2021.08.18 Siku ya Kimataifa ya Msaada wa Kibinadamu 2022 inayoandalia na (OCHA) 2021.08.18 Siku ya Kimataifa ya Msaada wa Kibinadamu 2022 inayoandalia na (OCHA) 

OCHA:#ItTakesAVillage ni kampeni ya Siku ya Msaada wa Kibinadamu

Katika siku ya kimataifa ya Msaada wa kibinadamu mwaka 2022 inamulika wale watoao misaada kwenye maeneo yao.Hawa ni watu ambao wanapokea wakimbizi na kutoa misaada mingi ambayo haijulikani kwa vyombo vya habari na wala mitandao ya kijamii.Katika wiki moja OCHA imeendesha kampeni iitwayo:#ItTakesAVillage ambayo kila mtu anaweza kushiriki kwenye mtandao wa kijamii na kutoa maoni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA katika kuelekea siku ya kimataifa ya Msaada wa kibinadamu mwaka 2022 ifanyikayo kila tarehe 19 Agosti imesema kuwa ‘inahitaji juhudi za watoa misaada ya kibinadamu ili kusaidia jamii inayokabiliwa na majanga. Kwa mfano nchini Uganda, huko Afrika Mashariki linalopokea wakimbizi, misaada hutoka si tu kwa mashirika ya kimataifa kama yale ya Umoja wa Mataifa bali pia watu binafsi. Kwa maana hiyo wakimbizi kutoka Congo DRC, na wakimbizi kutoka Sudan Kusini wameweza kusaidiwa iwe nchini Uganda, lakini hata Waganda wamesaidiwa nchini  Tanzania na wenyeji. Watu ni wengi duniani ambao wanasaidiwa kwa namna moja au nyingine na watu mahalia bila kusubiri mashirika ya kimataifa.

Watu wengi na familia na watoto wanahitaji msaada wa kibinadamu
Watu wengi na familia na watoto wanahitaji msaada wa kibinadamu

Katika wiki moja OCHA imeendesha kampeni iitwayo, #ItTakesAVillage ambayo kila mtu anaweza kushiriki kwenye mtandao wa kijamii na kutoa maoni, kuchapisha au kushirikisha wengine kama njia ya kuonesha mshikamano na watu wanaohitaij msaada na shukrani kwa wale wanaoweka rehani maisha yao kusaidia wengine.

Watu wengi na familia na watoto wanahitaji msaada wa kibinadamu
Watu wengi na familia na watoto wanahitaji msaada wa kibinadamu

Mnamo 19 Agosti 2003, kulitokea shambulio katika Hoteli ya Canal huko Baghdad, Iraq, ambayo  iliua wafanyakazi na wahudumu  22 wa utoaji  misaada, akiwemo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Bwana Sergio Vieira de Mello. Miaka mitano baadaye, mwaka 2009, Baraza Kuu lilipitisha azimio A/RES/63/139 linaloitaja kuwa 19 Agosti iwe  Siku ya watoa Misaada ya Kibinadamu Duniani. Hii ni fursa ya kusherehekea wafanyakazi wa utoaji  misaada ya kibinadamu duniani kote, lakini pia wale ambao wamepoteza maisha yao huku wakisaidia maskini zaidi, watu waliotengwa na wanaoishi katika mazingira magumu. Kila mwaka, Siku ya Kutoa msaada wa Kibinadamu Duniani huzingatia mada, inayoleta pamoja washirika kutoka katika mfumo wa kibinadamu ili kutetea uhai, ustawi na utu wa watu walioathiriwa na migogoro na usalama wa wafanyakazi wa kibinadamu. Mwaka huu 2022, madhumuni ya Siku hii yanayomulika wale wote watoao misaada kwenye maeneo yao bila kusubiri nani aanze au mashirika.

SIKU YA KIMATIAFA YA MSAADA WA KIBINADAMU 2022
19 August 2022, 12:03