Mama Teresa wa Calcutta alipokea zawadi ya Tuzo ya Nobel amani mnamo1979. Mama Teresa wa Calcutta alipokea zawadi ya Tuzo ya Nobel amani mnamo1979. 

Siku ya Kimataifa ya hisani:Papa amesema kidogo au kikubwa kinabadili maisha!

Kila ifakapo tarehe 5 Septemba,Umoja wa mataifa unaadhimisha Siku ya Hisani.Katika ujumbe mfupi wa Papakwenye mitandao ya kijamii katika fursa hii amesema iwe kidogo au kikubwa kitolewacho kwa furaha na kwa urahisi kinabadili maisha kuwa hifadhi.Katika ulimwengu uliogubikwa ubinafsi na kutojali wapo watu wa upendo wa kijamii na kidini kama Mama Teresa wa Kalkuta.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe mfupi kwa njia ya mitandao wa Papa Francisko ameandika  “ikiwa kile kidogo unashirikishana kwa upendo, hakiishi kamwe, lakini kinabadilika kuwa hifadhi ya maisha na ya furaha. Na ndivyo inavyotokea kwa sadaka yetu, iwe kidogo au kikubwa kitolewacho kwa furaha na kwa urahisi”. Ameandika hayo katika fursa ya kimataifa ya hisani iadhimishwayo tarehe 5 Septemba.

Chimbuko la siku ya kimataia ya hisani au upendo

Ilikuwa ni mnamo tarehe 17 Desemba 2012 ambapo Umoja wa mataifa ulitangaza kuwa 5 Septemba ya kila mwaka, Jumuiya ya Kimataifa itakuwa inaadhimisha Siku ya masuala ya hisani au upendo Kimataifa. Masuala ya hisani yana jukumu kubwa katika kuendeleza kazi za Umoja wa mataifa. Hili ni tendo ambalo linahusu kujitolea wakati au fedha, na kushiriki katika shughuli za kijamii au za sehemu nyingine duniani, kufanya vitendo vya kusaidia na utu wema bila dhamira ya kulipwa, vitendo hivyo na vinginevyo vya kuonesha mshikamano vinaweza kuusaidia sana Umoja wa Mataifa, lakini pia hata kwa mtu binafasi anayejotolea kufanya hivyo.

Mama Teresa wa Kalkuta
Mama Teresa wa Kalkuta

Haya pia  matendo yanasaidia kuwa na  nia njema ya kuishi pamoja kwa mshikamano na kujenga mustakhabali wa amani kwa watu wote duniani ambao kwa wakati huu na ujao unahitajika, katika ulimwengu ambao umeyumba yumba, uchumi, magonjwa ya mlipuko, maafa mengi ya asili kama ukame, mafuriko, vimbunga na mengine mengi yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.  Hata hivyo ni watu wengi ambao Papa Francisko wakati mwingine anasema kuwa wapo na wako katika  Mlango wa karibu ambao wanatumia muda wao au fedha zao kwa ajili ya kutekeleza masuala ya hisani kwa wengine. Mama Theresa wa Calcutta ni mfano halisi wa jana na leo ambaye alisimama kidete kutangaza na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo. Aliinama kuwasaidia maskini kama vile kuwapaka mafuta ya faraja na divai ya matumaini.

Mama Teresa wa Kalkuta
Mama Teresa wa Kalkuta

Mama teresa alitambua kutetea utu, heshima na haki zao msingi na alikuwa ni sauti ya maskini na wanyonge duniani, katika kuundeleza huo uwepo halisi wa Mungu kati ya maskini wenye kuhitaji. Mama Teresa wa Kolkata (26 Agosti 1910 – 5 Septemba 1997) alikuwa mtawa na mwanzilishi wa Shirika la Upendo aliyejulikana kimataifa hasa kutokana na huduma zake kwa watu maskini katika mji wa Kalkuta nchini India na kwingineko iliyofanya apatiwe tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1979. Katika siku ya leo ambapo anakumbukwa Mama Theresa wa Calcutta kurudi kwake kwa Mungu Baba asaidie kuwa kielelezo cha upendo aminifu wa Mungu kila wakati katika kila jamii. Ikumbukwe  tarehe 19 Oktoba 2003 alitangazwa na Mtakatifu Papa Yohane Paulo II kuwa mwenyeheri. Baada ya muujiza wa pili kufanywa na Mungu kwa maombezi yake,  Baba Mtakatifu Fransisko akamtangaza kuwa Mtakatifu mnamo tarehe 4 Septemba 2016. Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Septemba nsambamba na  Siku iliyotangazwa na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa siku ya kimataifa ya hisani au upendo kuanzia mwaka 2013.

05 September 2022, 17:02