Tafuta

Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika TICADS8: 27-28 Agosti 2022. Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika TICADS8: 27-28 Agosti 2022. 

Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika, TICAD8, Tunis, Tunisia

Serikali ya Japan inapenda kukazia zaidi kuhusu ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa baada ya maambukizi ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, kwa kujikita katika maendeleo ya viwanda yenye ushirika na maendeleo fungamani ya binadamu Barani Afrika. Serikali ya Japan tangu mwaka 1993 imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo fungamani Barani Afrika, TICAD8

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika “Tokyo International Conference on African Development (TICAD8)” unaanza rasmi tarehe 27 hadi tarehe 28 Agosti 2022 huko Tunis, Tusinia kwa kuwashirikisha wajumbe kutoa nchi mbalimbali za Bara la Afrika. Serikali ya Japan inapenda kukazia zaidi kuhusu ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa baada ya maambukizi ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, kwa kujikita katika maendeleo ya viwanda yenye ushirika na maendeleo fungamani ya binadamu Barani Afrika. Serikali ya Japan tangu mwaka 1993 imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo fungamani Barani Afrika.

Maendeleo fungamani ya binadamu ni muhimu sana Barani Afrika
Maendeleo fungamani ya binadamu ni muhimu sana Barani Afrika

Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshiriki muhimu sana katika mkutano huu, ili kukuza na kudumisha ukuaji wa uchumi imara, jumuishi na fungamani Barani Afrika. Mkutano huu umeratibiwa pamoja na Serikali ya Japan, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mshauri Maalum wa Afrika, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP, Kamisheni ya Umoja wa Afrika, AUC; pamoja na Benki ya Dunia, WB. Wajumbe wanashiriki mbashala mkutano huu na wengine wanatumia vyombo vya mawasiliano na mitandao ya kijamii. Hii ni nafasi kwa viongozi wakuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kukutana na wadau wa maendeleo kutoka Barani Afrika sanjari na wafanya biashara, ili kusaidia kuchochea mageuzi ya kiuchumi Barani Afrika, hasa mara baada ya mashambulizi ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 ambao umesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Benki ya Maendeleo ya Afrika inataka kujielekeza zaidi katika kukuza sekta binafsi inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa ukuaji wa uchumi Barani Afrika.

Japan imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo Barani Afrika.
Japan imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo Barani Afrika.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaojulikana kama “Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika” unaofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 Agosti 2022 Tunisia, nchini Tunis. Mkutano huo ni muhimu katika kupanga sera, mikakati ya ushirikiano na ajenda za maendeleo kati ya Japan na Afrika. Tanzania imekuwa ikifaidika na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za: miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji, elimu, afya na kilimo. Mkutano huu unafanyika Afrika kwa mara ya pili tangu mwaka 1993. Mara ya kwanza ulifanyika Jijini Nairobi, Kenya mwaka 2016. Katika Mkutano wa saba uliofanyika Yokohama, Japan mwaka 2019, Japan ilitenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni 20 kwa ajili ya kufanikisha malengo mbalimbali ya mendeleo katika kipindi cha miaka mitatu (2019 -2022).

Tunisia
26 August 2022, 15:29