Kila 12 Februari ni Siku ya Kimataifa dhidi ya matumizi ya watoto vitani
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Watoto kuwa Askari, kwa sababu kuajiri na kutumia watoto katika migogoro,ni ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto na sheria za kimataifa za kibinadamu! Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wasichana walioorodheshwa, waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia, na wavulana wadogo pia imekuwa ikiongezeka kwa ujumla wake. Ni uzoefu ambao bila kwenda mbali tumeshuhudia katika ziara ya Kitume hivi karibuni ya Baba Mtakatifu Francisko akiwa huko nchini DRC na Sudan Kusini aliyomalizika mnamo tarehe 5 Februari 2023. Akiwa huko alikutana na waathirika mbali wa masuala yote ya kiunyanyasaji na ukiukwaji mkuu wa makuzi ya watoto na watu wazima kwa ujumla.
Ni zaidi ya milioni miatatu walio hatarini kuandikishwa jeshini
Kwa hiyo kuna watoto zaidi ya milioni 337 walio katika hatari ya kuandikishwa jeshini, idadi ambayo ni mara tatu zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Kuna nchi 18 ambazo, tangu 2016 hadi leo, wana matumizi ya watotoaskari katika migogoro ya silaha kama vile nchini Afghanistan, Cameroon, Colombia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, India, Iraq, Mali, Myanmar, Nigeria, Libya, Ufilipino, Pakistan, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Siria na Yemen. Licha ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, lakini idadi ya kesi zilizosajiliwa zimezidi meongezeka kwa kasi.
Suala la watoto maaskari
Je watoto askari ni wakina nani? Ni swali ambalo linajionesha wazi zaidi kwa sababu mtoto askari ni mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18 ambaye, au ameajiriwa au kutumiwa na jeshi au kikundi chochote cha kiasi chenye silaha. Wavulana, na wasichana, barubaru wameorodheshwa wengi sana ambao sio tu kwenda kupigana, lakini pia hutumiwa sana katika kazi hatarishi kama vile wapelelezi, wajumbe, wapishi wa jikoni, wasaidizi wa kwenda shambani kulinda, na kwa madhumuni ya ngono kwa pande zote za kike na kiume kwa kuorodhesha mambo machahche. Mnamo mwaka mwaka 2019 pekee yake, takwimu za vyombo vya mashirika ya Umoja wa Mataifa zilibainisha kuwa zaidi ya watoto 7,740, wengine wakiwa na umri wa miaka sita tu, waliandikishwa na kutumika kama wanajeshi ulimwenguni kote. Mnamo mwaka wa 2020, ripoti ya Umoja wa Mataifa iliripoti kuwa takriban ya kesi 8600 zilithibitishwa za kuajiri watoto , pia kusisitiza jinsi hali hiyo inavyopuuzwa sana. Wengi waliajiriwa katika vikundi visivyo vya kiserikali, hata kama hapakuwapo na takwimu rasmi.
Na inaweza kuwa makadirio ni makubwa yaliofichwa kwa makusudi, kwa sababu ni suala ambalo lilichukuliwa kuwa haramu na mikataba ya kimataifa, ambapo suala hilo bado limeenea sana katika mataifa. Kwa sasa, kuna makumi, labda mamia ya maelfu ya watoto walioandikishwa katika vikundi vyenye silaha na wanaohusika katika migogoro. Katika maeneo hayo, kwa hakika watoto wanakuwa sehemu ya jeshi au kikundi kwa sababu mbalimbali. Wengine hutekwa nyara, kama tulivyelezwa na mashuhuda wa hivi karibuni huko Afrika, kutishiwa, kulazimishwa au kudanganywa kisaikolojia. Wengine wanasukumwa na umaskini na hitaji la kuishi sehemu nyingine baada ya kijiji chao kushambuliwa au baada ya wazazi wao kufariki dunia.
Uandikishwaji wa watoto katika migogoro ya kisilaha ni ukiukwaji
Bila kujali ushiriki wao, uandikishaji na matumizi ya watoto katika migogoro daima unawakilisha ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto na sheria za kimataifa za kibinadamu. Ikumbukwe itifaki ya Hiari ya Mkataba wa Haki za Mtoto kuhusu Ushiriki wa Watoto katika Migogoro ya Silaha, iliyoidhinishwa mnamo mwaka 2000, inaongeza umri wa chini wa kushiriki moja kwa moja katika mapigano ya kisilaha kuanzia miaka 15 hadi 18 na inakataza utumishi wa aina yoyote ya kijeshi au kuajiri watu chini ya umri wa miaka 18. Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ulioidhinishwa mnamo mwaka wa 1998, unaweka kama uhalifu wa kivita kuandikishwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15 katika vikosi vya kijeshi vya kitaifa na matumizi yao katika kushiriki kikamilifu katika uhasama kwenye migogoro ya kimataifa na ya ndani.
Mkataba wa Shirika la Kazi duniani ILO
Mkataba Na 182 wa Shirika la Kazi Duniani, ILO, ulioidhinishwa mnamo mwaka 1999, unafafanua uajiri wa kulazimishwa na wa lazima wa watoto kama mojawapo ya aina mbaya zaidi za ajira ya watoto na inakataza kila aina hiyo ya unyonyaji. Kwa mfano, ni zaidi ya watu milioni 3 kati ya watano wanahitaji msaada wa kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika watu hao milioni tatu, mmoja kati ya wanne alilazimika kuondoka nyumbani kwao na kuwa mkimbizi wa ndani au kukimbilia nchi jirani. Matukio ya usalama kwa wanawake na wasichana yameongezeka sana ikilinganishwa na miaka iliyopita na unyanyasaji wa kijinsia ambao mara nyingi unachukuliwa kuwa sababu ya hatari zaidi nchi zote zenye migororo na kusababisha ongezeko la kuajiri watoto askari.