DRC:mvutano huko Goma katika maandamano ya kupinga na kuomba usalama zaidi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mvutano mkali huko Goma nchini DRC mnamo tarehe 26 Septemba 2022 kwa maandamano ya kupinga kwa kile kiitwacho ‘mji uliokufa’ ulioamriwa na mashirika ya kijamii ya Kivu Kaskazini, kuomba kwa upande mmoja kuponya kijiji cha Bunagana kutoka mikononi ya M23 na kwa upande mwingine mwisho wa hali ya kuzingirwa na pia kuondoka kwa MONUSCO (Kikosi cha Utume wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC). Shule, maduka na masoko vilifungwa wakati kulikuwa na usafiri mdogo kwa umma uliokuwa ukizunguka, na wanafunzi wachache sana waliojaribu kwenda shuleni na kulazimishwa kurudi nyumbani.
Idadi ya watu inataka kukomeshwa kwa hali ya hatari iliyowekwa kwenye wilaya tatu za mashariki mwa DRC tarehe 6 Mei 2021 ili kupigana na vikundi vyenye silaha ambavyo vinapanda vifo na uharibifu katika maeneo hayo matatu. Hatima ya mji wa Bunagana, kwa takriban siku 100 mikononi mwa wapiganaji wa M23, imeziunganisha roho za wakazi wa eneo hilo kuomba uingiliaji madhubuti wa jeshi la Congo na kuondoka kwa MONUSCO inayoshutumiwa kwa kushindwa dhamana ya usalama.
Kuzaliwa upya kwa M23, ambacho ni kikundi cha wapiganaji ambao walikuwa wameweka silaha zao chini mwaka wa 2013, pamoja na kuongezeka kwa vurugu huko Kivu Kaskazini, kulisababisha makabiliano makali kati ya DRC na Rwanda, wakituhumiwa na Kinshasa kuwa wafadhili na kupenyeza kwao askari wenyewe chini ya kivuli cha waasi. Shutuma zilirejewa katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Congo, Bwana Felix Tshisekedi ambaye alisema kuwa Rwanda inawajibika kwa uchokozi wa kijeshi na ukaaji wa mashariki mwa DRC, ikiwa ni pamoja na kupitia madai ya Kigali kuunga mkono jeshi la waasi la M23. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA), zaidi ya wakimbizi wa ndani 250,000 wamelazimika kukimbia kutoka maeneo mbalimbali ya kaskazini-mashariki mwa DRC kati ya Juni na Septemba 2022 kutokana na ghasia za makundi yenye silaha.
Hata hivyo askari wa kulinda amani na polisi wawili wa Umoja wa Mataifa wameuawa baada ya waandamanaji kuvamia kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO huko Butembo na kupora silaha za polisi wa kitaifa na kuanza mashambulizi. Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa Habari jijini New York, Marekani Jumaane tarehe 27 Septemba kwamba polisi mwingine amejeruhiwa. “Tunaongeza sauti yetu kwa Kaimu Mkuu wa MONUSCO, Khassim Diagne, tunalaani mauaji ya wenzetu na tunatuma salamu za rambirambi kwa familia na wafanyakazi wenzao,” amesema Bwana Haq.
Bwana Diagne katika taarifa yake ya awali ameelezea ghasia dhidi ya Umoja wa Mataifa kuwa ni jambo lisilokubalika kabisa na halina maana kwa kuzingatia mantiki ya uwepo wa chombo hicho nchini humo kushirikiana na mamlaka kulinda raia na kukabili vikundi vilivyojihami sambamba na kujengea uwezo taasisi za seriklai na na huduma. Ametoa wito kwa mamlaka za DRC, mashirika ya kiraia, vikundi vya kjami kukataa ghasia.