Tafuta

Ifikapo katikati ya 2023 nchini India itakuwa na watu wengi duniani kuliko China. Ifikapo katikati ya 2023 nchini India itakuwa na watu wengi duniani kuliko China.  (AFP or licensors)

India itapita China kuwa na watu wengi zaidi duniani ifikapo katikati ya 2023

Hili ndilo limeibuka kutokana na makadirio ya Umoja wa Mataifa kuwa idadi ya watu wa India itakuwa watu bilioni 1.4286 ikilinganishwa na wakazi wa China 1.4257 bilioni.Katika nchi 8 nusu ya ukuaji wa kimataifa ifikapo 2050 itakuwa ni Congo,Misri,Ethiopia,India,Nigeria,Pakistan,Ufilipino na Tanzania.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

India itaipita China kama nchi yenye watu wengi zaidi duniani kufikia katikati ya mwaka huu,  haya ndiyo yanaibuka kutokana na makadirio ya Umoja wa Mataifa yaliyochapishwa tarehe 19 Aprili 2023. Idadi ya watu nchini India itakuwa bilioni 1.4286 ikilinganishwa na bilioni 1.4257 za China, kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kuhusu hali ya watu duniani.

Nchi 8, nusu ya ukuaji wa kimataifa ifikapo 2050

Idadi ya watu duniani inabadilika kwa kasi, kwani theluthi mbili ya watu wanaishi katika mazingira ya chini ya uzazi, wakati nchi nane zitachangia nusu ya makadirio ya ongezeko la watu duniani ifikapo 2050 ambazo ni: Congo DRC, Misri, Ethiopia, India, Nigeria, Pakistan, Ufilipino na Tanzania, kwa kupanga kwa upya kiasi kikubwa cha sifa ya dunia ya  nchi zenye watu wengi zaidi. Hii limedhihirishwa na ripoti ya hali ya idadi ya watu duniani 2023 na UNFPA, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu yenye kichwa: "Maisha bilioni nane, uwezekano usio na kikomo: suala la uchaguzi na haki.” Katika miktadha mingi ya uzazi wa chini, wanawake huripoti mapendeleo ya ukubwa wa familia kuliko wanavyofikia.

India itazidi China kuwa na watu wengi sana duniani
India itazidi China kuwa na watu wengi sana duniani

Uthibitisho wa sasa unaonesha kwamba katika nchi za Ulaya na Marekani, kwa mfano, ikiwa wanawake wanaokaribia mwisho wa miaka yao ya uzazi wangeweza kufikia maadili yao ya uzazi, kwa wastani, wangekuwa na watoto zaidi ya wawili tu kila mmoja. Hii pia ni hali katika nchi za kusini na mashariki mwa Ulaya, kama vile Italia, Ugiriki, Hispania na Bulgaria, ambapo uzazi unaotambulika ni sawa na au chini ya watoto 1.5 kwa kila mwanamke. Katika nchi hizo, pengo kati ya ukubwa bora na halisi wa familia ulikuwa wastani wa watoto 0.3 kwa kila mwanamke. Pia kwa mujibu wa ripoti ya UNFPA, inabaanisha kuwa asilimia 44 ya wanawake na wasichana katika wanandoa katika nchi 68 hawana haki ya kufanya maamuzi sahihi kuhusu miili yao linapokuja suala la ngono, kwa kutumia uzazi wa mpango na kutafuta huduma za afya. Na wastani wa wanawake milioni 257 duniani kote wana hitaji lisilofikiwa la uzazi wa mpango salama na wa kutegemewa.

Na Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinaendelea kuongezeka watu ifikapo 20250
Na Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinaendelea kuongezeka watu ifikapo 20250

Kwa njia hiyo vyombo hivi   vinasisitiza ongezeko la wasiwasi wa idadi ya watu na kutoa wito wa kufikiria kwa upya kwa kina juu ya jinsi gani nchi zinavyoshughulikia mabadiliko ya idadi ya watu. “Serikali zinazidi kupitisha sera za kuongeza, kupunguza au kudumisha viwango vya uzazi, lakini juhudi za kushawishi viwango hivi mara nyingi hazifanyi kazi na zinaweza kukandamiza haki za wanawake: Miili ya wanawake haipaswi kuwekwa mateka na idadi ya watu”, Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Natalia Kanem alisema na kuongeza kuwa  “Ili kujenga jamii zinazostawi na jumuishi, bila kujali ukubwa wa idadi ya watu, lazima tufikirie upya jinsi tunavyozungumza na kupanga mabadiliko ya idadi ya watu”. Kanem alisema kwamba “uzazi wa binadamu si tatizo wala si suluhisho. Tunapoweka usawa wa kijinsia na haki katika kiini cha sera zetu za idadi ya watu, tunakuwa na nguvu na uwezo bora zaidi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya haraka ya idadi ya watu. Kufuatilia malengo ya uzazi na kujaribu kushawishi maamuzi ya uzazi ya wanawake kutaishia tu katika kushindwa.”

19 April 2023, 15:14