maskofu walioshiriki, walipata muda mwafaka wa kubadilishana, kushirikishana mafunzo na mkakati wa kichungaji katika Makanisa yote ya nchi mbili, kwa mtazamo wa suala la vijana na amani, kuanzia tarehe 13-15 Novemba

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mkutano wa 24 wa Maaskofu wa Korea na Japan uliofanyika katika Jimbo la Uijeongbu, Korea ya Kusini, kuanzia 13-15 Novemba 2018, wamezungumzia juu ya vijana, amani na changamoto za kichungaji katika kutangaza Injili. Askofu Pietro Lee Ki-heon, mahalia, amewapokea washiriki katika mkutano ambao kila mwaka wanaungana nchi hizo mbili ambazo kwa nyakati zilizopita wamepitia kipindi cha kihistoria chenye migogoro na uadui , kwa maana hiyo, kukutana huko iwe ni kama ishara ya undugu katika imani na kama utashi wa kujenga Kanisa moja ili liweze kuinjilisha katika Bara la Asia Mashariki ,

Katika mkutano wao wamepata fursa ya kushirikishana mafunzo na mkakati wa kichungaji

Taarifa ya Mkutano huo inathibitisha kuwa, Maskofu walioshiriki, walipata muda mwafaka  wa kubadilishana, kushirikishana mafunzo na mkakati wa kichungaji katika Makanisa yote ya nchi mbili. Katika ajenda yao kulikuwapo na majadiliano juu ya uwepo wa ujumbe wa kikristo katika nyakati za mapinduzu ya nne ya viwanda, yale ya tekonolojia, wakati  huo huo, siku ziliofuata walitilia mkazo juu ya uchungaji wa vijana na jinsi gani ya kueneza Ujumbe wa upendo wa Kristo kwa vijana wa leo, kuanzia na hitimisho la Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana , ambayo imemalizika hivi karibuni mjini Vatican.

Walikuwa wakivuta hewa ya hali nzuri ya mapatano kindugu na ushikirikiano

Kati ya maaskofu 23 wa Korea, kulikuwa na Kardinali Andrew Yeom Soo-jung, Askofu Mkuu wa Seoul na pia  kati ya maaskofu 18 wa Japan, kulikuwapo na Kardinali Thomas Aquino Manyo Maeda, askofu Mkuu wa Osaka. Na kwa mujibu wa taarifa kutoka habari za Kimisionari Fiedes, katika mkutano walikuwa wakivuta hewa ya hali nzuri ya mapatano kindugu na ushirikiano ambao unaonesha matumaini ya  wakati endelevu.

Maaskofu wa Korea na Japan wameanza kuunganika kwa pamoja tangu  mwaka 1996

Kutokana na jimbo la  Uijeongbu kuwa  karibu sana na mpaka wa Korea ya kaskazini, Viongozi hawa wameweza pia kufanya ziara katika Kijiji cha Panmunjom, mahali ambapo wanafanya mikutano ya kisiasa ya hali ya juu, na  kwa ngazi ya Viongozi wa Kaskazini na Kusini, ni eneo linalolindwa na wanajeshi, ambapo maaskofu wa Korea  wamewataka waendelee na mchakato wa amani na mapatano kati ya Korea ya kaskazini na Kusini. Maaskofu wa Korea na Japan wameanza kuunganika  pamoja kufanya mkutano tangu  mwaka 1996 ili kuhamasisha mahusiano ya pamoja kichungaji na kuanzisha mambo mengine mapya ya pamoja kwa ajili ya Kanisa na kwa jamii nzima ya binadamu.

17 November 2018, 15:31