Tafuta

Kupiga marufuku wasichana na wanawake kwenda shule nchini Afghanistan ni jambo lisilo kubalika na Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa kibinadamu. Kupiga marufuku wasichana na wanawake kwenda shule nchini Afghanistan ni jambo lisilo kubalika na Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa kibinadamu. 

Afghanistan:Mashirika mengi kusimisha shughuli za usaidizi

Kufuatia na Mamlaka ya nchi kupiga marufuku wanawake na wasichana kujiunga na sekondari na vyo vikuu nchini Afghanistan,hata masharika ya kimataifa ya kibinadamu yamesitisha shughuli zake hadi itakapowekwa wazi hali halisi hii ya kunyima wanawake na wasichana hadhi yao ya elimu au ubaguzi huo.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

ActionAid imepokea kwa ugumu wa maamuzi ya kusimamisha kwa muda programu zake nyingi nchini Afghanistan hadi picha kamili na wazi itakapojitokeza. kuhusu kupiga marufuku kwa serikali kwa wanawake wanaofanya kazi katika mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs.) “Tumeshuhudia mmomonyoko wa taratibu wa haki za binadamu za wanawake nchini Afghanistan na kufungwa kwa shule za sekondari kwa karibu miezi tisa na baadae kupigwa marufuku kwa chuo kikuu”. Maagizo ya hivi karibuni yaliyotolewa tarehe 24 Desemba ambayo yanazuia wanawake kufanya kazi na mashirika ya kibinadamu kama vile la ActionAid yatakuwa na matokeo mabaya kwa watu wanaotegemea msaada wao,” linasema shirika hilo, ambalo linafanya kazi na zaidi ya watu milioni 15 wanaoishi katika zaidi ya nchi 40 maskini zaidi duniani na wamekuwepo Afghanistan tangu 2002.

Wanawake ni muhimu katika operesheni yoyote ya utoaji wa misaada ya kibinadamu, hasa katika muktadha wa Afghanistan, ambapo ni wanawake pekee wanaweza kuingiliana  kati ba kuboresha hali. Kwa upande wa shirika hili la  ActionAid, wamebainisha kuwa uwezo wa kutoa huduma nchini unategemea wanawake kuanzia  97 ambao wanafanya kazi bila kuchoka kuboresha maisha ya wale wanaowazunguka. Hivi sasa, karibu nusu ya wakazi wa Afghanistan hawana chakula cha kutosha na wanakabiliwa na njaa kali. Majira ya baridi hii, wengi wanakabiliwa na hali tete na hatua za haraka zinahitajika ili kuokoa maisha. Ikiwa wanawake watapigwa marufuku kufanya kazi, watu hawa hawataweza kufikiwa na kusaidiwa. Shirika la ActionAid litasalia katika mawasiliano ya karibu na wabia, wafadhili na maafisa wa serikali ili kuwezesha kubatilishwa kwa maagizo haya haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo, tunasimama katika mshikamano na wanawake, wanaume, wasichana na wavulana kote nchini ambao haki zao, maisha na maisha yao yataathiriwa pakubwa na uamuzi huu. Kwa mujibu wao wamebainisha kuwa wanataka ulimwengu wa haki na endelevu, ambapo kila mtu anafurahia haki ya kuishi kwa utu na uhuru kutoka kwa umaskini na ukandamizaji. Wanafanya kazi kwa ajili ya haki ya kijamii, usawa wa kijinsia na kutokomeza umaskini. Taarifa ya shirika hilo  inahitimisha.

Kupiga marufuku wanawake ni mbaya huko Afghanistan na hatua dhidi ya njaa pia: “Uamuzi wa mamlaka, katika muktadha na kwa kufuata kanuni za kiutamaduni zinazotumika nchini Afghanistan, ni kikwazo kwa kuendelea kwa shughuli zetu hasa hatua dhidi ya njaa”. Hayo yamesemwa pia na shirika jingine lisilo la Kiserikali ambalo lilizaliwa nchini Ufaransa miaka 40 iliyopita ambalo  limekuwa kilipambana dhidi ya njaa katika takriban nchi hamsini duniani kote, ambalo linasitisha kwa muda shughuli zake nchini Afghanistan (lakini shughuli za matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali zitalindwa) na kulaani uamuzi uliotangazwa na mamlaka ya Afghanistan wa kupiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika ya kibinadamu”.Programu zetu zinalenga zaidi watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 na wanawake wajawazito au wanawake walio katika umri wa kuzaa, shirika hilo limeeleza  katika taarifa, huku likihukumu uamuzi huu usioeleweka kwa sababu unaadhibu idadi ya watu dhaifu, hasa walioathiriwa na uhaba wa chakula ambao leo hii umeenea nchini humo.

Action Against Hunger ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limekuwa likifanya kazi nchini Afghanistan tangu 1995 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na lishe kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi katika maeneo ya mbali na kuajiri karibu watu 1,000, ikiwa ni pamoja na wanawake 400. Kati ya mwezi Januari na Julai 2022, ilisaidia karibu watu 500,000 kupitia kliniki zake zinazohamishika na vitengo vya lishe vya matibabu katika mikoa mitano ya nchi huko Kabul, Daykundi, Helmand, Ghor na Badakhshan.

28 December 2022, 10:34