Vatican News
Wito wa maaskofu wa Congo DRC ili watu waweze kupiga kura kwa uhuru, ulio na uwazi, amani na demokrasia katika nchi yao Wito wa maaskofu wa Congo DRC ili watu waweze kupiga kura kwa uhuru, ulio na uwazi, amani na demokrasia katika nchi yao 

DRC:maaskofu wanatoa wito ili uwazi na uaminifu uwepo katika kupiga kura ya Rais!

Katika hitimisho la Mkutano maalum wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (cenco), Maskofu wametoa ujumbe wao wenye wito wa kuweza kupiga kura kwa uhuru, ulio na uwazi, amani na demokrasia katika nchi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Uchaguzi unao aminika katika ukweli wa kidemokrasia ndiyo matashi mema ya kusubiri uchaguzi wa rais wa nchi ya Kidemokrasia ya Congo DRC, unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Desemba 2018, ambapo Maaskofu wanatoa tamko jipya katika wito mpya  ili upigaji kuwa uweze kufanyika kwa wazi, katika amani na uhuru kamili. Lengo lao ni kwamba katika  hali ya sasa ya siasa kijamii, haina uhakika na ndiyo maana katika ujumbe wao maaskofu wanaonesha jinsi gani walifanya mkutano wa dharura siku zilizopita ili kutazama masuala muhimu juu ya mchakato wa uchaguzi ambao umeanzishwa kwa mara nyingine tena katikati ya matatizo mengi mara baada ya kuuacha  uchaguzi huo mara kadhaa.

Uhuru katuka uchaguzi na amani bado havijaonekana

Maaskofu wanaandika kuwa, hakuna jambo linaweza kupotea iwapo kuna roho ya kupenda taifa na matashi ya kisiasa. Pampja na hayo , uhuru wa kuweza kuonesha hilo, bado haujawa na uhakika kwa wote, kwa maana wapo bado wapinzani mbalimbali wa Rais Kabira, wako ndani ya magareza au ni waomba hifadhi. Bila kuzungumzia juu ya usalama kwa ujumla, ambao katika hali halisi ya mipango ya amani inaonesha giza nene.

Hata hivyo katika ujumbe pia wmaaskofu wanaonesha juu ya janga la mlipuko wa Ebola Kaskazini mwa Kivu na pia kuwasili wa wimbi la wazalendo wa Congo waliofukuzwa nchini Angola. Katika mantiki hiyo, Maaskofu wanasisisiza kuwa ni vigumu kufikiria kwamba, uchaguzi unaweza kufanyaka katika hali ya uhuru kabisa na ambao unaweza kuwa na utashi wa kweli kwa watu. Japokuwa wanathibitisha kuwa siyo  kila kitu kinaweza kuptea iwapo kuna roho ya uzalendo na matashi mema ya kisiasa.

Kura iwe ya uwajibikaji

Katika ujumbe wao, maaskofu wanaorodhesha baadhi ya ushauri ambao watu wanaweza kufuata na  kwa maana hiyo, hawali ya yote wanasema , wapiga kura wawe na uhuru wa kupiga kura lakini kwa namna ya kuwajibika kwa ajili ya ustawi wa pamoja na kuwa na mtazamo dhidi ya wanasiasa wafisadi. Kwa kuhepuka wale wanaotaka kuuza uongo mtupu na kuadaa watu kwa ahadi za uongo, kwa maana hiyo watu wawe makini sana kwa mabadilishano ya hila hilo.

Pamoja na hayo katika ujumbe wao wanatoa wito kwa upya katika Tume ya Uchaguzi (Ceni) ambayo imetoa njia uhuru ya kuweza kutumia mfumo wa kieletroniki ambao ulikuwa umepingwa japokuwa una uhakika katika upihanji kura ili kuweza kutoa ule hali ile dhidi ya udanganyifu na matumizi ambayo itakuwa ni vigumu kwa wale wasio kuwa na elimu katika masuala ya kieletroniki . Katika suala hili, maaskofu wanatoa wito pawepo na dhamana zaidi ili kuwepo na udhibiti wakati wa kuhesabu kura.

Kufuatia Mkataba wa uliokuwa umewekwa wa tarehe 31 Desemba, maaskofu wanakumbusha kwamba wafuate sheria na makubaliano hayo, na ambapo katika hitimisho la ujumbe wao maaskofu wanathibitisha juu ya umuhimu wa siku hiyo ya uchaguzi kwa ajili ya wakati endelevu wa nchi yao kwamba: “ tunapaswa kujikita wote kwa namna ya kuzuia uongo wa uchaguzi ambao matokeo yake hayawezi kukubaliwa na wote na inawezekana kusababisha kungukia kwa kina katika vurugu zaidi nchini”.

Hata hivyo katika habari zaidi kutoka nchini Congo ni kwamba Afisa wa tume ya uchaguzi Jean-Pierre Kalamba amesema matokeo ya muda yatatangazwa katika kipindi cha wiki moja baada ya upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 30 Desemba, lakini matokeo kamili yatatangazwa tarehe 9 januari, 2019. Rais mpya anatarajiwa kuapishwa tarehe 12 Januari 2019 iwapo kila kitu kitakwenda kadiri sharia za uchaguzi. Hata hivyo hali ya wasiwasi imekuwepo nchini humo tangu Kabila alipokosa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili na wa mwisho. Tume ya uchaguzi ilikuwa imesema haiwezekani kuandaa uchaguzi kwa wakati kutokana na matatizo ya kuandaa usajili ya wapiga kura, hasa eneo lenye misukosuko la Kasai katikati ya nchi hiyo.

 

27 November 2018, 15:56