Siku ya Kimataifa ya kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika. Siku ya Kimataifa ya kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika.  (ANSA)

Siku ya Kimataifa ya kufuta Ujinga wa kutojua kusoma na kuandika

Siku ya Kimataifa ya kufuta ujinga wa kutokujua kuandika wala kusoma,huandimisha kila ifika Septemba 8.Kusoma na kuandika ni kipengele muhimu cha malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu na ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030. Lengo la 4 ni kuhakikisha kuwa vijana wengi na watu wazima wanaezeshwa kupata elimu.

Na  Angella Rwezaula, - Vatican.

Kila mwaka tarehe 8 Septemba, Siku ya Kimataifa ya kutojua Kusoma na Kuandika au  Siku ya Kimataifa ya Kusoma na Kuandika iliyoanzishwa  mnamo tarehe 26 Oktoba 1966 na kikao cha 14 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO. Wazo la kutenga siku kwa mada ya kisomo, hata hivyo, lilizaliwa wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Elimu, juu ya mada ya kutokomeza watu wasiojua kusoma na kuandika, uliofanyika  huko Tehran, kuanzia tarehe 8 hadi 19 Septemba 1965. Sherehe za  mwaka huu 2023 zinaongozwa na kauli mbiu: “Kukuza kusoma na kuandika kwa ulimwengu katika kipindi cha mpito: kujenga misingi ya jamii endelevu na zenye amani.” Kujua kusoma na kuandika leo hii  ni sawa na maendeleo,  yaani maendeleo, ufahamu, uboreshaji na ushirikishwaji. Lengo kuu la siku hii ni kukuza na kuongeza ufahamu wa kusoma na kuandika kama haki ya msingi ya binadamu na kama nyenzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi duniani.

Kusoma na kuandika nchini Italia na ulimwenguni leo

Kulingana na  Shirika la ‘ActionAid’, ambalo ni shirika huru la kimataifa lililojitolea kupambana na sababu za umaskini, kutojua kusoma na kuandika  linabainisha kuwa suala hili ni mojawapo ya matatizo makubwa zaidi duniani. Kulingana na takwimu za  2020, kuna watu milioni 763 ulimwenguni ambao hawajui kusoma na kuandika. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kusini mwa Asia na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa  takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu ya Shirika la Umoja wa Mataifa, la Elimu Syansi na Utamaduni (UNESCO), kuna suala la kweli la kike linalohusishwa na kutojua kusoma na kuandika katika kile kinachoitwa maeneo duni ya mbali kijiografia, kulingana na ambayo takriban theluthi mbili ya watu wasiojua kusoma na kuandika duniani katika maeneo haya, ingeundwa na  wanawake. Kwa hakika, kungekuwa na uwiano kinyume kati ya asilimia ya elimu ya wanawake na viwango vya ajira, na asilimia ya viwango vya uzazi.

Ni wazi kwamba kwa kuongezeka kwa kusoma na kuandika idadi ya kuzaliwa hupungua kwa kasi na kinyume chake. Inatokea kwamba watu wanaojua kusoma na kuandika wana uwezekano mkubwa wa kupata kazi, kupata zaidi na kuishi maisha yenye afya na usawa zaidi. Nchini Italia, kulingana na shirika la Hesabu ya watu (ISTAT), asilimia ya watu wasiojua kusoma na kuandika wamepungua mara kwa mara, kutoka asilimia 74.1% baada ya kuunganishwa kwa 1861, hadi 12.9% ya muujiza wa kiuchumi wa 1950, hadi 0.6% ya 2020. Hadi sasa, mikoa yenye watu wasiojua kusoma na kuandika ni Basilicata, Calabria na Molise ambayo ni kusini mwa Italia.

Malengo ya Siku ya Kimataifa ya Kusoma na Kuandika

Kusoma, kuandika, kuhesabu na kutumia teknolojia za kidijitali ni stadi za kimsingi za kuweza kuchukua jukumu tendaji na kuchangia maendeleo ya kiuchumi. Lakini kwa watu wengi haiwezekani au hata dhahiri kama mtu anaweza kufikiria. Licha ya mafanikio yaliyopatikana katika ngazi ya kimataifa, UNESCO inatukumbusha kuwa katika nchi nyingi sana elimu  bado ni haki inayonyimwa kutokana na mambo mengi kama vile umaskini, ukosefu wa rasilimali za elimu na miundombinu, ubaguzi wa kijinsia, urithi wa kitamaduni na migogoro ya silaha. Juhudi zinazoendelea kufanywa na jumuiya ya kimataifa zinaweza kusaidia kuondokana na vikwazo hivi na kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa kiwango kikubwa. Kwa sababu hii, malengo ya maadhimisho haya, ambayo yanalenga kukuza kusoma na kuandika na elimu ya kimataifa, ni tofauti na muhimu. Miongoni mwa mambo makuu tunayokumbuka: kuongeza uelewa wa umma juu ya umuhimu wa kupiga vita ujinga; kukuza, kuhimiza na kuboresha upatikanaji wa elimu ya msingi na aina nyingine zote za elimu kwa watu wote; kuboresha na kuhimiza ujuzi wa kidijitali.

Lengo la 4 la Maendeleo endelevu kufika 2023 ni kutoa fursa za elimu bora

Kaulimbiu hiyo pia ipo katika mpango wa utekelezaji kwa watu, sayari na ustawi endelevu wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa 2030, iliyotiwa saini na nchi 193 wanachama. Katika Lengo la 4 la Maendeleo Endelevu kufikia 2030, ni kutoa fursa za elimu bora, usawa na mjumuisho kwa wote, ambapo inataja kuwa: “Elimu bora ndiyo msingi wa kuboresha maisha ya watu na kufikia maendeleo endelevu. Matokeo muhimu yamepatikana kuhusu kuongeza upatikanaji wa elimu katika ngazi zote na kuongeza kiwango cha uandikishaji shuleni, hasa kwa wanawake na wasichana. Kiwango cha msingi cha ujuzi wa kusoma na kuandika kimeboreshwa kwa kiasi kikubwa, lakini juhudi zinahitaji kuongezwa maradufu ili kufikia matokeo bora zaidi kuelekea malengo ya elimu kwa wote. Kwa mfano, usawa kati ya wasichana na wavulana katika elimu ya msingi umepatikana duniani kote, lakini ni nchi chache zimefanikisha hili katika ngazi zote za elimu.”

Kusoma na kuandika kunaweza kuleta maendeleo ya ubinadamu

Serikali, taasisi za umma na za kibinafsi, vyama na mashirika, wataalamu na vituo vya mafunzo vimefanya mengi na vinafanya mengi ili kufanya yote haya yawezekane na kufikiwa. Kwa mfano Nchini Uswisi kwa mfano, CFC (Mkutano wa Uswisi wa Italia kwa ajili ya kuendelea na elimu ya watu wazima) kwa ushirikiano wa karibu na FSEA (Shirikisho la Uswisi la elimu inayoendelea) watafanya jioni za kusoma na kuonyeshwa filamu katika hafla ya Siku hiyo. Umeandaliwa  mkutano Ulimwenguni kote, wa ana kwa ana katika mtandaoni  Ijumaa, tarehe 8 Septemba 2023 huko Paris, Ufaransa. Maadhimisho haya ya kimataifa yanajumuisha Sherehe za Tuzo za Kimataifa za Kusoma na Kuandika za UNESCO kutangaza programu bora za mwaka huu zilizoshinda Tuzo (UNESCO King Sejong Literacy Award' linaloungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya Korea, 'UNESCO Confucius' na  Tuzo ya kusoma na kuandika kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Uchina).

UNESCO:Kila mmoja ajitolee kupunguza ujinga wa kusoma na kuandika

Zaidi ya hayo, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kusoma na Kuandika, UNESCO inakaribisha kila mtu kujitolea kukuza kusoma na kuandika na kuchukua hatua za kupunguza kutojua kusoma na kuandika. Kuna njia nyingi za kufanya hivyo, kwa mfano: kusaidia mashirika yanayofanya kazi kwa ajili ya kusoma na kuandika; toa wakati wako kama mtu wa kujitolea; kusambaza umuhimu wake; toa mchango kwa shirika linalokuza shughuli; kujua faida zake; kuandaa au kushiriki katika matukio ya ndani. Kujua kusoma na kuandika ni haki ya kimsingi ambayo lazima ihakikishwe kwa kila mtu, bila kujali umri, jinsia, dini au kabila.

08 September 2023, 10:12