Ukraine:Mkutano wa UN wapiga kura&mpango wa amani wa China
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mwaka mmoja uliopita, yaani tarehe 24 Februari 2022, saa 11.05 alfajiri kwa saa za huko mashariki ya Ulaya, ambapo ilikuwa saa nne asubuhi nchini Italia, vita vya Ukraine vilianza na mabomu ya kwanza kurushwa na jeshi la anga la Urussi kwenye miji ya nchi hiyo jirani, ambayo pia ilivamiwa na wanajeshi wa kirussi. Vifo vya kwanza vilihesabiwa kati ya watetezi wa Kiukrene na wakaaji wa Urussi, ambao walilenga kuwasili jiji la Kiev katika siku chache baada ya uvamizi huo. Ni miezi kumi na miwili baadaye, hata hivyo, mzozo bado unakabiliwa na mkwamo, lakini unaendelea kuhesabu waathirika wa kiraia na kijeshi wengi sana kupita kiasi.
China imewasilisha mpango wa amani wenye vipengele 12
Katika siku ya terehe 24 Februari 2023 ya kutimia mwaka mzima tangu kuibuka kwa vita nchini Ukraine, serikali ya China iliwasilisha mpango wa amani wenye vipengele kumi na mbili: wa kwanza kati ya vyote “unatoa wito wa kuheshimu uhuru wa kitaifa wa nchi zote”. Mpango wa nane kati ya 12 unasomeka kwamba: “silaha za nyuklia haziwezi kutumika pamoja na zile za kibayolojia na kemikali”. Kwa hiyo China inaziomba Urussi na Ukraine “kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ili kuepuka kushambulia raia au miundo ya kiraia”, lakini pia inapinga: “vikwazo vyovyote vya upande mmoja visivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa”. Katika taarifa kutoka jiji kuu la Beijing nchini China inahimiza “kusitishwa kwa mapigano na kukomesha mapigano nchini Ukraine kwa sababu vita havioni washindi”, na kutoa wito wa “kuzuia mgogoro kutoka nje ya udhibiti na kuunga mkono Urussi na Ukraine ili kuanza tena majadiliano ya moja kwa moja haraka iwezekanavyo na inawezekana.”
Azimio la Umoja wa Mataifa:Urussi ijiondoe haraka katika vita Ukraine
Hata hivyo, saa chache kabla katika mkesha wa kumbu kumbu ya uvamizi huo, nchini China, India na nchi nyingine 30 zilijizuia kupiga kura juu ya azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lililoidhinishwa na ndiyo 141, ambayo inakaribisha “Urussi kujiondoa bila masharti na mara moja kutoka Ukraine kwa amani ya kina, ya haki na ya kudumu kwa kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa”. Nakala hiyo, ambayo ilikuwa na kura 7 dhidi ya, (Urussi, Belarus, Siria, Korea Kaskazini, Eritrea, Mali, Nicaragua) inathibitisha “dhamira ya uhuru, haki, umoja na uadilifu wa eneo la Ukraine ndani ya mipaka yake inayotambuliwa kimataifa”.
Nchi 141 zinazokubaliana ni sawa na wakati ule wa tarehe 2 Machi 2022
Italia pia ni miongoni mwa wafadhili 75 wa azimio hilo. Wengine waliojizuia ni Cuba, Pakistan, Angola, Ethiopia, Algeria, Afrika Kusini, Zimbabwe, Iran, Armenia, Kazakhstan na Uzbekistan. Nchi nyingi za kusini mwa Ulimwengu zinasisitiza umbali wao kutoka katika kile wanachokiona kama vita vya Magharibi. Kwa hiyo idadi ya kura za kuunga mkono za nchi 141 ni sawa na azimio lililoidhinishwa mnamo tarehe 2 Machi 2022.