DRC:Zaidi ya watu 120 wamekufa kwa mafuriko,mitaa ya Kinshasa
Na Angella Rwezaula;- Vataican.
Kuna mitaa 24 ya Kinshasa ambayo wanaishi karibu milioni 12 kati ya watu milioni 17 kwa ujumla wanaoishi humo na ambao wamepata madhara makubwa yaliyotokana na mafuriko ambayo yaliukumbwa mji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) usiku wa kuamkia kati ya tarehe 12 na 13 Desemba 2022. Inasadikika vifo vingi sana ambapo walio wengi ni watoto waliokufa baada ya nyumba zao kuanguka katika mtaa wa Binza Delvaux, kata ya Ngaliema. Kanisa mahalia limetuma salamu za rambi rambi kwa kile kilichotokea. Hata ukaribu kwa watu waliokumbwa na janga hilo pia umeonesha na Askofu Mkuu wa Kinshasa, Kardinali Fridolin Ambongo, Ofm Cap. Kwa upande wa Askofu Crispin Kimbeni wa Jimbo la Kisantu, akiwaelekeza Dekania ya Kimwenza ambayo iko Kishasa lakini ambayo ni sehemu ya Jimbo la Kisantu aliwashauri watu wote watoe msada wa mshikamano mkubwa kwa wale wenye kuhitaji.
Kwa mujibu wa Askofu Kimbeni amesema kuwa: “Nchi ambayo kwa ugumu wake inatambua kipindi kigumu chini ya mantiki zote. Kwan gazi ya kijamii, watu wako wanaishi hali ngumu ambayo haijawahi kutokea, Licha ya majengo mapya na ujezni wa wa makani ambayo yamejaa mji, mateso na umaskini vinaendelea kuongezeka. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya matajiri na tabaka alenye kuhitaji ambayo inaongezeka kashfa kwa utajiri wake na kwa na kwa sehemu kubwa ya watu imeundwa wasio na ajira, licha ya kuwa na vyeti vya mafunzo ya chuo kikuu na vyuo vya juu”.
Askofu akiendelea alisema: “Wasio na ajira ndio hasa kipimo cha kudorora kwa kiwango cha kiuchumi cha watu. Kiukweli, licha ya kuonekana kwa kuchanua kwa kiungo cha kiuchumi, watu wana matatizo makubwa kutokana na ukosefu wa kazi, vyombo vya usafiri, miundombinu ya kutosha ya biashara ... Muktadha wa kisiasa unaongeza zaidi matatizo ya wakazi wa Congo: uvamizi wa Congo na nchi jirani, hasa Rwanda na Uganda, haisaidii nchi hiyo kujipanga kisiasa. Iwapo jumuiya ya kimataifa itaendelea kufumbia macho hali ya Congo, tunaweza kuwa katika hatari ya kuona msiba kwa Afrika yote ya Kati. Wakongo wanaogopa kuachwa na kila mtu na wanataka kujilinda, na hivyo kuendeleza chuki dhidi ya wageni”.
Kuhusiana na matazamio ya Ziara ya Papa , Askofu Kimbeni amesema: “Nchi inasubiri kuwasili kwa Baba Mtakatifu Francisko anayetarajiwa mnamo tarehe 31 Januari 2023. Kwa njia hiyo maandalizi hayajawahi kusimama kwa sababu ni matumaini ya kumkaribisha Baba Mtakatifu katika ardhi yetu, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Uthibitisho wa hivi karibuni umetuchochea kuharakisha na kukamilisha kazi huko Ndolo, ambapo Misa Takatifu itaadhimishwa Jumatano tarehe 1 Februari 2023. Watu wote wamepokea kwa shauku na shukrani zawadi hii ambayo Papa Francisko anataka kutoa kwa nchi nzima, hasa katika kipindi hiki maalum cha kihistoria.” Askofu Kimbeni akiakisi ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali kwa kuzingatia ziara hiyo ya Papa alisema: “Sisi katika jimbo la Kisantu tunaendelea kwa namna nzuri. Mapadre wengi watakuwepo kwenye sherehe mbalimbali zilizoandaliwa. Hizo ni pamoja na misa ya tarehe Mosi Februari 2023 huko Ndolo, mkutano wa maombi utakaofanyika alasiri ya tarehe 2 Februari 2023 katika Kanisa kuu la Kinshasa.” Kulingana na makadirio ya maafisa wa afya wa eneo hilo, jimbo la Kisantu lina wakazi 1,155,742.
Katika mafuriko hayo watu zaidi ya 120 wamekufa na salamu za rambi rambi za UN
Katika mafuriko yaliyoambatana na maporomoko ya udongo na kusabisha vifo,majeruhi wengine wengi na nyumba kuharibiwa, kati ya tarehe 12 na 13 huko Jamhuri ya kidemokraisia ya Congo (DRC, Katibu Mkuu wa UN Bwana Guterres ametoa salama za rambi rambi kwa sababu ya Mafuriko hayo kukatimsha maisha ya zaidi ya watu 120. Katika tukio hilo la mafuriko Bwana Antonio amesema kushtushwa na idadi ya watu waliopoteza maisha na uharibu mkubwa uliosababishwa na mafuriko makubwa kuwahi kuikumba nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC, tangu mwaka 2019. Kupitia taarifa iliyotolewa tarehe 14 Desemba 2022 na msemaji wake mjini New York Marekani, Bwana Antonio Guterres amesema “Mvua kubwa zinazonyesha na kusababisha mafuriko mjini Kinshasa na katika baadhi ya majimbo ya DRC yamesambaratisha nyumba na mashamba, pamoja na shule na miundombinu mingine ya umma.” Kwa mujibu wa duru za habari zaidi ya watu 120 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mafuriko hayo yaliyoambatana na maporomoko ya udongo na kujeruhi wengine wengi.
Hali hiyo imemfanya hata Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi aliyekuwa ziarani Marekani kwa ajili ya mkutano baina ya Marekani na Muungano wa Afrika AU kukatisha ziara na kurejea nyumbani ambako kumetangazwa siku tatu za maombolezo kwa ajili ya waliopoteza maisha. Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika, serikali na watu wote wa DRC huku akiwatakia ahuweni ya haraka majeruhi. Amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unaonesha mshikamano na DRC ukisaidia hatua za kukabiliana na hali hiyo. Duru zinasema mji wa Kishasa wenye wakati wapatao milioni 15 umeathirika sana huku nyumba, barabara na miundombinu mingine ikifunikwa na maji.