Nicaragua,wachungaji 11 wa kiinjili watiwa mbaroni
Osservatore Romano
Wachungaji 11 wa Kiinjili wanaohusishwa na shirika la Mountain Gateway nchini Marekani la wametiwa mbaroni na mahakama ya Nicaragua kwa tuhuma za uchakachuaji wa fedha. Kwa wanachama wa shirika lenye makao yake huko Texas - walikamatwa miezi miwili iliyopita na kuzuiliwa katika kifungo cha upweke bila kuwasiliana na wanasheria au wanafamilia na hivyo majaji walitoa hukumu za kati ya miaka 12 na 15 jela, pamoja na faini ya dola milioni 80 kwa kila mtu.
Kesi ilifanyika nyuma ya milango iliyofungwa. Hii iliripotiwa na shirika la Kutetea uhuru (Alliance in Defense of Freedom, Adf Internacional,) ambalo lilizungumzia hukumu isiyo ya kawaida kutokana na kesi ambapo mamlaka hazikuweza kuwasilisha ushahidi wowote. ADF imeomba kuingilia kati kwa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu kwa kutaka mamlaka ya Managua dhamana ya heshima kwa wafungwa wakati wa kukaa gerezani.
Wakati huo huo, kwa mwaka wa pili mfululizo, katika Juma Takatifu ilifanyika Nicaragua bila maandamano katika mitaa ya miji na Njia ya Msalaba kwani yalipigwa marufuku na mamlaka. Shughuli pekee zilizoidhinishwa zilifanyika ndani ya mahali pa ibada au katika maeneo yao. Maafisa elfu nne wa polisi walipangwa kuzunguka makanisa nchini ili kuhakikisha kwamba marufuku hiyo imefuatwa kikamilifu.