Afrika nzima inashabikia Morocco katika michuano ya kombe la Dunia
Na Angella Rwezaula; Vatican.
Macho na masikio ni kutazama na kusikiliza kile kinacho endelea huko Qatar katika michuano ya Kombe la dunia 2022. Kwa upande wa Padre Francesco Giuliani, mmisionari wa Italia katika nchi ya AfrikaKaskazini akihojiwa na Vatican News kuhusiana na matazamio ya ushindi alisema timu ya taifa ya Morocco inajitahidi kutumia mbinu zote za kimpira kwa kuwa na wachezaji wengi wanaocheza kwenye timu mbali mbali za Ulaya na kushinda katika moyo wa Afrika. Walishinda kundi 'F' la Kombe la Dunia huko Qatar wakichuana na Croatia na kuwaondoa Ubelgiji na Canada. Baadaye Hispania katika mchakato wa hatua ya timu 16 bora na Ureno katika robo fainali, ikiwa na bao moja pekee lililofungwa, kwa kujifunga dhidi ya Canada.
Baada ya Cameroon, Nigeria, Senegal na Ghana, timu ya Afrika Kaskazini inatazamia kufanikiwa katika Kombe la Dunia la Qatar, lililojaa wanasoka wengi waliozaliwa Ulaya, amesisitiza Padre Francesco Giuliani, mmisionari wa Consolata katika katika maoni kuhusu ushindi huo na matarajio ambao amebainisha kwamba “lengo lililofikiwa na Morocco ni furaha kubwa kwa sababu kwa nchi inawakilisha changamoto na ushindi. Tuseme inawakilisha fursa ya kuwasilisha hali halisi ya mtu kwa mataifa mengine ya Dunia. Kombe Lakini si hivyo tu, ushindi huu pia ni fahari kwa Afrika yote”.
Utambulisho wa kimichezo
Katika kusherehekea ushindi kati ya mchuoano na Ureno alisema padre huyo kuwa "niliona jambo fulani na lazima niliseme jambo zuri. Msikiti ulio hapa karibu na Kanisa letu vimefungua milango yake. Watu wengi kabla ya kwenda kuandamana na kucheza barabarani walipitita karibu na msikiti kumshukuru Mungu kiukweli ili kupata neema hiyo kwao". Kwa maana hiyo Mmisionari huyo alisema na ukweli wa pili ambao ni ule wa sherehe kama vile sherehe ya familia na watoto, akina mama na familia nzima wakitembea kwenye barabara ili kujiunga na umati na kushangilia timu yao ya taifa kwa furaha kubwa. Kwa njia hiyo ni kusema ukweli huo kwamba ulileta familia pamoja na ilikuwa na uzoefu kama ule ambao kawaida unaona furaha ya kuwa na harusi au ubatizo."
Matarajio
Matumaini ya kimichezo ni kwamba timu ya Morocco itaweza kufikia fainali. Kwa njia hyo Padre Giuliani alieòeza jinis ambavyo wao wako katika kijiji kidogo, kiitwacho Oujda ambacho kiukweli ni jiji kubwa kwenye mpaka na Algeria, na wanasalimiana kwa tabasamu, kana kwamba wanasema 'lazima wafike fainali'. Kwa maana hiyo yeye anafikiria kwamba Kombe hilo la Dunia kwa hakika linaweza kuunda uhusiano muhimu na mzuri sana na nchi ambazo Moroco inawakilisha tayari katika mazungumzo na uhusiano wa kiutamaduni, kijamii, kiuchumi na kifedha. Kwa upande wa Mtawa huyo amesema ni kidogo ni bara la Afrika yote kwa wakati huu ambayo ina mizizi kwa Morocco kwa sababu mafanikio ya michezo ya nchi ni hatua ya mbele katika mchakato wa ukuaji na maendeleo ya bara zima. Barani Afrika soka kwa hakika si mchezo tu lakini ni ukweli unaounganisha mataifa, watu na kuimarisha mahusiano ya kijamii, alihitimisha maoni yake.
Je, Wamorocco wanaamini? kuwa kombe la dunia litakuwa Afrika?
Mashabiki wa Morocco, wakishangazwa na juhudi za upande wao, hakika wanaamini kuwa timu itasimama kidete kwenye kilele cha ushindi. Makumi kwa maelfu ya washabiki waliwasili Qatar kabla ya mechi ya hatua ya 16 bora na tena kabla ya robo fainali. Hata kama walizua hali ya mvurugano wakati wa mechi hizo lakini pia kwa kusubiri pambano la Jumatano tarehe 14 Desemba 2022 kwenye Uwanja wa Al Bayt ambapo inatarajiwa kujisikia kama mechi ya nyumbani kwa upande wa Afrika Kaskazini.