Tafuta

Katika nchi nyingi bado kuna mengi ya kufanya ili kuhakikisha wanawake wanamiliki ardhi kwa uwiano sawa na wanaume na kwamba mifumo ya kisheria inalinda haki zao kwa muibu wa  ripoti  ya FAO.  Katika nchi nyingi bado kuna mengi ya kufanya ili kuhakikisha wanawake wanamiliki ardhi kwa uwiano sawa na wanaume na kwamba mifumo ya kisheria inalinda haki zao kwa muibu wa ripoti ya FAO.  

Ripoti ya FAO:kukosekana usawa kijinsia husababisha pengo la 24% la uzalishaji

Zaidi ya theluthi moja ya wanawake wanaofanya kazi duniani wameajiriwa katika mifumo ya kilimo cha chakula, mbayo ni pamoja na uzalishaji wa mazao ya kilimo ya chakula na yasiyo ya chakula,pamoja na shughuli zinazohusiana na kuhifadhi,usafirishaji na usindikaji hadi usambazaji.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuweka mazingira sawa kwa wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya chakula na kilimo kunaweza kuleta ukuaji na kusaidia kulisha mamilioni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limesema  hayo tarehe13 Aprili 2023 katika ripoti mpya. Zaidi ya theluthi moja ya wanawake wanaofanya kazi duniani wameajiriwa katika mifumo ya kilimo cha chakula, ambayo ni pamoja na uzalishaji wa mazao ya kilimo ya chakula na yasiyo ya chakula, pamoja na shughuli zinazohusiana na kuhifadhi, usafirishaji na usindikaji hadi usambazaji.  Lakini katika ripoti hiyo mpya, FAO inasema kuwa kukosekana kwa usawa wa kijinsia kama vile ufursa ndogo kwa wanawake kupata ujuzi na ŕasilimali, na mzigo mkubwa wa wa kuolipwa, husababisha pengo la asilimia 24% katika uzalishaji kati ya wanawake na wanaume wakulima katika mashamba ya ukubwa sawa.  Wafanyakazi wanawake katika sekta ya kilimo pia wanalipwa karibu asilimia 20 chini ya wenzao wa kiume, inasema FAO.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Bwana  Qu Dongyu alinukuliwa akisema kuwa: “Ikiwa tutakabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika mifumo ya kilimo na kuwawezesha wanawake, dunia itapiga hatua katika kushughulikia malengo ya kumaliza umaskini na kuunda ulimwengu usio na njaa”.  Kwa mujibu wa FAO, kuziba pengo la kijinsia katika uzalishaji wa mashambani na pengo la mishahara katika ajira za kilimo kungeongeza pato la taifa kwa karibu dola trilioni moja na kupunguza idadi ya watu wasio na chakula kwa milioni 45, wakati ambapo njaa inaoongezeka ulimwenguni. 

Ripoti hiyo aidha inaonesha kwamba upatikanaji wa ardhi kwa wanawake, huduma, mikopo na teknolojia ya kidijitali uko nyuma ya wanaume, huku mzigo mkubwa wa huduma zisizo na malipo unapunguza fursa zao za elimu, mafunzo na ajira. FAO inasema kuwa kanuni za kijamii za kibaguzi zinaimarisha vikwazo vya kijinsia kwa maarifa, rasilimali na mitandao ya kijamii, kuwazuia wanawake kutoa mchango sawa katika sekta ya kilimo cha chakula. Katika nchi nyingi bado kuna mengi ya kufanya ili kuhakikisha kuwa wanawake wanamiliki ardhi kwa uwiano sawa na wanaume na kwamba mifumo ya kisheria inalinda haki zao, inasema ripoti hiyo.  Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa katika mifumo ya kilimo cha chakula, majukumu ya wanawake huwa yametengwa na hali zao za kazi zinaweza kuwa mbaya zaidi kuliko za wanaume - zisizo za kawaida, zisizo rasmi, za muda, wasio na ujuzi wa chini, au za wanaohitaji nguvu kazi

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula vile vile linasema kuwa changamoto za ajira kamili na sawa za wanawake katika mifumo ya chakula huzuia uzalishaji wao na kuendeleza mapungufu ya mishahara. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuunda uwanja sawa katika suala la tija ya kilimo na malipo ya kilimo kungeongeza asilimia moja ya pato la taifa la kimataifa, au karibu dola trilioni moja, na kupunguza uhaba wa chakula kwa asilimia mbili, na kufaidika watu milioni 45. Haya ni makadirio ya kushangaza wakati ambapo njaa duniani inaongezeka. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 345 duniani kote wanakabiliwa na viwango vya mgogoro wa uhaba wa chakula mwaka huu, ongezeko la karibu milioni 200 tangu mapema 2020. Kati ya hawa, milioni 43 wako hatua moja mbali na njaa.

Waandishi wa ripoti hiyo pia wanaonesha kuwa miradi ya kilimo ambayo inawawezesha wanawake ina manufaa mapana ya kiuchumi na kijamii. Kwa mujibu wa FAO, ikiwa nusu ya wazalishaji wadogo watafaidika na afua za maendeleo ambazo zililenga kuwawezesha wanawake, ingeinua kwa kiasi kikubwa mapato ya watu milioni 58 wa ziada na kuongeza ustahimilivu wa nyongeza ya milioni 235. Kiwango cha uajiri wa wanawake katika mifumo ya chakula cha kilimo katika baadhi ya nchi zinazoendelea kinaonesha athari inayoweza kuwa nayo afua za kukuza usawa. Kwa mfano, kusini mwa Asia, asilimia 71 ya wanawake wote wanaofanya kazi wameajiriwa katika sekta (dhidi ya asilimia 47 ya wanaume).

FAO inaeleza aidha kuwa ufuatiliaji na kuongeza kasi ya maendeleo ya usawa wa kijinsia katika mifumo ya kilimo cha chakula hutegemea ukusanyaji na utumiaji wa data za ubora wa juu, zinazogawanywa kwa jinsia, umri na aina nyingine za tofauti za kijamii na kiuchumi, ambazo kwa sasa hazipo, pamoja na utafiti mkali wa jinsia. Katika ngazi ya sera, waandishi wa ripoti wanapendekeza hatua za haraka za kuziba mapengo yanayohusiana na ufikiaji wa mali, teknolojia na rasilimali. Wanasema kuwa kuboresha uzalishaji wa wanawake katika sekta ya kilimo kunahitaji uingiliaji kati ambao hushughulikia matunzo na mizigo ya kazi ya nyumbani isiyolipwa, kutoa elimu na mafunzo, na kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi. FAO pia inatetea programu za ulinzi wa kijamii ambazo zimeonesha kuongeza ajira na ustahimilivu wa wanawake. Kwa kweli, utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wakati uchumi unapopungua, kazi za wanawake zinatangulia, kama ilivyokuwa wakati wa janga la UVIKO-19. Wanawake daima wamekuwa wakifanya kazi katika mifumo ya chakula cha kilimo. Ni wakati wa kufanya mifumo ya chakula cha kilimo kufanya kazi kwa wanawake, alibainisha Bwana Qu katika utangulizi wake wa ripoti hiyo.

18 April 2023, 15:38