Ukraine:milipuko yenye nguvu usiku huko Kyiv&Ziara ya Zelensky Ulaya imehitimishwa!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Karibu milipuko kumi yenye nguvu ilisikika usiku wa tarehe 15 Mei huko Kyiv. Kengele za hatari ya mashambulizi ya anga inafanya kazi katika mikoa yote ya nchi, kutokana na mashambulizi ya Kirussi ya kiwango cha kipekee, na idadi kubwa ya makombora katika muda mfupi zaidi: utawala wa kijeshi wa mji mkuu wa Kiukreine umetangaza jambo hilo. Meya wa Kyiv Vitaliy Klitschko alisema vifusi vya roketi hizo vimeanguka katika wilaya mbalimbali, huku jengo moja likiharibiwa huko Solomyanskyi magharibi mwa Kyiv. Kuna watatu waliojeruhiwa kufuatia uvamizi wa Urussi uliofanywa usiku.
Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky alihitimisha safari yake barani Ulaya. Kutoka kwa ndege iliyokuwa ikimpeleka nyumbani, alielezea kufurahishwa kwake na mkutano na Papa Francisko na kwa msaada uliothibitishwa na Italia, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. “Kuna uungwaji mkono zaidi wa kujiunga kwetu na Umoja wa Ulaya, kuelewa zaidi kwamba uanachama wa NATO wa Ukraine hauwezi kuepukika,” alisema, akithibitisha kwamba silaha hizo mpya zitatumika kupinga Urussi na mashambulizi mapya ya kukabiliana nayo. Kituo cha mwisho kilikuwa jijini London, ambapo rais wa Ukraine alipata ahadi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Sunak kusambaza mamia ya makombora mengine ya ulinzi wa anga na ndege mpya za masafa marefu zaidi ya kilomita 200.
Majeruhi ya raia
Mashambulizi ya roketi yanaonekana kuongezeka pande zote mbili za mstari wa mbele nchini Ukraine, kulingana na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu. Tangu tarehe 24 Februari 2022, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Masuala ya Kibinadamu Martin Griffiths alisema, kumekuwa na waathrika wa kiraia 23,600 wa Ukraine, lakini inahofiwa kwamba idadi halisi itakuwa kubwa zaidi. Bwana Griffiths alisisitiza kwamba changamoto kubwa inahusiana na kushinda vikwazo vya kufikia maeneo yote ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia, ambayo kwa sasa iko chini ya udhibiti wa kijeshi wa Urussi, na ni lazima kuchunguza chaguzi zote ili kufikia raia, popote walipo.
Kwa hiyo katika zira ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitua London kwa mshangao asubuhi tarehe 15 Mei, kama sehemu ya ziara yake ya Ulaya ambayo ilimshuhudia akisimama Italia, mjini Vatican, Ujerumani na Ufaransa. Katika mji mkuu wa Uingereza, Bwana Zelensky aliwasili kwa helikopta ya kijeshi huko Checkers, makazi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, ambaye alimkaribisha kwa kusema: “Ujasiri na ujasiri wa Rais Zelensky na Ukraine ni msukumo kwa sisi sote.” Na kwa upande wa kiongozi wa Kiukraine alitoa shukrani za dhati kwa msaada mkubwa wa kijeshi uliotolewa na London kwa Kyiv. Hakika, London itathibitisha usambazaji zaidi wa mamia ya makombora ya ulinzi wa anga na mifumo ya angani isiyo na rubani, ikijumuisha ndege mpya zisizo na rubani za masafa marefu zenye safu ya zaidi ya kilomita 200. Nyenzo ambazo zitawasilishwa katika miezi ijayo nchini Ukraine inapojiandaa kuongeza upinzani wake kwa uvamizi unaoendelea wa Urussi. Na Waziri Mkuu wa Uingereza alitoa wito kwa washirika wa Magharibi kutoa msaada wa kijeshi wa Kyiv katika wakati huu muhimu katika upinzani wa Ukraine kwa vita vya kutisha vya uchokozi ambavyo haikuchagua au kuchochea”.
Na wakati huo huo Bwana Zelensky Dominika tarehe 14 Mei 2023 alikuwa Paris, Ufaransa, ambapo alikaribishwa na Rais Emmanuel Macron na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Wakati wa chakula cha jioni Bwana Zelensky aliomba kama alivyofanya hata jijini Roma na Berlin, Ujerumani silaha za kisasa zaidi kama vile mizinga, jeti, na silaha za kupambana na ndege. Kiongozi huyo pia alithibitishwa na washirika hao watatu wa Ulaya, wakisisitiza kwamba msaada unahitajika ili kuanzisha mashambulizi ya kukabiliana na machafuko na kupata ushindi wa mwisho. Ni hapo tu, alisema, kutakuwa na msingi wa kuanza mazungumzo na Moscow. Rais wa Ufaransa Macron na mwenzake wa Ukraine pia wametoa wito wa kuwekewa vikwazo vipya dhidi ya Urussi kufuatia mkutano wao wa kilele wa pande mbili mjini Paris.