Ukraine,Usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine umeanza tena!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Usafirishaji wa bidhaa za chakula kutoka Ukraine umeanza tena kupitia ukanda wa baharini. Hayo yamesemwa na waziri wa ulinzi wa Uturuki Bwana Hulusi Akar. Kufikia hadi sasa angalau meli sita zimeondoka kutoka bandari za Ukraine. Hivyo kwa sasa, mauzo ya nafaka kutoka Ukraine, mojawapo ya wazalishaji wakubwa duniani ni salama. Upatanisho msingi umetoka huko nchini Uturuki. Kwa hakika, Moscow ilikuwa imetishia kulipua makubaliano hayo baada ya baadhi ya meli zake kugongwa huko Sevastopol. Kwa upande wa Marekani wameridhika na kukaribisha kurejeshwa kwa makubaliano ya ngano, akihimiza Urussi kuipyaisha
Hata hivyo, Moscow bado haijaamua kama kuongeza mkataba wa mauzo ya nje kutoka bandari ya Ukraine. Hii imesemwa na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, aliyenukuliwa na wakala wa Interfax. Mkataba huo unaisha tarehe 19 Novemba. Rais wa Ukraine Zelensky, hata hivyo, anazungumzia matokeo ya kidiplomasia na kusisitiza kwamba Uturuki, Umoja wa Mataifa na "pia wahusika wengine wakuu katika uhusiano wa kimataifa wamechukua hatua kwa wakati na haki".
Kwa upande wa kijeshi pia tarehe 2 Novemba na usiku mapigano makali yaliendelea. Kwa sababu ya mlipuko wa mabomu ya Urussi, njia mbili za mwisho za mawasiliano zenye nguvu ya juu za kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia na mfumo wa umeme wa Kiukreni ziliharibiwa na sasa zimekatika kabisa. Milipuko ilitikisa mji wa Nikopol nchini Ukraine usiku kucha, huku jeshi la Ukraine likiharibu maghala manne ya silaha za Urussi na matangi yaliyokuwa yamebeba mafuta.
Rais Zelensky mwenyewe alikuwa na mazungumzo ya simu tarehe 3 Novemba asubuhi na rais wa Indonesia ambaye atakuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 huko Bali tarehe 15 na 16 Novemba ijayo. Wakati huo huo, Urussi imeibua shutuma kuhusu mjini Kiev kwamba imeundwa 'bomu chafu'. Hilo ilisisitizwa na katibu wa Baraza la Usalama la Urussi, Nikolai Patrushev. Kwa mujibu wake:Tunaamini kuwa mchakato huu haufanyiki bila ushiriki wa nchi za Magharibi, Patrushev alisema katika mkutano wa makatibu wa mabaraza ya usalama ya nchi za CIS huko Moscow.