Tafuta

Shughuli bao zinaendelea nchini Morocco kutafuta manusura au watu ambao wamebaki chini ya vifusi kwa kutumia hata mbwa. Shughuli bao zinaendelea nchini Morocco kutafuta manusura au watu ambao wamebaki chini ya vifusi kwa kutumia hata mbwa.  (AFP or licensors)

Morocco:Idadi ya vifo imezidi kuongezeka hadi 3000&zaidi ya watoto 1000

Idadi ya vifo imezidi kuongezeka kwani inasemekana hadi sasa ni 3,000 na majeruhi 5,530.Kulingana na Unicef, zaidi ya watoto elfu 100 wameathiriwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika maeneo ya tetemeko la ardhi bado kuna watu wengi wamelala chini ya vifusi na wengine wanalala nje bila msaada. Katika baadhi ya vijiji mahema yamefika, na watu wengi wamekaribishwa kwenye majengo salama lakini mikoa mingine kuna watu wanalala chini lakini bila mahali pa kujisitiri. Kwa bahati nzuri wengine walipokea angalau blanketi lakini kuna hitaji la haraka la kupata malazi." Tifwat Belaid, meneja mwandamizi wa programu wa ActionAid, yaani matendo ya msaada  ambaye amekuwa akifanya kazi bila kukoma tangu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 siku ya Ijumaa tarehe 8 Septemba 2023 lilipogonga katika mikoa karibu na Marrakech, kusini mwa nchi, aliripoti hali hiyo kwa Shirika la habari za kidini la Baraza la Maaskofu Italia (SIR) kutokea Rabat, mji mkuu wa Morocco kuhusu hali hiyo.

Nyumba nyingine ziemanguka na nyingine kama hivyo nchini Mrocco
Nyumba nyingine ziemanguka na nyingine kama hivyo nchini Mrocco

Shirika la "ActionAid", ambayo imekuwa ikifanya kazi nchini Morocco kwa miaka 20, ilifanya kazi mara moja kupitia washirika wake wa ndani katika maeneo yaliyoathirika ya Al-Haous, kitovu cha tetemeko la ardhi, El Chaoud, Taroudant, Azilal, Chichaoua na Ouarzazate, katika safu ya milima ya Atlas. Timu ya ActionAid ipo kwa wakati huu kutathmini mahitaji. Ugawaji wa chakula, maji, nguo na vifaa vya msaada ambao tayari umeanza. “Makumi ya maelfu ya watu wamepoteza makao yao lakini hakuna takwimu rasmi za watu waliohamishwa makazi yao,” aliripoti Belaid na kwamba  “Inahitaji kubadilishwa siku baada ya siku. Tunahitaji blanketi kujikinga na baridi na juu ya malazi yote. Majeruhi walipelekwa hospitali na Jeshi la Kifalme lakini kuna hitaji kubwa la dawa kwa wagonjwa ambao wanajikuta wametengwa na bila matibabu. Tunajaribu kupata msaada huu moja kwa moja au kupitia washirika wa ndani.Barabara katika baadhi ya vijiji zimefungwa, kwa hivyo inabidi tusubiri hadi ziweze kupitika”.

Wafanyakazi wanatoa msaada
Wafanyakazi wanatoa msaada   (AFP or licensors)

Kwa njia hiyo “ni muhimu kufanya jitihada za kuratibu kati ya wale wote wanaoshughulika na misaada ili kujaribu kuelewa ni nani anahitaji nini na jinsi ya kuwafikia. Misaada ya kibinadamu inaandamana sambamba na juhudi za majeshi na mamlaka za mitaa. Alifafanua. Katikati ya janga kama hilo, kipengele chanya zaidi "kimekuwa mshikamano wa watu wa Morocco wote: kila mtu anahamasishwa kuchangia mablanketi, mahema, madawa na pesa. Kuna hisia kubwa ya mshikamano na umoja. Wengi wetu tunajua watu katika maeneo ya tetemeko la ardhi au kwenda kupanda milima ya Atlas kwa hivyo tunaguswa sana."

Watu hawana mahali pa kulala
Watu hawana mahali pa kulala   (AFP or licensors)

Mfanyakazi wa kibinadamu alizungumzia uhamasishaji mkubwa pia wa jumuiya ya kimataifa.  Kwamba "Mashirika mengi ya kimataifa kama vile ActionAid yamechukua hatua madhubuti na watu wa Morocco wote wanashukuru. Sasa kuna watu wengi na mashirika yanayohusika katika uwanja huo lakini basi itabidi tufikirie juu ya ujenzi mpya, makazi na kazi, lakini pia juu ya kujenga upya jamii na muundo wa kijamii."Alihitimisha.

13 Septemba 2023, 16:22