Tafuta

Msaada kutoka Yorda umefika Libya kutokana na mafuriko na kimbunga Daniel. Msaada kutoka Yorda umefika Libya kutokana na mafuriko na kimbunga Daniel.  (AFP or licensors)

Libya,vifo na uharibifu kutokana na Kimbunga Daniel ni zaidi vifo elfu 6

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko katika Libya inatisha.Zaidi ya watu elfu 10 hawapo:Derna inabaki kuwa jiji lililoathiriwa zaidi,lakini idadi hiyo inaongezeka kila dakika.Kwa sasa haiwezekani kuhesabu uharibifu wa miundombinu na wakati huo msaada na rambi rambi kutoka pande za dunia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mara baada ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko  Jumatano tarehe 13 Septemba amesema "Ninawaalika kuungana na sala yangu kwa ajili ya wale walipoteza maisha, kwa ajili ya familia zao na kwa wale waliorundikana. Wasikose mshikamano wetu  wa kuelekeza kwa kaka na dada waliojaribiwa namna hiyo na mkasa huu”. Hata hivyo tarehe 12 Septemba 2023 alituma ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Paroli Katibu wa Vatican kuhusiana na mkasa huu mbaya sana.


Dhoruba iliyoikumba Libya bila huruma Dominika tarehe 10  Septemba 2023, ilisababisha mauaji ya kweli. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni maeneo ya pwani ya Jabal al-Akhdar na Benghazi, ambapo amri ya kutotoka nje iliwekwa na shule kufungwa. Katika mkoa huo, ambao tayari umekumbwa na mvua kubwa kwa siku kadhaa mfululizo, kuna mamia ya nyumba na miundombinu iliyoharibiwa na ghasia za mafuriko. Mafuriko hayo yaliacha miili isiyo na uhai barabarani, kupindua magari, kuharibu majengo na kufunga barabara zinazohitajika kufikia maeneo yaliyoathirika zaidi.


Hali katika mji wa Derna ni janga tu. Kwa sababu robo ya jiji lilisombwa na maji baada ya mafuriko kusababisha kuporomoka kwa bwawa la Wadi Dernah. Idadi ya vifo katika jiji hilo ni karibu 5300, lakini miili inaendelea kupatikana katika kila maeneo mbalimbali. Tariq al-Kharraz, mwakilishi wa serikali ya mashariki ya Cyrenaica, alisema kuwa mamia ya miili imerundikana kwenye makaburi na manusura wachache wanaweza kuwatambua. Baadhi ya shuhuda zinaripoti jinsi ambavyo maji yalivyopanda hadi mita tatu. Miundombinu ya jiji, ambayo ilikuwa  tayari imechakaa, haikuweza kuhimili ghadhabu ya dhoruba hiyo kali.

Hata hivyo uumbe za mshikamano na ukaribu umezidi kuongezaeka ambapo  kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Tripoli, Dbeiba, mtu hodari wa Cyrenaica, Jenerali Haftar alikuwa ameomba msaada.  Jumuiya ya kimataifa inahamasisha na kuandaa utumaji wa wafanyakazi na misaada. Msimamo wa nchi zote umefupishwa kwa maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres, ambaye alionesha ukaribu na watu na mamlaka ya Libya katika wakati huu mgumu. Kwa mujibu wake alisema "Umoja wa Mataifa unafanya kazi na washirika wa ndani, kitaifa na kimataifa ili kutoa haraka msaada wa kibinadamu unaohitajika kuleta kiwango cha chini cha usaidizi kwa wakazi wa maeneo yaliyoathirika."

13 Septemba 2023, 15:57