Rais wa Ukraine Zelensky na mke wake wakati wanasikiliza hotuba ya rais wa Poland wakati wa ziara yake. Rais wa Ukraine Zelensky na mke wake wakati wanasikiliza hotuba ya rais wa Poland wakati wa ziara yake.  (ANSA)

Baadhi ya makanisa katika sehemu ya mashariki ya nchi yamepigwa

Katika maneno ya Rais wa Ukraine Zelensky kupitia Telegram:“Tunasherehekea sikukuu ya Pasaka kwa imani isiyotikisika katika ushindi wetu.” Wakati huo huo Poland na Hungaria zinavunja mshikamano kwa ajili ya Ukraine kuhusu uagizaji wa ngano kutoka nje.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mapigano makali sana yaliendelea katika eneo la mashariki mwa Ukraine ambapo ni  moto halisi  na ukali haujapungua hata  katika usiku wa Pasaka ambao Kanisa la Kiorthodox lilisherehekea Dominika tarehe  16 Aprili 2023. Idadi iliyotokana na shambulio la bomu katikati mwa Donetsk karibu na Kanisa Kuu la Kugeuzwa Sura, wakati mkesha wa Pasaka inadaiwa mtu mmoja alifariki na wengine kadhaa walijeruhiwa. Baadaye Kanisa la la kiorthodox la Mtakatifu  Michele Maalaika Mkuu katika mkoa wa Zaporizhzhia, lililopigwa na makombora ya Kirussi, liliharibiwa. Wakati wa shambulio hilo, hakuna shughuli zozote zilizokuwa zikiendelea.

Naye Rais Zelensky aliandika kwenye Telegram yake kwamba “Leo tunasherehekea Pasaka kwa imani isiyotikisika katika ushindi wetu. Tayari tumetoka mbali. Labda vilele ngumu zaidi vinatungojea. Tutawashinda. Na kwa pamoja tutakutana na alfajiri (...) Bendera ya bluu na njano hakika itainuliwa duniani kote,” alimalizia Zelensky. Kwa mujibu wa Jenerali Mkuu wa Jeshi la Ukraine alilitipoti kuwa “Mapigano makali yanaendelea huko Bakhmut” kwamba adui walianzisha mashambulizi yasiyofanikiwa katika maeneo ya karibu ya Khromove na Ivanivs'ke," katika vitongoji vya nje kidogo ya Bakhmut na jaribio la Moscow kuwazingira wanajeshi wa Ukraine ndani ya jiji hilo.

Dominika tarehe 16 Aprili, Rais wa Urussi Vladimir Putin alikutana na Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu mjini Moscow. Kulingana na taarifa za  Kremlin, pande zote mbili zimethibitisha tena ushirikiano wao wa karibu wa kijeshi. Li Shangfu hasa alisisitiza uhusiano wa nguvu na Moscow wakati wa mkutano wa wao na Rais wa Urussi Vladimir Putin huko Kremlin. “Tuna mahusiano yenye nguvu sana, ambayo yanapita zaidi ya miungano ya kisiasa na kijeshi ya wakati wa Vita Baridi na ambayo ni imara sana, alisema wakati wa mkutano huo, ambao ulitangazwa kwenye televisheni ya Urusi. "Hii ni ziara yangu ya kwanza nje ya nchi tangu niingie madarakani kama waziri wa ulinzi na nimeichagua Urussi, aliongeza kwamba  "asili maalum na umuhimu wa kimkakati wa uhusiano wetu wa nchi mbili".

Kwa upande wa Ulaya, Poland na Hungaria imevunja mshikamano na Ukraine na kuacha kuagiza nafaka kutoka nchi hiyo. Warsaw imetoa sauti ya maandamano ya maelfu ya wakulima na wajasiriamali wadogo, kutokana na ukosefu wa vyombo vya usafiri, sehemu kubwa ya nafaka inayopelekwa Afrika na Mashariki ya Kati imesalia katika maeneo ya Ulaya ya Mashariki na kusababisha bei kushuka, katika sekta za kilimo za ndani. Ikifuatiwa na kuungaziwa na Budapest na ufunguzi wa kuzingatia kuacha uagizaji na Bulgaria.

17 April 2023, 15:24