Selikali ya Angola yawafukuza watu kutoka katuka machimbo ya madini Selikali ya Angola yawafukuza watu kutoka katuka machimbo ya madini 

Congo DRC: Kipeo kipya cha kibinadamu chazuka!

Caritas na Unicef zinatoa taarifa juu ya kipeo kipya cha kibinadamu kinachoendelea kuikumba mipaka ya Angola na Congo DRC kwenye majimbo menne ya Popokabaka, Luiza, Luebo e Matadi kufuatia na kufukuzwa watu kwa ghafla kwa upande wa Serikali ya Angola katika machimbo ya dhahabu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika wiki nne tu ni  zaidi ya watu 450,000 waliofukuzwa na kuelekea katika maeneo ya Kamano na mipaka yake. Hiki ni kipeo kipya cha kibinadamu kinachoendelea kuikumba hata mipaka ya Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vongo kwenye majimbo menne ya Popokabaka, Luiza, Luebo e Matadi kufuatia na tendo hilo la  kufukuzwa kwa ghafla kwa upande wa  Serikali ya Angola mamia elfu ya watu wa Congo waliokuwa wanafanya kazi katika madini ya dhahabu kwenye maneno ya Lunda Norte.

Maparokia na vituo vya Caritas mahalia, vimekuwa tayari kuanza shughuli ya kusaidia watu walio rundikana japokuwa na zana ambazo hazistahili kulingana na mahitaji yao. Caritas ya Parokia ya Kamako, imefungua majengo yake yote kwa ajili ya kuwakaribisha zaidi ya watu 2,300 kati ya vituo vyake  vya Caritas na mashule mawili katoliki.  Hata hivyo hata Caritas ya Congo iko inafanya maandalizi lakini ikiwasiliana na mitandao mengine ya Caritas kimataifa ili kuweza kuratibu namna ya utoaji wa msaada.

Hata hiyo Caritas ya Italia kwa miaka mingi inashirikiana na Caritas ya Congo kutoa msaada kwa  idadi kubwa ya dharura na kutengeneza mipango modogo midogo ya maendelea, kufuatia na kipeo hiki kipya ambacho kinaikumba hali na kinatoa uwezekano wake wa kuingilia kati kusaidia Caritas mahalia.

Pamoja na hayo taarifa nyingine inasema kuwa, takribani watoto 80,000 waliorejea hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Angola hivi sasa wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu hayo yamesema na kuthibitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.   Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF iliyotolewa mapema wiki hii ni zaidi ya raia 300,000 wa DRC wamerejea nyumbani tangu tarehe Mosi Oktoba, hali inayozusha hofu miongoni mwa wadau wa misaada ya kibinadamu kwamba taifa hilo ambalo limeghubikwa na machafuko sasa liko katika hatihati ya zahma nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF Christopher Boulierac watoto waliorejea DRC hali yao ni tete: “Maelfu ya watoto wanatembea mwendo mrefu , wakikabiliwa na hali mbaya ya hewa , njaa, kutokuwepo usalama na hatari ya kufanyiwa ukatili. Wana fursa ndogo ya kupata maji safi na huduma za afya na pia wanakosa elimu. Tuna wasiwasi sana kuhusu hali zao n aza familia zao.” Ameongeza kana kwamba hiyo haitoshi bei za vyakula zimeongezeka kwa kiasi kikubwa sana katika baadhi ya maebneo na kufanya hali kuwa mbaya kwa watoto hao na familia zao.

UNICEF na wadau wake wamefanya tathimini  ya mahitaji ya kibinadamu katika majimbo ya Kamako na Kasai ambako wengi wanaorejea ndio wanaishi na wanajiandaa kuwasaidia watoto na familia zao kwa kuwawekea mabomba ya maji safi ya kunywa, makazi ya dharura 27, kuwagawaia vyandarua vya mbu kuzuia malaria, kukabiliana na utapia mlo, kutoa chanjo za surua , kuwawekea maeneo ya kusomea na kuunganisha watoto na familia zao. Na kuweza kukidhi mahitajoi hayo UNICEF inahitaji dola milioni 3.

01 November 2018, 14:24