2020.04.07: simu msaada wa kisaikolojia, kiroho. 2020.04.07: simu msaada wa kisaikolojia, kiroho. 

Siku ya Afya duniani.Simu Rafiki:kuongezeka wasiwasi kwa vijana

Chama kinaripoti juu ya ongezeko la matatizo yanayoathiri zaidi ya watoto wote,yaliyochochewa na kipindi cha janga la uviko ambacho kimeisha.Ni zaidi ya maombi 110,000 ya usaidizi kwa mwaka 2022.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ugumu wa kutazama uwezekano wa siku zijazo, katika hali iliyojaa wasiwasi unaosababishwa na sasa. Ni hali ya vijana wengi ambao wanajikuta katikati ya matatizo ya kuwepo na usumbufu wa kisaikolojia. Ili kuashiria hii ni ‘Telefono Amico’yaani  Simu rafiki ambayo, tangu 1967, imeunga mkono wale wanaoomba msaada kwa ajili ya mazungumzo ya simu, huduma za barua pepe na whatsapp. Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya  Afya Duniani tarehe 7 Aprili 2023, Chama cha Simu Rafiki,  kinaoneesha kusikitishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu waliogeukia huduma hiyo, zaidi ya maombi 110,000 ya kuomba msaada kwa mwaka 2022 pekee, huku kukiwa na ongezeko kubwa la vijana, hasa kwa wasichana na kwa kasi kubwa ya kuongezeka kwa mwenendo huo.

Ni katika mazingira magumu ambayo vijana wanahamia leo hii yanayotokana na hofu na kutokuwa na uhakika, yamezidishwa na matukio ya miaka ya hivi karibuni: kutoka katika  ukosefu wa kazi, hadi wasiwasi wa watu wazima, kupitia vita ambayo inaonesha hakuna dalili za kuacha. Kwa mujibu wa Cristina Rigon, makamu wa rais wa Telephone Amico akizungumza na Vatican News amesema:"Tunatambua hali ya kutokuwa na utulivu kwa vijana, kutokana na ugumu wa kujenga maisha ya baadaye, ambayo mara nyingi hujitokeza katika ujana, wakati ambapo mtu huanza kuelezea njia yake mwenyewe. Tunaona ugumu na mkanganyiko mambo ambayo yanaweza kusababisha kujiumiza na matatizo ya kula, yote ambayo yanaweza kuwa matokeo ya haja ya kusikilizwa, pia kutokana na ukaribu wa uwongo ambao mara nyingi husababishwa na mitandao ya kijamii".

Kilichosikitisha sana maisha ya watoto na watu wazima ni janga la UVIKO-19 ambalo, tangu mwanzoni mwa 2020, limebadilisha usawa wa jamii, ikifafanua upya mipaka ya maisha ya kila siku ya vijana na zaidi. Pamoja na athari kubwa ambazo virusi vimeleta kwa ghafla maisha ya kila mtu, kumekuwa na ongezeko la watu ambao wamepata nguvu ya kuomba msaada. "Maombi ya msaada kwa hakika yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa usumbufu  lakini pia ni kweli kwamba watu pengine waliona haki ya kuomba msaada zaidi kuliko siku za nyuma, kuanza kuondoa ugumu huu katika kuomba msaada".

"Yeyote anayegeukia Telefono Amico Italia mara nyingi hajisikii karibu na watu wanaoweza kumsikiliza, na matokeo ya upweke ambayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwake. Katika hali mbaya zaidi kuna visa vya kujiua ambavyo, kwa bahati mbaya, wakati mwingine hufanikiwa." Msaada ambao kila mtu anaweza kutoa ni muhimu, ukitoa nafasi ya siku yao kwa kusikiliza kwa bidii kwa wale walio na shida. Kwa maana hii, Telefono Amico itakuwa hai wakati wa Pasaka na ibada ya kiutamaduni isiyoisha ya Pasaka: watu waliojitolea watakuwa wakishiriki kuanzia saa 4.00 asubuhi Jumamosi hadi saa 6 za usiku wa Jumatatu ya Pasaka”.

Msaada wa nguvu, pia kwa sababu ya ukweli kwamba vipindi muhimu zaidi kwa afya ya akili mara nyingi hupatana na likizo. Shirika la hiari linalojulikana sana ni hatua muhimu ya usaidizi, ambayo hata hivyo haipaswi kugeuza mawazo kutoka kwa kile kinachohitajika ili kuwasaidia vyema wale wanaokabiliwa na matatizo haya kwani Mwaka huu 2023, katika Siku ya Afya Duniani ina mada ya upatikanaji wa matibabu, swali la wazi kwa sababu si kila mtu anaweza kupata msaada muhimu wa kisaikolojia.  Kwa hiyo "Telefono Amico  yaani Simu Rafiki  inachukuliwa kuwa aina ya msaada wa kwanza wa kihisia, lakini kiukweli watu wengi wanaowasiliana nasi pia watahitaji kufuata njia zilizopangwa zaidi".

07 April 2023, 17:57