Tafuta

Tetemeko: mahema ya watu wahanga wa tetemeko la ardhi huku Uturuki na Siria. Tetemeko: mahema ya watu wahanga wa tetemeko la ardhi huku Uturuki na Siria.  (ANSA)

Takriban watu 24,000 wamekufa kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Siria

Idadi ya waathirika wa tetemeko kubwa la ardhi lililokumba Uturuki na Siria siku ya Jumatatu 6 Februari imeongezeka na kufikia zaidi ya 23,800.Hii iliripotiwa na CNN,ikitoa mfano wa mamlaka ya nchi hizo mbili.Shughuli za uokoaji zinaendelea bila kusitishwa.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Katika Janga ambalo lilitokea mnamo Jumatatu tarehe 6 Februari 2023 la Tetemeko kubwa sana nchini Ututuki na Siria,watu wanaendelea kuteseka kwa baridi kali na wakati huo huo makundi ya msaada yakizidisha nguvu zao. Lakini katikati ya mkasa huo mkubwa pia kuna miale ya mwanga. Kwa maa 119 baada ya tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki, mtoto wa miaka kumi na sita alitolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi vya jengo, ambapo waokoaji waliweza kumpata baada ya kusikia sauti yake. Kaskazini-magharibi mwa Siria,  pia mtoto mchanga wa kike alipatikana akiwa hai na ambaye alikuwa bado  amefungwa kwa kitovuwakati  mama yake, alikuwa amekufa kwa sababu ya tetemeko la ardhi. Hayo ni baadhi tu ya masuala ya uokoaji wa ajabu unaoendelea kufanyika katika saa hizi nchini Uturuki na Siria.

Msaada mwingine  wa kimatibabu umepakiwa kuelekea huko Siria kutoka Uwanja wa ndege wa Piza Italia
Msaada mwingine wa kimatibabu umepakiwa kuelekea huko Siria kutoka Uwanja wa ndege wa Piza Italia

Kwa hiyo idadi ya waathirika wa tetemeko kubwa la ardhi lililokumba Uturuki na Siria siku ya Jumatatu 6 Februari 2023 inazidi kuongezeka na kufikia zaidi ya 23,800. Hilo liliripotiwa na shirika la habari la CNN, ikitoa hata mfano wa mamlaka ya nchi hizo mbili. Shughuli za uokoaji zinaendelea bila kusitishwa usiku na mchana kwa sehemu zote mbili husika la janga hilo.

Watu wakiwa wanasali mbele ya makaburi ambayo wameanza kuzika waathirika wa tetemeko huko Uturuki.
Watu wakiwa wanasali mbele ya makaburi ambayo wameanza kuzika waathirika wa tetemeko huko Uturuki.

Vikwazo vya Marekani vyasitishwa kwa Siria

Maamuzi muhimu yamefanywa kufuatia maafa ya kibinadamu yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi. kwa mmfano Marekani ilitangaza kusimamisha kwa muda baadhi ya vikwazo vya kiuchumi kwa serikali kuu ya Siria. Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) pia kilitangaza kuwa kimesitisha kwa muda hatua zake dhidi ya taifa la Uturuki. Umoja wa Mataifa pia uliripoti kuwa zaidi ya watu 5,300,000 huenda ikwa wameachwa bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi nchini Siria tu bila kuweka ile ya Uturuki.

Maombolezo ya watu wakisindikiza geneza kwenye mazishi
Maombolezo ya watu wakisindikiza geneza kwenye mazishi

Msaada wa kibinadamu

Kutoka ulimwenguni kote kuanzia  Marekani, hasa, mfuko wa kwanza wa misaada ya kibinadamu umefikia na hatimaye ukatumwa nchini Uturuki wenye thamani ya dola milioni 85. Helikopta za Marekani(Black Hawk) zinasaidia shughuli za usafirishaji wa ndege kutoka uwanja wa ndege wa Incirlik nchini Uturuki, na kuwapeleka waokoaji mahali wanapohitajika ni mkubwa zaidi.

Wanajeshi Uturuki wakitafuta ndani ya vifusi waathirika wa tetemeko la adhi
Wanajeshi Uturuki wakitafuta ndani ya vifusi waathirika wa tetemeko la adhi
11 February 2023, 12:48