Tafuta

Watu na watoto wao wanafuta hifadhi kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo,huko Goma. Watu na watoto wao wanafuta hifadhi kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo,huko Goma. 

UNICEF,Italia kuhusu Kongamano la Kimataifa juu ya Haki za watoto mjini Vatican

Kufikia mwisho wa 2023,karibu watoto milioni 50 walikimbia makazi yao kutokana na migogoro,ghasia na majanga ya asili,asilimia 40 ya watu wote waliolazimika kuhama makazi yao ulimwenguni.Tukiangalia 2025,tunakadiria kuwa watoto milioni 213 katika nchi na maeneo 146 watahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu.Ni idadi kubwa sana.Haya yamesemwa na Iacomini,Msemaji wa UNICEF Italia katika fursa ya Kongamano kuhusu haki za Watoto linalofanyika mjini Vatican Februari 2-3.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Katika Kongamano la kimataifa kuhusu haki za Watoto ambao umefanyika mjini Vatican tarehe 2-3 Februari 2025, Msemajai wa Shirika la Kusaidia Watoto UNICEF, Italia, Andrea Iacomini ametoa tamko lake. Msemaji huyo alibainisha kuwa: “Kongamano la Kimataifa la Haki za Watoto, uliohimizwa na Papa Francisko, uliofunguliwa katika makao makuu ya kitume mjini Vatican, linawakilisha fursa muhimu sana ya kuweka kipaumbele juu ya changamoto zinazotukabili sisi watu wazima, kwa wanasiasa, vyama vya Serikali na wale wote wanaoweza kwa njia yoyote kuchangia katika kulinda na kurejesha utoto wa watoto na kuboresha hali zao za maisha. Watoto ndio walio hatarini zaidi katika jamii zetu.

Kwa mujibu wa Iacomini alisisitiza kuwa "Kongamano hilo linalooongozwa na mada ya: “Tuwapende na kuwalinda” linafuatia Siku ya kwanza ya Watoto duniani iliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko na kufanyika mnamo tarehe 25 Mei 2024 kwenye Uwanja wa Olimpiki, ambapo sisi kama UNICEF tulishiriki, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza amani na haki ya watoto wote, kila mahali."

Leo, mamilioni ya watoto duniani kote wananyimwa haki zao za kimsingi kutokana na migogoro mbalimbali, kuanzia migogoro hadi matokeo ya mabadiliko ya tabianchi, kutoka dharura za kiafya hadi umaskini unaoongezeka, takriban watoto milioni 460 wanaishi au wanakimbia migogoro mikali; zaidi ya watoto bilioni 1 - karibu nusu ya watoto duniani - wanaishi katika nchi ambazo ziko katika hatari kubwa sana kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kufikia mwisho wa 2023, karibu watoto milioni 50 walikimbia makazi yao kutokana na migogoro, ghasia na majanga ya asili,asilimia 40 ya watu wote waliolazimika kuyahama makazi yao ulimwenguni. Tukiangalia mbele hadi 2025, tunakadiria kuwa watoto milioni 213 katika nchi na maeneo 146 watahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu ambapo idadi kubwa sana! Tunatumaini kuwa Mkutano huu unaweza kutoa mwanga kwa watoto wa kike na kiume wadogo wasioonekana."

Makilishi wa UNICEF Italia atoa maoni yake kuhusu Kongamano la Vatican
03 Februari 2025, 13:13