Ajali ya baharini huko Cutro,idadi ya waathirika imeongezeka hadi 66
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Eneo lenye miili ya watu waliofariki Dominika iliyopita tarehe 26 Februari ilifunguliwa Jumatano tarehe Mosi Machi 2023 katika eneo la Palamilone huko Crotone. Mwili wa mwisho kupatikana ni mtoto wa kiume wa miaka 5-6. Na Zaidi ya watu sitini walionusurika ambao wako kwenye Cara ya jiji la Calabria, Kusini mwa Italia. Kwa hakika hali ni ngumu sana, kwa sababu kila mmoja wao wa manusuria amepoteza mwanafamilia. Na wakati huo huo watu bado wako katika hali ya mshtuko mkubwa wa kihemko. Na UNICEF na Save the Children pamoja na mashirika mengine yaliyopo na yanayofanya kazi katika dharura yametoa msaada wa awali wa kisaikolojia na kihisia tangu mwanzo. Uingiliaji kati ulilenga kusaidia watoto na familia za kigeni ambazo hazisindikizwa.
Hadi sasa familia zote zilizokuwepo zimeunganishwa tena. Kuna jumla ya familia 7 huko CARA, karibu zote ambazo zilipoteza jamaa katika ajali ya meli. Miongoni mwao ni mmoja alieyetoka Afghanistan na wanafamilia yake 7 wote. Katika mahojiani aliweza kuelezea tabia ya watu kwenye mashua na mkasa wa baharini. Kati ya familia yake, ni yeye tu na binamu yake mwenye umri wa miaka 12 waliokolewa kwa kuogelea kuelekea ufukweni.
Kwa sasa Mashirika yanawasiliana na huduma za kijamii na vituo vya mapokezi ili kufuatilia utunzaji wa watoto, uhamisho wao hadi kwenye vituo vinavyofaa vya mapokezi na uanzishaji wa ulinzi inapobidi. Shughuli ya usaidizi pia zitaendelea katika siku zijazo ili kuhakikisha usaidizi wa kisaikolojia na uanzishaji wa njia za kujumuisha. UNICEF na Save the Children wamekuwa Calabria tangu mwezi Agosti 2022 na timu ya kudumu inayoundwa na mtaalam wa sheria, mfanyakazi wa kijamii, mpatanishi wa kiutamaduni, na mratibu wa kukabiliana na mpaka na hivi karibuni wameimarisha uwepo wao kwenye hilo ili kukabiliana na dharura.
Uingiliaji wa pamoja unafanywa kama sehemu ya mpngo uitwao “PROTECT”, unaofadhiliwa na Kurugenzi Kuu ya Tume ya Ulaya ya Uhamiaji na Mambo ya Ndani (HOME) ili kuimarisha uingiliaji kati wa ulinzi kwa ajili ya wasichana zaidi ya elfu 20, vijana, barubaru na wakimbizi na wahamiaji wanawake nchini Italia. Kwa jumla, tangu 2014 hadi leo, zaidi ya watu 26,000 wamekufa kwenye njia ya Mediterania. Mashirika hayo mawili yanathibitisha umuhimu wa kuhakikisha njia mbadala salama za kuvuka bahari na shughuli za utafutaji na uokoaji ili kuepuka kujirudia kwa mikasa hii.