Mkutano Mkuu wa B20 umehitimishwa huko Indonesia,kisiwa cha furaha
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Mkutano wa Mataifa makubwa yenye utajiri au B20 huko Bali umefikia hitimisho tarehe 14 Novemba 2022. Katika taarifa ya mwisho wa mkutano huo uliofanyika nchini Indonesia wamebainisha jinsi nchi nyingi wanachama zimelaani vikali vita vya Ukraine, na hatia ya kusababisha mateso makubwa ya binadamu na kuzidisha udhaifu uliopo katika uchumi wa dunia. Kando ya mkutano huo pia ilifanyika Kongamano la Kisiwa cha Furaha likiongozwa na mada ya Laudato si' na ambamo vyama, harakati na viongozi wa kidini waliweza kushiriki. Jukwaa liliwasilisha maonesho juu ya mifumo ya ikolojia, na jinsi inavyowezekana kujenga nyumba, Kanisa, hekalu au mashua kwa njia endelevu. Kujenga kwa njia isiyo ya kuchafua inawezekana, alisema Clara Dallas, mjasiriamali wa Kiitaliano ambaye anafanya kazi katika sekta hiyo na amekuwa akiishi Indonesia kwa miaka kumi na tano, akizungumza na mwandishi wa habari wa Vatican, Luca Collodi aliyekuwa anafuatilia mkutano huo moja kwa moja huko Bali nchini Indonesia.
Kwa mujibu wa Bi Clara Dallas, alisema kwamba inahitajika kutumia vifaa kama kenaf au katani, ambayo nyuzi zake ni ngumu sana kwa ajili ya ujenzi wa fanicha, vigae na sakafu. Nyenzo nyingine ambayo inaweza kuwakilisha mustakabali wa uendelevu wa mazingira ni basalt. Alisema kwamba hiyo zana inapatikana sana nchini India na Indonesia kwa sababu inatoka katika mawe meusi ya volkeno na kuna mengi huko Indonesia. Miongoni mwa faida za basalt, ukweli kwamba ni nguvu zaidi kuliko chuma na tini, pamoja na kuchanganya ubora na vifaa kama saruji. Basalt ni ya bei nafuu, ina athari ndogo kwa mazingira na ni rahisi kutumia, alisema mjasiriamali. Inaweza kutumika kutengeneza viwanda katika nchi zilizo kwenye maji ambazo zina basalt nyingi kwa bei ya chini.
Hatimaye, basalt pia hufanya kazi nzuri, iwe ya jua kwa ajili ya joto na baridi , na kuifanya kuwa bora kwa ajili ya kujenga mambo ya ndani ya nyumba. Kwa njia hii Bi Dallas aliongeza kusema kuwa inawezekana kujenga kanisa au hekalu. Nishati kutoka angani na duniani inafyonzwa na kisha kuingizwa kwa njia ya usawa. Juu ya uwezekano wa maslahi ya kibiashara nyuma ya nyenzo hizo za ubunifu, mjasiriamali alisisitiza jinsi alivyokutana na wawekezaji wengi wanaopenda mabadiliko ya bidhaa. Muktadha hu osio wa kipekee kwani wajasiriamali wengine wanaanza, kwa mfano, kujenga paneli za jua za bei ya chini kuanzia na taka taka kutoka akatika matunda ya kiwi na papai.
Indonesia inafafanuliwa kuwa nchi inayoendelea, yenye rutuba na yenye uwezo wa kujitegemea. Kuna chakula, maji, malighafi, nishati, kila kitu kipo. Umuhimu mkubwa sana ni ukweli kwamba ni nchi ambayo imani tano za kidini ziko pamoja. Na hii sio jambo dogo kuona kwamba watu wanaishi pamoja katika vijiji sawa wakijumuika na maungamo madhehemu matano. Kwa maana hiyo migongano ni michache alisisitiza. Walakini, mjasiriamali huyo anabainisha kukosekana kwa uhusiano wa Indonesia na ulimwengu wa nje, hasa na Ulaya kwamba , hata hivyo, kuna watalii wengi na Waitaliano wengi wanaoishi hapo. Jumuiya inaundwa na watu ambao wana maoni sawa. Hata hivyo, mawasiliano, ya kiutamaduni na kibiashara, yanabaki kuwa machache sana. Kwa maana hiyo alisema ni wao kama watalii wanapaswa kupeleka mambo yao ya Ulaya na kujitangaza wafahamike.