Cop27 kwa ahadi na vizingiti barani Afrika
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ingawa nishati ya mafuta imekuwa mgogoro mkuu wa Tabianchi, ambao unaathiri zaidi Afrika, zaidi ya makampuni mia mbili yako yanaanzisha miradi mipya ya uchimbaji na usafirishaji wa gesi kutoka eneo la Afrika, kinyume na ahadi za uondoaji wa hewa ya ukaa. Hili halitaongeza hata kidogo upatikanaji wa nishati kwa Waafrika, ambao kiukweli wataachwa tena peke yao kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, umaskini na ukiukwaji wa haki za binadamu tu lakini pia hata unyonyaji zaidi wa nchi zao. Kutumia vyema rasilimali ya mtu ni mojawapo ya malengo makuu ya serikali nyingi za Afrika. Cha kushangaza ni kwamba wanatazamia faida, tu na hivyo kupuuza athari za mazingira.
Masuala ya kiuchumi pia ni kitovu cha fedha za kukabiliana na mpito wa nishati na madai ya fidia kwa uharibifu uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Nchi nyingi za Afrika, kama vile Algeria, Libya, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Qatar, zimekuwa msingi katika miezi ya hivi karibuni katika kukidhi mahitaji mapya ya gesi barani Ulaya kutokana na mgogoro wa Ukraine. Hatari ni kufunga maisha yao ya baadaye na nishati ya mafuta kupitia upanuzi wa sekta ya mafuta na gesi, na hivyo kupunguza kasi ya mpito wa kiikolojia.
Vile vile, kuna mbio za Ulaya katika kutafuta kupata gesi asilia ikimiminika (LNG) kwenye masoko ya kimataifa ambayo inaweza kuongeza ushindani katika nchi zinazoendelea. Mbio za mafuta na gesi barani Afrika ni tofauti kabisa na malengo ya COP27. Nishati ya mafuta, kiukweli, ndiyo chanzo cha mgogoro mkubwa wa tabianchi ambao sayari inakabiliwa nayo. Walio nyuma ya makampuni 200 na makampuni ya mafuta, gesi na makaa ya mawe ambayo yanatafuta rasilimali mpya na hifadhi katika eneo la Afrika ni wawekezaji wa kigeni na benki za biashara. Alieleza hayo Padre Filippo Ivardi mmisionari wa Kikomboni na mtaalamu wa masuala ya Afrika.
Kwa mujibu wa Padre Ivardi alibainisha kwamba kukimbilia huku kwa nishati ya mafuta, kushughulikia mzozo wa sasa wa nishati pia husababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa hewa chafuzi. kwa maana hiyo ikiwa wataendelea kwa kasi hiyo kufikia 2030, sio tu kwamba itawezekana kupunguza kwa nusu uzalishaji wa CO2 kama inavyotarajiwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa, walakini hii itaongezeka kwa 10.6%. Hata Afrika yenyewe, ambayo inaweza kuwa na uwezo wa ajabu katika suala la nishati mbadala, bado inazingatia gesi, makaa ya mawe na mafuta pamoja na serikali nyingi ambazo kwa bahati mbaya wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi kuliko manufaa ya nchi zao wenyewe au hiyo ya kimataifa.