Jumuiya ya Mt.Egidio na Mpango'Rigiocattolo'kwa ajili ya Afrika 2022
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inawaalika wote na wenye mapenzi mema katika kununua mchezo au michezo ya watoto kwa ajili ya Afrika 2022. Huo ni mpango ambao unaona udhihirisho wa watoto na vijana wanaohusika katika mwaka huu katika mipango ya Jumuiya hiyo na ambapo huko jijini Milano Italia umefikia toleo lake la 22. Vijana kutoka Nchi ya Upinde wa mvua (imejikita katika miji mbali mbali ya Italia), wakisaidiwa na wenzao kutoka shule na vikundi vingi vya jiji, ambao watauza michezo na vitabu vilivyotumika kwenye viwanja, vitu ambavyo vilikusanywa na kupangwa kwa upya wakati wa mwaka mzima ili kuzuia upotezaji na kusaidia asili.
Makusanyo ya fedha kutokana na mauzo hayo yatakwenda kusaidia Mpango wa DREAM, yaani Ndoto kwa mtazamo wa kimataifa wa matibabu ya UKIMWI katika nchi kumi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinajumuisha:(Msumbiji, Malawi, Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Guinea, Guinea Bissau, Nigeria, Angola, Demokrasia ya Congo, Cameroon), mpango ulioanza mnamo mwaka 2002 na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.
Mpango wa Dream unathibitisha tena haki ya kutunza kila mtu, na hasa kwa watoto wa Kiafrika ili waweze kuwa na maisha marefu mbele yao ambayo wangependa kila mtoto wao awe na haki yake. Mpango wa Rigiottolo pia huko mstari wa mbele katika kulinda mazingira na kuelimisha vijana kuhusu ikolojia: kwa sababu michezo haitupiwi bali inatengenezwa kwa upya, kuweza kutumika tena na hivyo kusaidia kuzuia mtawanyiko zaidi wa plastiki kwenye mazingira, kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo.
Aidha wamebainisha kwamba Viwanja ambavyo vinawaona vijana wa Upinde wa mvua ni vile vya Roma, Napoli, Novara, Milano, Genova, Bari, Firenze, Catania, Messina, Livorno, Pisa, Padova, Trieste, Parma na baadaye Paris, Barcelona, Madrid, Manresa na tena Antwerpen, Genk na Liège nchini Ubelgiji, Gladbach na Würzburg nchini Ujerumani. Huko Milano mpango huko Rigiocattolo unafanyika Jumamosi na Dominika tarehe 17-18 Desemba 2022 katika uwanja wa Mtakatifu Carlo kwenye kona na njia ya Vittorio Emanuele, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 1.00 za jioni.