Vijana wa Afrika Wafokolari waliunganika nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka 2022. Vijana wa Afrika Wafokolari waliunganika nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka 2022. 

UN,Gutterres:Vijana wahusishwe katika utungaji wa sera&kupitisha maamuzi

Bila vijana hushiriki kikamilifu wa utungaji sera na upitishaji uamuzi,ajenda 2030 itasalia kuwa ndoto tu.Amesema hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana Gutterres katika hadi yake ya kisera iliyochapishwa tarehe 19 Aprili 2023.“Vijana wamekuwa kichocheo cha mabadiliko ya jamii kupitia uhamasishaji wa vijana.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mustakabali wenye haki, usawa na endelevu hautawezekana bila ushiriki wa vijana bilioni 1.2 duniani, amesema hayo  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres katika andiko lake la kisera lililochapishwa tarehe 19 Aprili 2023. Hati hiyo imetoa  wito wa kupanua na kuimarisha ushiriki wa vijana katika utungaji wa sera za umma na kuhakikisha wanashiriki katika ngazi zote za kupitia uamuzi,ili hatimaye kufanikisha ajenda 2030 na maendeleo endelevu. Katibu Mkuu amesisitiza kuwa vijana ni msingi wa ubainishaji wa majibu ya  mambo muhimu ambayo dunia inahitaji kwa sasa. “Vijana wamekuwa kichochea cha mabadiliko ya jamii kupitia uhamasishaji wa vijana, kuhamasisha harakati za hatua kwa mabadiliko ya tabianchi, kutafuta haki dhidi ya ubaguzi wa rangi, kuhamasisha usawa wa jinsia na kutafuta hadhi ya utu kwa wote,” ameandika Katibu Mkuu.

Ujumuishwaji katika maeneo ya utungaji sera

Kwa kuhamasisha  ujumuishwaji wao kwenye maeneo ya utungaji sera, amebainisha kuwa  vijana wanatoa mtazamo mpana wa kuimarisha na kupitia uamuzi wa kina. Licha ya idadi yao kubwa, lakini vijana bado hawaonekani pindi linapokuja suala la kutunga sera na kupitia uamuzi, hati hiyo inabainisha. Kwa hiyo “Hii ni dhahiri kwenye ngazi ya kitaifa, ambako mifumo kama vile mabunge ya vijana au mabaraza ya vijana yayaohangaika kuleta mabadiliko kwenye uamuzi ambao unafanyika kwenye ngazi ya mawaziri, kura kwenye bajeti za ndani, au michakato ya amani na makubaliano ya vipindi vya mpito. “Hali hiyo hiyo ni wazi katika ngazi ya kimataifa, licha ya kuibuka kwa fursa za vipande vipande, ambapo vijana bado wanaendelea kushiriki kwa ufinyu kwenye upitishaji uamuzi kuhusu maendeleo endelevu, kuhamaisha  amani na usalama na haki za binadamu,” amesema Katibu Mkuu.

Kuimarisha ushiriki wa vijana

Katika hati hiyo  inamulika mapengo  yaliyoko na vikwazo na hivyo kuweka mapendekezo ya kuziba mapengo. Kwa mfano Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  amesisitiza kuwa mfumo wa Umoja wa Mataifa una dhima muhimu katika kusaidia vijana kujiandaa ipasavyo kushiriki katika ngazi zote za kupitisha uamuzi. Iwapo mifumo ya kimataifa itakuwa tayari kuweka mazingira ya sasa na yajayo kwa wote, basi ushiriki wenye maana wa vijana lazima uwe ndio maadili ya kila jambo badala ya kufanyika wakati fulani pekee,”  amesisitiza Katibu Mkuu. Pamoja na kupanua na kuimarisha ushiriki wa vijana, andiko hilo linatoa wito wa kupitisha kiwango cha kimataifa cha ushiriki kamilifu wa vijana katika upitishaji uamuzi. nKwa miaka nenda rudi, serikali, mashirika ya vijana na mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepitisha msururu wa kanuni za msingi za kuhakikisha ushiriki kamilifu na wenye maana wa vijana ikiwemo kuhakikisha unafanyika kwa msingi wa haki, unafadhiliwa vya kutosha, ni wazi, unafikika haas kwa vijana wenye ulemavu. Mapendekezo mengine ni wito wa kuanzisha chombo cha ushauri cha vijana katika kila nchi, na kuhakikisha ushiriki wa uhakika wa vijana kama sharti katika michakato yote ya kupitisha uamuzi kwenye Umoja wa Mataifa.

Hatua za UN kwa ajili ya vijana

Katika hati ya  Bwana António Guterres  inataka kuhakikisha kuwa vijana wanajumuhishwa katika mifumo yote inayohusisha serikali na Umoja wa Mataifa, na kupitisha mipango ya wazi ya vijana kushiriki katika kazi zote za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Aidha inataja hatua zaidi ambazo Umoja wa Mataifa unapaswa kuchukua ikiwemo kupitia upya kanuni za kazi za Baraza la Usalama na vyombo vyake vingine vinavyohusika na ushiriki wa vijana, na kuanzisha kwa mara ya kwanza Mkutano wa Kwanza wa aina yake kwenye Umoja wa Mataifa ambapo kiongozi atajibu maswali ya vijana na hivyo kuhakikisha uwakilishi fanisi wa vijana. Chapisho lake hilo  la kisera ni ripoti ya karibuni zaidi ya Katibu Mkuu kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mustakabali, utakaofanyika mwakani ambamo nchi zitachunguza majawabu ya pamoja kwa ajili ya dunia bora, kuimarisha usimamizi wa dunia kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Ni  andiko la tatu katika mfululizo wa mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti yake Katibu Mkuu kuhusu  Ajenda ya Pamoja  iliyochapishwa mwaka 2021.

UN yatoa wito kwa vijana
20 April 2023, 10:38