Tafuta

Dk. Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi 4 hadi 29 Oktoba 2023. Dk. Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi 4 hadi 29 Oktoba 2023. 

Dk.Ruffini:Dira ya Sinodi ni Kanisa la kukaribisha wote

Ni kawaida kwetu kujiuliza:tuko wapi ulimwenguni,tuko wapi kwenye safari yetu?Tumefikia wapi? Na wapi?Na zaidi ya yote,je,mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma,pamoja na sehemu ndogo ya watu rahisi waliobatizwa ulisaidia?Ni maswali ya Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kukutana pamoja, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikiliza kila mmoja kumesaidia kugundua tena kile kinachotuunganisha kuwa katika Kristo, kwa kutembea pamoja, ardhi nzuri ambapo mbegu inaweza kukua; kushuhudia kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana; kuthamini daima, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe kile kinachotutenganisha... Ndiyo maneno ambayo Dk. Paulo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi ambaye kila siku ya siku za Sinodi akiwa amezungukwa na wasemaji aliweza kutoa habari ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea tangu kuanza kwa Sinodi ya XVI ya Maaskofu kuanzia tarehe 4 -29 Oktoba 2023, ikiongozwa na Mada kuu:Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume. Hata hivyo Sinodi hii imegawanyika katika awamu mbili ambapo ya kwanza imehitimishwa na ya pili ni Oktoba 2024.

Mama baba wa Sinodi na Mama
Mama baba wa Sinodi na Mama

Kwa njia hiyo mara baada ya hitimisho la Sinodi hiyo, akitoa maoni yake katika Makala ya  Habari za Kikanisa SIR la Baraza la Maaskofu Italia kuhusiana na tukio hilo muhimu, Dk Ruffini anabainisha kuwa  "baada ya kufikia hatua ya nusu ya Sinodi hii, ambayo inatutaka tujifikirie upya kama Kanisa, tunajikuta tukistaajabishwa katika ulimwengu wenye mgawanyiko ambao "umepoteza njia ya amani, ambayo umempendelea Kaini kuliko Abeli" (Tazama Sala ya Papa Francisko ya amani ya 27.10.2023); sayari ambayo "inabomoka na labda inakaribia mahali pa kuvunjika" (Papa Francisko, Laudate Deum,2). Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa hiyo anasisitiza kuwa "Ni kawaida kwetu kujiuliza: tuko wapi ulimwenguni, tuko wapi kwenye safari yetu? Tumefikia wapi? Na wapi? Na zaidi ya yote, je, mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma ulisaidia, pamoja na sehemu ndogo ya "watu rahisi waliobatizwa"? Je  ulisaidia nini?

Washiriki wa Sinodi
Washiriki wa Sinodi

Akiendelea Dk Riffini anabainisha kuwa, “Hati ya muhtasari inaishia kwa kunukuu Injili ya Marko (Mk 4.30 ) isemayo "Ufalme wa Mungu umefanana na mbegu ya haradali ambayo ikipandwa ardhini ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inakuwa kubwa sana hivi kwamba ndege wa angani wanaweza kujificha kwenye kivuli chake. " Na hivyo  ndivyo ilivyokuwa kwa ajili ya kukusanyika, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikilizana kwa ajili ya kugundua tena kile kinachotuunganisha kuwa katika Kristo; kutembea pamoja, ardhi nzuri ambapo mbegu inaweza kukua." Dk. Ruffini aidha anabainisha kwamba katika Sinodi hii ni wazi ilikuwa ni ushuhudia kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana. Na hii ni kwa sababu lazima kuthamini kila wakati, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe kile kinachotutenganisha. Kuelewa kwamba jukumu la ushirikiano ambalo kila mtu anaitwa, hata  katika utofauti wa karama na huduma ni huduma na sio nguvu. Vile vile ni kugundua upya  kwa jinsi gani hotuba ya Yesu juu ya umaskini inatuhusu sisi sote, kama watu na kama taasisi. Zaidi pia ni kupendekeza na kuepuka ukasisi wowote (ule wa walei na ule wa mapadre waliowekwa wakfu).

Kujadili na kutembea pamoja
Kujadili na kutembea pamoja

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aidha alisisitiza kuwa ni kugundua tena umuhimu wa kila moja; na zaidi ya ushirika wote unaotufanya kuwa wamoja, washiriki wa mtu mwingine. Kutafakari juu ya nafasi ya wanawake, ambao walikuwa wa kwanza kutangaza ufufuko wa Yesu. Kutoa msukumo mpya kwa uekumene. Kuwa Kanisa la kukaribisha watu wote. Na zaidi kila mtu, ambapo hakuna mtu aliyetengwa. Kuwa Kanisa ambalo halifikirii kulingana na migawanyiko na alama za ulimwengu, lakini linalojiuliza kila wakati ikiwa Yesu angefanya nini akikabiliwa na kaka au dada aliyejeruhiwa. Na ni kwa jinsi gani angehakikisha kutowatenga na ukombozi. Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi aidha alithibitisha jinsi ambavyo kuna changamoto nyingi ambazo tunakabiliana nazo kama Kanisa. Zinahusu ukuhani, ushemasi, huduma zisizowekwa wakfu, maisha ya wakfu, familia na hali ngumu za ndoa; Huduma ya Kipetro, Uekumene, mawasiliano katika enzi ya kidijitali. Pia zinahusu mada yenye utata wa utambulisho wa kijinsia na mwelekeo wa kijinsia.

Kila siku Dr Ruffini na tume yake walihabarisha juu ya kinachoendelea cha Sinodi
Kila siku Dr Ruffini na tume yake walihabarisha juu ya kinachoendelea cha Sinodi

Dk. Ruffini alisisitiza kuwa, "lakini yote hayo ni upendo unaojumuisha wote. Sheria moja tu inaelezea Kanisa la Sinodi inayokubalika:ya  upendo; ubunifu wa kimisionari wenye msingi mzuri, vumilivu, wema; “si lenye wivu, si lenye majivuno, si lenye kuvimba” (rej.1Kor 13:4). Hivi ndivyo Mkutano ulituambia ambao umehitimishwa hivi karibuni. Na imetuonesha dira na siyo orodha ya mambo. Mamilioni, mabilioni ya watu ni kama msafiri aliyesafiri katika barabara kati ya Yerusalemu na Yeriko. Kwa hiyo hatuwezi kusema sikujua. Kwa hili tutahukumiwa (rej. Mt 25).” Anahitimisha maoni yake Dk. Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi iliyaonza tarehe 4 hadi 29 Otoba 2023.

Wakati wa kutoa taarifa ya sinodi
Wakati wa kutoa taarifa ya sinodi
DK.Ruffini baada ya Sinodi
04 November 2023, 12:58