Burkina Faso:Watu kama 70 wameuawa kwa siku nne tu katika mapigano ya kijihadi
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Mapigano ya umwagaji damu zaidi yalianza mnamo tarehe 17 Februari 20223 wakati wanajeshi wasiopungua 51 waliuawa katika shambulio la kuvizia kati ya Déou na Oursi, karibu na mpaka wa Mali na Niger. Wanajeshi ambao walikuwa wamebadilishwa tu baada ya miezi kadhaa mbele walishambuliwa walipokuwa wakirejea katika kambi yao huko Dori. Vile vile takriban wanajeshi wengine kumi na watano waliuawa Februari 20 wakati kikosi cha Tin-Akoff kaskazini karibu na mpaka na Mali. Kwa mujibu wa vyanzo vya Ulinzi huko Burkina Fasi walibainisha juu ya shambulio kalina wakati huo huo Vyanzo vingine vinaripoti kuwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo. huku 19 wakiwa wamefariki na wengine kadhaa kupotea.
Hata hivyo hali mbaya ya ukosefu wa usalama ilikumbukwa na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Burkina Faso na Niger (nchi nyingine iliyoathiriwa na wimbi la wanajihadi) ambao mwishoni mwa Mkutano wao, waliwaalika waamini wa Kikristo na watu wenye mapenzi mema kwa sala na mshikamano thabiti na wale ambao wameathiriwa moja kwa moja na matokeo ya vita hivi visivyo vya haki vilivyowekwa katika nchi zao. Kwa mujibu wao waliandika kuwa “Tunaomba umoja wa dhamira kwa upande wa wana na binti wa Burkina Faso kukabiliana na ugaidi na matokeo yake yote makubwa”.
Waathirika wa kiraia huongezwa na majeruhi wa kijeshi. Shambulio la hivi karibuni zaidi katika kijiji kimoja kaskazini mwa nchi ni mnamo tarehe 13 Februari 2023 wakati wanaume kadhaa waliokuwa kwenye pikipiki waliposhambulia kijiji cha Sanakadougou katika jimbo la Kossi. Takriban watu 12 walikufa na sita kujeruhiwa. Vile vile kijiji kizima kilichomwa moto na kuwalazimisha wenyeji kukiacha bila kuchukua chochote.
Kuibuka tena kwa mashambulio ya vikundi vya wanajihadi kunatokea wakati wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa wakiondoka katika eneo la Burkina Faso, kutokana na mizozo na utawala wa kijeshi ambao ulichukua madaraka kwa mara ya pili mnamo Septemba iliyopita. Mbali na waaadhirikaa, takribani watu 10,000 katika miaka 7, za ghasia zimesababisha kuhama kwa watu wote kutoka maeneo yenye usalama zaidi. Inakadiriwa kuwa nchini Burkina Faso kuna wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 2, jambo linalozidisha hali ya kibinadamu ambayo tayari ni hatari. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) lilitangaza mwishoni mwa 2022 kwamba karibu watu milioni 3.5 watahitaji msaada wa dharura wa chakula katika miezi ijayo.