Tafuta

Tarehe Mosi Oktoba Mwaka 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II alimtangaza Mtakatifu Katarina wa Siena kuwa ni Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya Tarehe Mosi Oktoba Mwaka 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II alimtangaza Mtakatifu Katarina wa Siena kuwa ni Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya   (REUTERS)

Mtakatifu Katarina wa Siena Miaka 25 Tangu Atangazwe Kuwa Mwombezi wa Ulaya

Tarehe Mosi Oktoba 1999 Mt. Yohane Paulo II alimtangaza Mtakatifu Katarina wa Siena kuwa ni Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya na kwa mwaka 2024, Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu atangazwe kuwa Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya yameanza kutimua vumbi Jimbo kuu la Siena na yatahitimishwa rasmi 5 Mei 2024 kwa Ibada ya Misa Takatifu itakayoadhimishwa na Kardinali Lazzaro “Yu Hung Shik” Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kila mwaka ifikapo tarehe 29 Aprili, Mama Kanisa anaadhimisha Kumbukumbu ya Mtakatifu Katarina wa Siena, “Catharina wa Siena” Bikira na Mwalimu wa Kanisa. Katarina kwa lugha ya Kigiriki maana yake ni “Mwanamke asiyekuwa na mawaa”. Huyu alikuwa ni mtawa wa Shirika la Wadominikani, mwanataalimungu mahiri, mwanafalsafa wa kutupwa na mtu aliyekuwa na maono mapana katika maisha. Alifariki dunia kunako tarehe 29 Aprili 1380 akiwa mjini Roma. Papa Pio II akamtangaza kuwa Mtakatifu kunako mwaka 1461. Na ilipogota tarehe 4 Oktoba 1970, Mtakatifu Paulo VI akamtangaza Mtakatifu Katarina wa Siena kuwa ni Mwalimu wa Kanisa. Ilikuwa ni mwaka 1939 Papa Pio XII alipomtangaza kuwa ni Msimamizi na Mwombezi wa Italia pamoja na Mtakatifu Francisko wa Assisi.

Mtakatifu Katarina wa Siena 1999-2024 Miaka 25 ya Jubilei
Mtakatifu Katarina wa Siena 1999-2024 Miaka 25 ya Jubilei

Katika historia na maisha yake, anakumbukwa sana kama mjumbe wa amani, mshauri wa Mababa watakatifu waliolazimika kukimbilia uhamishoni kutokana na misigano ya kisiasa. Alikuwa kweli ni “mwanamke wa shoka, aliyesaidia mchakato wa toba na wongofu wa ndani, unaosimikwa katika Injili ya upendo; amani na upatanisho wa kweli. Ni Mtakatifu aliyejisadaka kwa ajili ya umoja wa Kanisa, akasali na kujitosa kwa moyo wake wote. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusali na kumwomba Mtakatifu Katarina wa Siena ili aweze kuombea umoja wa Kanisa na kuisaidia Italia katika kipindi hiki kigumu cha historia yake, bila kulisahau Bara la Ulaya.

Mt. Katarina wa Siena Mwombezi na Msimamizi wa Ulaya
Mt. Katarina wa Siena Mwombezi na Msimamizi wa Ulaya

Itakumbukwa kwamba, tarehe Mosi Oktoba Mwaka 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II alimtangaza Mtakatifu Katarina wa Siena kuwa ni Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya na kwa mwaka 2024, Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu atangazwe kuwa Mwombezi na Msimamizi wa Bara la Ulaya yameanza kutimua vumbi Jimbo kuu la Siena na kuhitimishwa rasmi tarehe 5 Mei 2024 kwa Ibada ya Misa Takatifu itakayoadhimishwa na Kardinali Lazzaro You Heung-sik, “Yu Hung Shik” Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri.

Katarina wa Siena
29 April 2024, 15:24