Somalia: Unicefu imebainisha juu ya watoto nchini Somalia wanalazwa kila dakika hospitalini kutokana na utapimalo wa kukithiri. Somalia: Unicefu imebainisha juu ya watoto nchini Somalia wanalazwa kila dakika hospitalini kutokana na utapimalo wa kukithiri.  

UNICEF/Somalia:mtoto 1 kila dakika analazwa kwa utapiamlo mbaya

Tangu mwezi Agosti watoto 44.000 wamelazwa kwa sababu ya utapiamlo mbaya nchini Somalia.Ni kusema kwamba analazwa mtoto mmoja kwa kila dakika.Ni kwa mujibu wa UNICEF ambapo katika dharura kama hiyo jibu lake imeunda timu ya kuweza kusaidia kutibu watoto walioshambuliwa na utapamlo,kwa kutafuta kufikia watoto katika maeneo magumu-

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Watoto waliolazwa kwa sababu ya utapiamlo wa kukithiri tangu mwezi Agosti ni zaidi ya arobaini elfu kwa maana ya kusema ni kila dakika analazwa mtoto. Kwa maana hiyo watoto wenye utapiamlo  mbaya sana wanafikia mara 11 ya kufikia hatua ya  kuhara na surua ukilinganisha na watoto wenye lishe bora. Katika mkasa wa namna hi inchini Somalia iko katika kikomo cha kijanga ambacho hakikuwahi kuonekana kwa makumi ya miaka. Kwa mujibu wa Msemaji wa Shirika Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. James Elder katika mkutano na waandishi wa habari katika Jumba la Umoja wa mataifa, huko Geneva tarehe 18 Oktoba 2022 alisema, kwa sas anchini Somalia, kila dakika, kwa kila siku, mtoto mmoja analazwa katika moja ya vituo vya kiafya kwa sababu ya utapiamlo wa kukithiri.

Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF
Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF

Takwimu za mwisho zinaeleza kwamba watoto 44.000 waliolazwa hospitalini kwa sababu ya utapiamlo. Ni mtoto ambaye mama anatembea siku ili kuweza kusaidiwa. Ni mtoto ambaye mwili wake unapambana kuweza kuishi. Ni mtoto ambaye maisha yake yana changamoto kwa kuishi. Ni wazi kwamba watoto ambao wanajikuta nyuma ya  hali kama hii na ya kuongopesha, takwimu ni zile za wale wanaofika katika kituo kwa ajili ya tiba. Katika nchi ambayo ufikiaji wake huko mashakani na mgumu, bado kuna vizingiti vya ugaidi na hatari kwa wahudumu wa kibinadamu, ambapo wanaogopa kwamba maelfu na maelfu ya watoto hawafikiwi msaada ambao wanauhitaji.

Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF
Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF

Hata hivyo katika dharura kama hiyo jibu la Unicef imeunda timu ya kuweza kusaidia kutibu watoto walioshambuliwa na utapiamlo, kwa kutafuta kufikia watoto katika maeneo magumu kuweza kufika. Hadi sasa Unicef imewasaidia watoto 300,000 wenye utapiamlo wa kukithiri; kwa kusafirisha maji ya dharura, yamewafikia watu 500,000 tu kwa miezi mitatu ya mwisho. Lakini shida kubwa bado inabaki ile ya ufadhili. Ikiwa kwa mieizi ya mwisho wamefikiwa fedha za kusaidia, shukrani kwa USAID, shirika moja la Uingereza la kutoa misaada na Tume ya Ulaya, ufadhili wa muda mrefu ni sehemu ya mabadiliko muhimu yanayohitajika ili kuzuia njaa kutokea tena na tena. Kwa mfano, ombi la UNICEF la miaka mitatu la kusaidia familia na jumuiya zao kujenga ustahimilivu katika eneo la Pembe ya Afrika kwa sasa linafadhiliwa kwa asilimia 3 pekee.

Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF
Watoto nchini Somalia wako hatari ya utapiamlo wa kutisha wanahitaji msaada kwa mujibu wa UNICEF

Linapokuja suala la mzozo ambao Somalia inakabiliana nao hivi leo, imekuwa kawaida kufanya ulinganisho wa kutisha na njaa ya 2011, wakati watu 260,000 walikufa. Walakini,  msemaji huyo alibainisha kwamba anachosikia kutoka  kwa wataalamu wa lishe hadi wafugaji  ni kwamba mambo yanaonekana kuwa mabaya zaidi leo hii. Mwaka 2011, baada ya misimu mitatu ya mvua kushindwa kunyesha, idadi ya watu walioathirika ilikuwa nusu ya sasa na hali ya jumla ya  mvua na mavuno ilikuwa ikirejea. Leo hii kuna misimu minne ya mvua zilizoshindikana; utabiri wa msimu wa tano wa mvua ni mbaya zaidi na idadi ya watu walioathirika ni mara mbili ya mwaka 2011. Mambo ni mabaya na kila dalili inaonesha kuwa yatazidi kuwa mabaya. Ikiwa hawataingilia kati na kuwekeza zaidi, watakabiliwa na vifo vya watoto kwa kiwango ambacho hakijaonekana kwa nusu karne.

Janga la utapiamlo nchini Somalia.UNICEF inaomba msaada
19 October 2022, 16:05