Katibu Mkuu wa UN,vita vya Tigray na Ethiopia:lazima kufanya kazi kurejesha amani
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Sio tu vita vya Ukraine vinavyo mfanya Bwana Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa na wasiwasi bali pia alitaka kusisitiza tarehe 17 Oktoba 2022 kwa waandishi wa habari ambao walikuwa wakimsubiri mbele ya wadau kwa ajili ya mawasiliano ya haraka. Kwa mujibu wake alisema “Hali nchini Ethiopia inazidi kuwa mbaya ya udhibiti, vurugu na uharibifu umefikia viwango vya kutisha. Mfumo wa kijamii unasambaratika. Uhasama katika eneo la Tigray nchini Ethiopia lazima ukomeshwe sasa, ikiwa ni pamoja na kujiondoa mara moja na kujitenga kwa wanajeshi wa Eritrea kutoka Ethiopia ”.
Kwa mujibu wa Bwana Guterres, hata katika Pembe ya Afrika alisisitiza kwamba “hakuna suluhisho la kijeshi”. Alipodokezwa kwamba serikali ya Ethiopia na majeshi ya Eritrea ambao siku hizi wanadhani wana ushindi mikononi mwao hawafikiri hivyo, Bwana Guterres alijibu: “Siku zote inakuwa hivi, hata huko nyuma wapo waliokuwa wakidhani tayari wameshinda. Lakini kwa migogoro yote hii hakuna suluhisho la kijeshi, lazima tufanye kazi kurejesha amani”. Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, raia nchini Ethiopia sasa wanalipa gharama mbaya kwani alisema: “Mashambulizi ya kiholela, hata katika maeneo ya makazi, yanaua watu wengi wasio na hatia kila siku, kuharibu na kupunguza upatikanaji wa miundombinu muhimu kwa huduma muhimu.
Mamia ya maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao tangu uhasama umeanza tena mnamo mwezi Agosti, mengi kwa mara ya pili ”. Baadaye Bwana Guterres alielezea hali ya kutisha: “Pia tunasikia ripoti za kutisha za unyanyasaji wa kingono na vitendo vingine vya ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaume. Pande zote lazima zizingatie wajibu wao wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Raia lazima walindwe na pia wafanyakazi wa kibinadamu ambao wanashambuliwa na hata kuuawa, ili kuokoa maisha ya misaada ya kibinadamu. Na kiwango cha hitaji ni cha kushangaza ”.
Hata kabla ya kuanza tena vita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwambia kwamba, watu milioni 13 walihitaji chakula na msaada mwingine huko Tigray, Amhara na Afar. Uwasilishaji wa misaada huko Tigray umesimamishwa kwa zaidi ya wiki saba na usaidizi huko Amhara na Afar pia umesitishwa. Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa Bwana Guterres, pande zote lazima ziruhusu na kuwezesha upitishwaji wa haraka na usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu kwa raia wote wanaohitaji huku kurejeshwa kwa haraka kwa mazungumzo kuelekea njia yenye ufanisi, ya kudumu na ya kisiasa inahitajika. Jumuiya ya kimataifa lazima sasa zikusanyike kwa ajili ya amani nchini Ethiopia”.
Bwana Guterres alisema Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono Umoja wa Afrika kwa njia yoyote iwezekanayo ili kukomesha ndoto hii mbaya kwa watu wa Ethiopia. Hata hivyo, Guterres alisema, Baraza la Usalama linaonekana kugawanyika, kuna wale wanaoamini kwamba mgogoro wa Ethiopia ni mzozo wa ndani na hivyo kwamba hawapaswi kuushughulikia. Kwa hiyo alijibu kwamba: Sidhani hivyo, ni mgogoro ambao umesababisha athari na pia tuna uingiliaji kati wa wanajeshi wa Eritrea ndani ya Ethiopia”.