Tafuta

Mkutano wa COP15 huko Canada:Bi Elizabeth Maruma Mrema,katibu mkuu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai (CBD) . Mkutano wa COP15 huko Canada:Bi Elizabeth Maruma Mrema,katibu mkuu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai (CBD) . 

COP15,Montreal,Canada:kuunda mfumo mpya wa Bioanwai duniani

Mfumo wa baada ya 2020 wa Ulimwengu wa Bioanwai ndio mpango kabambe zaidi wa kimataifa ambao haujawahi kutengenezwa kwa ajili ya bioanuwai ambao ndio lengo kuu la mazungumzo katika Mkutano wa 15 wa Wanachama wa Mkataba wa Kibiolojia uanonedelea huko Montreal,Canada,tangu 5-17 Desemba2022.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Mkutano wa 15 au COP 15 wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu bioanwai, (CBD) unaendelea mjini Montreal Canada ulioanza tarehe 7 Desemba na unatarajia kuhitimishwa tarehe 17 Desemba 2022 ambapo unazikutanisha serikali kutoka duniani kote na wadau wengine muhimu kwa lengo la kuafikiana malengo mapya yatakayoiongoza dunia katika hatua za kubadili mwelekeo na kusitisha upotevu wa bayoanuai ambayo ni tegemeo la viumbe na mazingira ifikapo mwaka 2030. Kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai (CBD) upotevu huo wa bayoanuai unaongezeka kwa kasi ambayo inatishia mustakabali wa dunia kwani uhai wa viumbe vyote vilivyomo duniani unategemea bayoanuai na matendo ya wanadamu ndio chachu ya upotevu huo. 

Bi Mrema Katibu Mkuu CDB katika Mkutano wa COP15 huko Canada
Bi Mrema Katibu Mkuu CDB katika Mkutano wa COP15 huko Canada

Katibu mkuu wa (CBD), Bi Elizabeth Maruma Mrema  akizungumza na Vyombo vya habari vya Umoja wa Mataifa (UN News) wakati akiwa  katika mkutano huo mjini Montreal Canada unaondelea ameeleza ni kwa nini mkutano huo wa kuchukua hatua ni muhimu.  Kwa mujibu wake anasema ni muhimu kwa sababu hasa ni kutokana na ripoti zilizotolewa hivi karibuni na wanasayansi na wanabaolojia, ripoti zote zinasema matendo yetu sisi binadamu dhidi ya bayoanuai ndio yanasababisha hali mbaya ya dunia tuliyofikia wanasayansi wanatuambia tumeshasababisha bayoanuai kupotea kwa asilimia 97, tumechafua hali ya ardhi kwa asilimia 75, bahari majiasilimia 66 pia tumechafua maeneo kwa asilimia 85, matumbawe kwa asilimia 50 yote imepotea.”

Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai
Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai

Bi. Mrema kwa kukazia zaidi alifafanua kwamba binadamu hawawezi kuishi bila bayoanuai  kwa sababu bayoanuai ndio inayotupa chakula, ndio inayotupatia maji ya kunywa na kutumia na ndio inayotupa madawa. Pia bioanuai ndio inayopatia watu sio tu chakula bali na maisha, kazi, makazi yanatokana pia na hii asili. Ameendelea kusema kwamba wanasayansi wameweka bayana kuwa wanadamu wamesababisha hali mbaya ya mazingira katika kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika Ulimwengu huu, hivyo kama hakuna kitakachofanyika wakati huu na kwa haraka ina maana vizazi vijavyo, watoto wao, wajukuu zao watakuwa hawana mahali pa kuishi wakati wao kama  watu wazima walioko sasa hivi ndio waliochafua hayo mazingira.

Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai
Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa CBD, wanasayansi wanasema licha ya maafa yote yaliofanyika kuharibu bayoanuai bado asilimia 50 ya maendeleo ya nchi yanatokana na bayoanuai ambayo ni sawa na dola bilioni 44 kwa mwaka ambazo zinatokana na faida ya bayoanuai. Kwa mantiki hiyoameongeza kusema amesema inapoendelea hali halisi ya kuharibu bayoanuai ni kuzikosesha fursa nchi za ajira ya kazi zote zinazotokana na bayoanuai.  Ili faida itokanayo na bayoanuai iweze kuendelea kuwepo kwa kizazi hiki na vijavyo Bi. Mrema amesisitiza kwamba “Ili bayoanuai iweze kusaidia wananchi ni lazima ilindwe, inahitaji iangaliwe vizuri, uhudumiwe na pale ilipoharibika iweze kurudishiwa na manufaa yanayotokana na bayoanuai yaweze kugawanywa bila upendeleo kwa watu wote hasa tukiangalia wale watu wa asili ambao maeneo wanayokaa ndiyo wanasayansi wamesema yana bayoanuai nzuri zaidi na endelevu kuliko sehemu zingine zote.”

Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai
Mkutano wa Cop15 unaendelea nchini Canada kuhusu Baoianuai

Kwa kutambua hilo CBD inasema ndio maana dunia nzima kwa sasa iko Montreal Canada wakijadiliana ili kuweza kuja na mfumo mpya wa bayoanuai utakaoweza kuisaidia dunia sio tu kupunguza upotevu wa bayoanuai bali kuukomesha kabisa kabla ya mwaka 2030 ambao ndio ukomo wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Bi. Mrema amefafanua kuwa mfumo huo mpya utahakikisha bioanuai inalindwa kwani mfumo mpya una malengo kamili ambayo yatawezesha kuwafikisha hapo kwenye,  malengo ambayo ndani yake yatakuwa na malengo ya hatua ambazo kila nchi itapaswa kuzichukua, na kila nchi itatakiwa pia kutoa ripoti inafanya nini ili kuweza kuchangia katika kuhakikisha upotevu wa bayoanuai unakomeshwa.”  Katika Mkutano huo wa  majuma mawili Bi  Mrema alieleza matarajio yao  kwamba wanatategemea baada ya muda huo  viongozi walioko hapao waweze kukubaliana na huo mfumo, ambao sasa utawezesha kuiongoza dunia nzima na umuhimu utakaofuata baada ya hapo ni kuhakikisha huo mfumo mpya au mkataba mpya tutakaokubaliana unatekelezwa katika nchi. Isipofanyika hivyo inamaana tutakuwa na mkataba kwenye karatasi ambao hautasaidia kurudisha maji tunayopoteza, kuchafua hewa, madawa tunayohitaji na pia kuhakikisha bayoanuai inaendelea kutupatia kazi.”

COP15 NCHINI CANADA
13 December 2022, 10:36