Tafuta

Moshi mkubwa katika majengo uliosababishwa na mabomu  huko Khartoum Kaskazini, Sudan. Moshi mkubwa katika majengo uliosababishwa na mabomu huko Khartoum Kaskazini, Sudan. 

Sudan:ufyatuaji risasi unafanyika kila mahali na upatanisho mgumu

Ushuhuda wa mtawa kutoka nchi ya Sudan amebainisha kuwa amri ya kutotoka nje ilikiukwa,watu walifungiwa ofisini,bomu liligonga hata ua wa Kanisa.Kwa hiyo mji mjuu wa nchi hiyo hauna usalama na balozi zinafungwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa siku hizi Sudan imekuwa nchi iliyochomwa moto na makundi mawili, jeshi la kawaida na wanamgambo kwa kile kinachoitwa ‘Vikosi vya Msaada wa Haraka’. Mapigano makali sana ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya 400 na 3,500 kujeruhiwa, kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni na ambapo tarehe 21 Aprili 2023 pia yalisababisha kifo cha mwendeshaji wa shughuli za Shirika la Kimataifa la Uhamiaji.  Mji mkuu wa Khartoum hauko salama kutokana na wimbi la mapigano na kwa muda sasa umekuwa uwanja wa vita, huku ufyatuaji risasi, makombora yakipiga maeneo mengine pia. Mjini kuna watu wengi ambao kwa siku nyingi wamezuiliwa kutoka katika ofisi zao  ambako wameshindwa kutokana na  mapigano ya mitaani.

Bomu kanisani

Madaktari wasio na Mipaka (MSF) pia wamezungumzia hali ya janga, kwani shirika  ambalo linatibu mamia ya waliojeruhiwa katika maeneo mbalimbali, wengi ni raia waliopigwa na risasi zilizopotea na wengi ni watoto, alisema Cyrus Paye, mratibu wa Mpango huo wa MSF. Hali hiyo hiyo ambayo ilizungumzwa katika mahojiano na Vatican News  na mmisionari wa Italia kwa njia ya simu nchini Sudan na Mwandishi Christine Seuss. Mtawa huyo, ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu za kiusalama, alisema kuwa katika mji wa Bad bomu lilianguka katika ua la Kanisa Kuu Katoliki, na kuvunja madirisha na kuharibu jengo hilo, kwa bahati nzuri kidogo halisababisha maafa ya watu. Na huko Khartoum, katika baadhi ya maeneo ufyatuaji risasi ni endelevu na awamu za amri ya kutotoka nje iliyotangazwa hazijazingatiwa.

Jukumu la Wakristo

Kanisa pamoja na jumuiya nyingine za kikanisa, siku zote zimejiepusha kutoa maoni au kushiriki katika nyanja ya kisiasa na zina uwezo mdogo wa kuleta matokeo kwa vile Wakristo ni wachache sana wa idadi ambayo ni karibu  asilimia 2- 3% katika Sudan yote”. Pia kuna uwepo mkubwa wa Wakristo wasio Wasudan lakini wa Sudan Kusini, ambao hata hivyo hawana la kusema kwa sababu wao sio raia wa nchi hiyo na kwa hivyo hawana hadhi ya kisiasa ya kuwa nayo katika  kauli zao. Mmisionari amehitimisha kwa kubainisha kuwa ikiwa safari ya Papa nchini Sudan Kusini mwezi Februari ilitoa ujumbe mzito kwa idadi ya watu, kwa bahati mbaya huko Sudan haijaonekana katika kiwango cha mashirika ya kiraia au jamii ya kisiasa na kwa hivyo haionekani kuwa hivyo leo hii, athari kwa maisha ya kisiasa na hali ya kijamii na kijeshi ni kubwa.

22 April 2023, 14:08