Ukraine,watoto wakimbizi Ulaya wana wasiwasi kuhusu wakati ujao wa maisha!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Hakuna amani kwa watoto wa Ukraine walioathiriwa na mzozo. Hata wale ambao wamepata hifadhi katika nchi nyingine za Ulaya wanabeba majeraha ya vita katika nafsi na akili zao. Mateso ambayo yamekuwa yakisisitizwa tena na Baba Mtakatifu Francisko kila mkutano,kila sala ya Malaika wa Bwana na hivi karibuni wakati wa Misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro alipozungumzia dhuluma na mateso wanayopata watu wa Ukraine.
Takwimu za utafiti
Kulingana na utafiti wa Save the Children, wenye kichwa "Haya ni maisha yangu na sitaki kupoteza mwaka: uzoefu na ustawi wa watoto wanaokimbia kutoka Ukraine", inabainisha kuwa angalau mtoto mmoja kati ya wawili wa Kiukreni kati ya wale ambao wameiacha Nchi hiyo na kukimbilia katika mataifa mengine ya Ulaya, ana wasiwasi na mashaka kuhusu mustakabali wake. Kwa namna ya pekee asilimia 50% ya vijana walio chini ya umri wa miaka 16 na 78% ya wale walio na umri wa zaidi ya miaka 16 wanakabiliwa na mashaka hayo wakati asilimia 57% ya jumlawanahisi furaha kidogo tangu kuondoka nchini Ukraine. Hakuna hata kile kizuri katika suala la elimu pia kwani viwango vya uandikishaji shuleni katika nchi mwenyeji za Ulaya kwa vijana waliokimbia vita bado viko chini. Takriban theluthi moja hawakuhudhuria shule kabla ya likizo ya majira ya joto na robo hawakuwa na mipango ya kujiandikisha katika taasisi ya ndani katika mwaka wa shule wa 2022-2023.
Wito kwa serikali wenyeji
Kwa sababu hiyo, shirika la kibinadamu linalohusika na sekta ya watoto linazitaka serikali zote husika kuongeza juhudi zao za kuvunja vizuizi vinavyozuia watoto wa Kiukreni kuhudhuria shule, ili kuhakikisha zinapatikana furaha kikamilifu za haki za ulinzi, afya na elimu na kukua kwa amani katika nchi mwenyeji.
Vikwazo katika kujenga urafiki
Utafiti unaotegemea zaidi ya mahojiano elfu moja ya watoto wakimbizi na walezi wao unaonesha wazi kwamba watoto ambao wamekwenda shule hawana uwezekano mkubwa wa kuhisi upweke. Kwa maana hiyo inafaa pia kuzingatia kuwa zaidi ya nusu ya wavulana, wasichana na vijana waliohojiwa, asilimia (57%), wanaamini kuwa hali yao inaweza kuboresha shukrani kwa uwepo wa marafiki kutoka katika jamii inayowakaribisha ambapo asilimia (56%) wana fursa ya kufanya mazoezi ya michezo au asilimia (54%) vitu vya kufurahisha na kujifunza lugha ya kienyeji Wavulana wana uwezekano mkubwa zaidi wa wasichana kuripoti hamu ya kuwa na marafiki katika jumuiya ya mwenyeji (64% dhidi ya 52%, mahalia). Kwa hakika, ripoti inaonyesha kwamba lugha ni kikwazo cha wazi cha kuundwa kwa urafiki wa ndani, katika maandishi vijana kadhaa wanazungumzia ugumu wa kuwasiliana na kuunda mahusiano.
Ni takriban ya wakimbizi milioni 8
Kwa hivyo, shirika la Kimataifa la Save the Children linakumbusha kuwa tangu tarehe 24 Februari 2022 takriban wakimbizi milioni 7.7 wamekimbia kutoka Ukraine ili kutafuta usalama katika nchi nyingine za Ulaya, na asilimia 40 kati yao wanakadiriwa kuwa watoto wadogo. Wengi wao walishuhudia matukio mabaya, walilazimika kukimbia nyumba zao na kuwaacha wapendwa wao. Serikali za nchi wenyeji kwa njia hiyo zina jukumu muhimu katika kuwasaidia watoto na vijana hawa ili hali kama vile wasiwasi na mashaka kutokuwa na furaha zisije kuwa matatizo ya muda mrefu ya afya ya akili.
Majira ya baridi: hali za wakimbizi haziwezeshi urafiki
Waliohojiwa watoto elfu moja wa wakimbizi ambao wameonesha hisia za kutokuwa na wasiwasi, lakini zaidi ya yote wamegundua kuwa licha ya juhudi za serikali, wengi bado wako nje ya mifumo ya shule ya nchi zinazowapokea na kwamba wanachokosa zaidi ni uwepo wa marafiki, hali ambazo uenyeji wake haurahisishi kufahamiana na wenzao”, kwa mujibu wa Antonella Inverno, mkuu wa sera za utotoni na ujana katika shirika la Kimataifa la Save the Children nchini Italia.