Tafuta

2023.03.05 Tanzania: Ishara ya mshikamano wa mablanketi kwa ajili ya uturuki imetolewa na Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Tanzania katika Ubalozi wa Uturuki. 2023.03.05 Tanzania: Ishara ya mshikamano wa mablanketi kwa ajili ya uturuki imetolewa na Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Tanzania katika Ubalozi wa Uturuki. 

Tanzania,Dar Es Salaam:Ishara ya mshikamano kwa wahanga wa tetemeko Uturuki

Ishara ya mshikamano kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam Tanzania,ambalo limewakilisha mablanketi katika Ubalozi wa Uturuki,Tanzania ili waweze kufikishwa mahali husika nchini mwao kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la Ardhi lililoikumba nchi ya Uturuki na Siria hivi karibuni.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kufuatia na tukio la tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi ya Uturuki na Siria mnamo tarehe 6 Februari 2023, ni karibu mwezi mmoja sasa ambapo misaada inaendelea kutolewa kwa ajili ya wahanga. Hii ni misaada ya kila aina. Kwa sababu Nyumba, hospitali ofisi na majengo mengi yaliharibiwa sana au kuanguka kabisa,na kusababisha vifo vingi sana na walionusurika wamebaki na baridi na katika hali ya mshtuko mkubwa.

Msaada wa mablanketi  kutoka Tanzania kuelekea Uturuki kwa wahanga wa tetemeko
Msaada wa mablanketi kutoka Tanzania kuelekea Uturuki kwa wahanga wa tetemeko

Hadi sasa ni msafara wa misaada ya kibinadamu kutoka sehemu zote za dunia iliyofikishwa  mara moja  na ambayo bado wanaendelea kupeleka huko Uturuki na Siria kwa ajili ya  familia zilizoachwa bila makazi na vifaa vingi vya kujihami baridi. Ni kutoka katika mataifa yaliyoendelea na yale yanayoendelea kwa kadiri ya moyo wa kibindamu.

Mwakilishi wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania akipokea mablanketi kwa ajili ya wahanga wa nchi yao
Mwakilishi wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania akipokea mablanketi kwa ajili ya wahanga wa nchi yao

Katika muktadha huo hata Kanisa Kuu Katoliki  la Mtakatifu Joseph,  Dar Esa laam , Tanzania, limeunga mkono nchi ya Uturuki kwa kutoa mshikamano wake wa  Mablanketi kwa ajili ya Kaka na dada wa Uturuki waliokumbwa na tetemeko baya la ardhi. Msaada huo ulikabidhiwa katika Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, katika Jiji la Dar Es Salaam, tarehe 2 Machi 2023.

Wawakilishi wa Almashauri ya Walei Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam wakiwa ubalozi wa Uturuki
Wawakilishi wa Almashauri ya Walei Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam wakiwa ubalozi wa Uturuki

Mshikamano huo, unafanya kufikiria kile ambacho Mama Teresa wa Kalkuta alisema kuwa:  “Kile tunachofanya ni tone tu katika bahari. Lakini kama si tone hilo, bahari, ingekosekana”, na msemo mwingine unasema kwamba: “Hakuna tajiri ambaye hahitaji kupokea na  hakuna mtu masikini ambaye hana chochote cha kutoa”.  Kama haitoshi bado methali nyingne “Kutoa ni moyo wala si utajiri”.

Bi Margherita Ikonga Mwenyekiti wa Almashauri Walei Dar akitia saini kwenye  Ubalozi wa Uturuki Tanzania
Bi Margherita Ikonga Mwenyekiti wa Almashauri Walei Dar akitia saini kwenye Ubalozi wa Uturuki Tanzania

Kwa hiyo katika tendo la kukabidhi msaada huo, aliyepokea kwa niaba ya Balozi wa Uturuki alikuwa ni Katibu wa tatu Msaidizi wa Ubalozi huo,  Bwana Oguxgan Balci na wakati huo huo waliokabidhi mshikamano huo kwa niaba ya Kanisa Kuu  la Mtakatifu Yoseph alikuwa ni Bi Margherita Ikongo, Mwenyekiti wa Almashauri ya Walei, Kanisa Kuu la Mtakatifu Yoseph, na  Bi Lima D’Silva, Katibu wa Halmashauri ya Walei, Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar Es Salaam Tanzania.

Unicef: watoto milioni 2,5 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu

Katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki, watoto milioni 2.5 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Hii ni takwimu iliyotolewa hivi karibuni mwishoni mwa Februari na Unicef, wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya mkurugenzi mkuu wa Unicef, ​​ Bi Catherine Russell nchini Uturuki. Unicef ​​​​hadi sasa imefikia karibu watu 277,000 , ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 163,000  na vifaa vya kuokoa maisha, kama vile  vifaa vya usafi, nguo za baridi, hita za umeme na blanketi. Kupitia washirika wake  pia imewafikia zaidi ya watu 198,000 wenye huduma ya kwanza ya kisaikolojia na burudani katika maeneo yaliyo athirika na miji mingine.

Bi Rusell wa Unicef akitembelea maeneo ya tetemeko huko Siria na Uturuki
Bi Rusell wa Unicef akitembelea maeneo ya tetemeko huko Siria na Uturuki

Bi Russell alikumbusha umuhimu wa huduma za kijamii, ikiwa ni pamoja na maji, usafi wa mazingira na msaada wa kisaikolojia kwa watoto walioathirika. Pia alitembelea nafasi inayofadhiliwa na Unicef ​​ya watoto huko Gaziantep, ambapo watoto na wazazi wanapokea usaidizi wa afya ya akili na ushauri nasaha ili kuwasaidia kupona na kurejesha hali yao.  Kiongozi huyo pia alikutana na baadhi ya familia huko Kahramanmaras ikiwa ni pamoja na familia kadhaa za wakimbizi wa Siria, na kuona vituo vya mapokezi vya muda ambapo watu 17,000 wanaishi karibu theluthi moja yao ni watoto. Kwa mujibu wake alisema “Tetemeko la ardhi lilikuwa janga kwa watoto katika jamii zilizoathiriwa. Unapotembea, unaona vipande vya maisha ya kila siku ya familia, kana kwamba yameganda kwa wakati.”

Watu wanaoishi kwenye mahema na wakati kuna baridi
Watu wanaoishi kwenye mahema na wakati kuna baridi

Na wakati huo huo tukirudi kufikiria baada ya zaidi ya miaka 11 ya vita, nchini Siria ambayo kwa hakika tetemeko hili la ardhi linazidisha hali mbaya ya maisha ya watu, njia bora zaidi ya kusaidia ni mchango wa kawaida kwa kila hali ili kuweza kuwafariji kwa namna moja au nyingine, kama “ tone moja langukalo katika bahari”. Kwa hiyo  Nchini Uturuki, Unicef​​​​imeomba dola milioni 196 ili kufikia watu milioni 3, wakiwemo watoto milioni 1.5, na misaada muhimu, maji, usafi wa mazingira, afya na lishe, ulinzi wa watoto, elimu na msaada wa kibinadamu na fedha  kwa  ajili ya watoto walio katika mazingira magumu.

Jimbo la Dar Es Salaam limetoa msaada wa Mablanketi kwa ajili ya wahanga wa Uturuki
05 March 2023, 16:40