Marekani:theruji imekwisha ua zaidi ya watu 50 huko New York!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jimbo la Buffalo na New York ndio maeneo yaliyoathiriwa zaidi na vifo 30, watu wengi wakiwa wamekwama ndani ya magari yao, na theluji ikianguka. Gavana Kathy Hochul, ambaye alikuwa ametangaza hali ya hatari kabla ya Noeli , alizungumzia kuwa ni “vita dhidi ya asili ya mama ambavyo vinatupiga kwa kila kitu alichonacho". Mamia ya Walinzi wa Kitaifa walitumwa kusaidia waokoaji na uokoaji zaidi ya 500 ulifanyika wikendi pekee, kutia ndani ule wa mwanamke aliyesaidiwa kujifungua. Dhoruba ya karne hii bado haijaisha, alionya Hochul, ambaye alitoa marufuku ya kuendesha gari katika Kaunti ya Erie, ambako Buffalo iko, kwa saa nyingine 24.
Kimbunga cha bomu'la msimu wa baridi pia kilisababisha vifo na uharibifu huko Vermont, Ohio, Missouri, Wisconsin, Kansas na Colorado. Huko Florida kipimajoto kilishuka chini sana hivi kwamba iguana waliganda na kuanguka kutoka kwenye miti. Lakini hali ya joto ya chini siku hizi ilikuwa yenye digrii -45. Huko Canada, ambapo kumekuwa na vifo 4 hadi sasa, majimbo ambayo yameathiriwa na dhoruba hiyo ni Ontario na Quebec.
Jimbo la Buffalo na New York ndio maeneo yaliyoathiriwa zaidi na vifo 30, watu wengi wakiwa wamekwama ndani ya magari yao, wakati theluji ikianguka katika masaa machache tu. Gavana Kathy Hochul, ambaye alikuwa ametangaza hali ya hatari kabla ya Noeli , alizungumzia kuwa ni vita dhidi ya asili ya mama ambavyo vinatupiga kwa kila kitu alichonacho”. Baridi hiyo pia ilitatiza juhudi za kutoa msaada kwa wimbi jipya la wahamiaji wanaowasili kutoka Mexico. Hali mbaya zaidi iko katika mji wa mpakani wa El Paso, ambapo ukosefu wa vifaa umewalazimu maelfu ya watu kuishi Noeli mitaani.
Kudhalilisha wahamiaji na wakimbizi kwa matumizi ya siasa: Katika tukio hili hata hivyo katika mkesha wa Desemba 24, zaidi ya wahamiaji 100 walipakiwa ndani ya mabasi matatu na kutumwa mbele ya nyumba ya Makamu wa Rais wa Marekani, Bi Kamala Harris mjini Washington, wakati halijoto ilikuwa nyuzi 12 chini ya sifuri. Huu nu Uchokozi wa mara kumi wa gavana wa chama cha Republican, Greg Abbott ambako Ikulu ya Marekani ilikosoa ikimtuhumu kwa kuandaa “unyanyasaji wa kikatili na wa aibu na unyonyaji wa kisiasa”.
Walifika katika eneo la Naval Observatory, anakoishi makamu wa rais, wahamiaji hao wakiwa wamevalia nguo nyepesi, wengi wao wakiwa fulana tu, waliokolewa mara moja wakiwa na blanketi na vyakula vya moto na kupelekwa katika Kanisa la jirani. Hii si mara ya kwanza kwa Abbott kutumia hali ya kukata tamaa ya maelfu ya watu wanaokimbia vita, uhalifu na umaskini kwa malengo ya kisiasa. Mwezi Septemba iliyopita alikuwa ametuma wahamiaji 50 mbele ya nyumba ya Harris, wakati gavana wa Florida Ron DeSantis alikuwa ametuma mamia ya watu kwenye kisiwa cha chic cha Marekani, katika shamba la mizazabibu la Martha.