Ukraine:Utume kutoka AIEA utafika katika Kituo cha Zaporizhzhia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Nchini Ukraine, wasiwasi unaendelea juu ya hatima ya kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, kinachodhibitiwa na Warusi na kuwa eneo la mabomu katika maeneo ya jirani. Katika saa chache zilizopita, vyanzo vya habari vya Ukraine vimeripoti, kuwa vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi zaidi ya 200 ya anga kwenye mji wa Orhiv, katika eneo ambalo mtambo huo unapatikana, na kusababisha majeruhi. Waathitika watano, kulingana na vyanzo vya Urusi, kwa uvamizi wa Kiukreni kwenye eneo la Energodar.
Kituo cha Kakhova kilishambuliwa
Mto wa chini katika eneo hilo, kituo cha nishati cha Kakhova, ambacho bwawa lake hutoa nishati kwa ajili ya kiwanda cha nyuklia, pia kilishambuliwa na Warusi. Vipindi ambavyo haviondoi hofu ya ajali ya nyuklia, huku roketi zikiwasili mita mia moja tu kutoka kwa majengo ya kinu mwishoni mwa juma. “Viwango vyote vya usalama vinasalia kufanya kazi na mionzi iko katika kiwango cha kawaida”, imesema Kiev, ambayo anaishutumu Urusi kwa kugeuza mtambo huo kuwa kituo cha kijeshi, wakati kwa upande wa Moscow wanasema kuwa ni vikosi vya Ukraine vinavyohusika na mashambulizi.
Wajumbe 14 kutumwa ili kuona usalama wa nyuklia
Kwa mujibu wa Bwana Rafael Mariano Grossi, ambaye ni mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA amethibitisha kuwa wajumbe 13 watatumwa mwishoni mwa wiki hii na hakuna hata mmoja anayetoka nchini Marekani na Uingereza ili kukagua kiwanda hicho. “Ninajivunia kuongoza utume huo aliandika, na kwamba lazima tulinde usalama wa kinu kikubwa zaidi cha nishati ya nyuklia nchini Ukraine na Ulaya.
Tusitishe silaha za nyuklia
Na kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres, amesema “Hebu tusitishe silaha za nyuklia kwa historia, mara moja na kwa wote”, na kuongeza kuandika kwenye twitter kuwa: “Ulimwengu wetu umeshikiliwa na silaha za nyuklia kwa muda wa kutosha. Vifaa hivi vya kifo havihakikishii ushindi au usalama, viliundwa kwa matokeo pekee ya kuharibu". Wakati huo huo, wapiganaji wa Urusi waliingia katika anga ya Belarus Jumapili usiku na kufyatua angalau makombora matano dhidi ya ardhi ya Ukraine, huku majengo 30 yakiwemo hospitali yakiharibiwa kutokana na shambulizi la usiku la Urusi katika wilaya ya Sarny. Makombora matano pia yalipiga mji wa Kherson.